You Can Win If You Want

Ijue nguvu ya imani

Nguvu ya imani

Nguvu ya imani ikiwa kubwa na matokeo ya mafanikio huwa makubwa zaidi, 

Ufunguo wa mafanikio makubwa au madogo katika maisha ya kila siku ni “imani “

Hali ya kuwa na uhakika wa kile unachotaka kufanya hata kabla hujaona matokeo ndio imani nyenyewe

Hutenda miujiza katika maisha ya kila siku , kitu cha msingi ni dhamira ya dhati kutoka moyoni

Hakuna muujiza katika mafanikio bali imani yako ndio muuzaji wako,” imani ikiwa kubwa na mafanikio huwa makubwa” 

Hivyo lazima uwe na imani na kile unachotaka kukitimiza kwanza na kuona kuwa itawezekana katika moyo wako hata kama kuna ugumu katika utekelezaji

Hatua ya kwanza katika mafanikio ya jambo lolote unalotaka kufanya ni kupandisha nguvu ya imani yako. 

Ijue nguvu ya imani

Nguvu ya imani inavyofanya kazi 

Hufungua mlango wa kwanza wa mafanikio na ndio  ufunguo sahihi wa kwanza unaofungua mlango wa nje wowote wa mafanikio

Nguvu hii huponya kila aina ya changamoto na matatizo katika mambo yote 

Kwahio katika jambo lolote lile kubwa au dogo, liwe rahisi au gumu kitu cha msingi ni kuwa lazima uanze na imani

Kabla hujafanya chochote kwanza amini, bila ya kusita sita au kuwa na hofu kutoka moyoni

“Dhamiria” na amini bila kusukumwa na sababu zingine zozote za nje wala kulazimishwa na mtu au mazingira bali imani ya dhati na kusimimia unachoamini  na unachotaka pekee

Ukiwa na nguvu kubwa ya imani husaidia kutochoka, Kutokukata tamaa na kutafuta njia kila wakati ya kufanikisha unachoamini

          “Penye nia pana njia

Hakuna mganga, hakuna nabii au shekhe yoyote ambae anaweza kukuponya kupitia dawa zake, maombi yake au dua zake

Zaidi huangalia kile unachoamini wewe kwanza kisha hutengeneza namna ya kukufanya uamini zaidi hata kama hakuna matokeo ya kweli

Ndio maana ukienda kanisani, msikitini au kwa mganga kitu ambacho atakusisitiza ni kuwa lazima uwe na imani kwenye  kile anachokufanyia

Japokuwa huwa hawafunguki moja kwa moja kuwa imani ndio tiba yako kwa sababu zao za kimaslahi

Wengi wamefungwa na upofu katika hili hivo kubaki kuwa watumwa wa mitume feki na waganga wa uongo

Hakuna mtu mwenye nguvu zaidi na upofu mkubwa kama mtu mwenye imani ya kitu fulani. 

Kitu cha kuzingatia 

Unachotakiwa ni kuanza na imani hata kabla hujaanza kufanya chochote kwa vitendo

Kama ukiona kuna dalili za kusita katika hilo basi ni bora uache kwanza mpaka pale utakapokuwa na uhakika “IMANI” kwenye  kile unachotaka kufanya

Kwasababu hutopata matokeo unayotaka kwa muda unaotaka zaidi ya mateso na changamoto zisizo za lazima. 

Mafanikio yanaambatana na nguvu ya imani 

mafanikio ni mchakato unaopaswa kufanyika katika hali ya kufurahika bila presha kubwa wala heka heka zisizo na maana yoyote

Kufanikiwa ni matokeo ya kile unachokiamini na mchakato katika njia sahihi, hivo jambo la kuzingatia siku zote ni IMANI yako.

Share this article
Shareable URL
Next Post

Alama za Nyakati Na Mafanikio

Acha Comment Yako

Read next

Huruhusiwi ku copy. Asante.