Kuzuia hali ya kukata tamaa ni kitu cha msingi na kinachosaidia kufikia malengo yoyote uliyonayo
Kukaa tamaa ni hali ambayo humkuta kila mtu hasa anapokuwa katika utekelezaji wa malengo makubwa
Kuna muda mambo huwa magumu sana na mtu huamua kuacha anachofanya
Hivo leo ntaongelea namna ya Kutokukata tamaa ili kufikia mafanikio kwa kukupa siri Moja kubwa
Katika harakati za maisha ya kila siku kuna muda tunakutana na changamoto za aina mbali mbali ambazo wakati mwingine hupelekea kukata tamaa na kuelemewa kwa mawazo na hata kufikiria kuacha kile tunachokipambania
Jifunze kuzuia hali ya kukata tamaa
Lakini unapaswa kupambana mpaka mwisho na kuona matunda ya jambo unalo pambania iwe elimu, biashara, kazi, kipaji au jambo lolote lile
Hakikisha kuwa haukubali kurudi nyuma mpaka pale utakapoona faida ya jasho lako.
Tafuta Sababu Ya Kuendelea na zuia hali ya kukata tamaa
Wakati mama yangu anapigania uhai wake wa mwisho aliniita na kuniambia
mwanangu kwa hali yangu ilivyo najua siwezi kupona na sina urithi mkubwa wa kukuachia zaidi ya neno moja tu kuwa “SOMA SANA” hata kama ndugu wasipokusaidia hakikisha unatafuta namna ya kusoma na usikate tamaa”.
Baada ya mama yangu kufariki kitu pekee nilichobakinacho ni Kauli yake,
Kauli ile ilijirudia akilini mwangu mara kwa mara na sikukubali kuacha masomo hata pale nilipokosa msaada kutoka ndugu wote
Niliamua kutafuta kazi ya kuniingizia kipato muda wa nje ya masomo na haikuwa rahisi kwani Ndio kwanza nilikuwa kidato cha tatu tu
Hali ilikuwa ngumu sana maana sikuwa na uhakika wa chakula, vifaa vya shule, ada wala mahala pa kuishi
Lakini kwasababu nilikuwa na nia ya dhati na hamasa ya maneno ya mama sikukubali kushindwa kabisa
Mambo yalikuwa magumu sana lakini nilijitahidi mapaka nikamaliza elimu ya chuo kikuu,
Ila mpaka sasanina amini kama yasingekuwa maneno ya mama basi kamwe nisingeweza kuendelea na masomo.
Angalia hamasa yako upya
Najua umekata tamaa na Huna nguvu za kusonga mbele, lakini nakuomba usiishie njiani
Jiulize kwanini ulianza kufanya unachokifanya na kwanini unataka kuacha ikiwa hujafikia lengo lako
Fikiria furaha utakayopata baada ya kutimiza malengo yako na majuto utakayopata kama ukiishia ulipo sasa, Ninaamini sio rahisi Ila unaweza
Hebu tamaza nyuma na kisha angalia hamasa yako upya, ongeza hamasa na simama katika mkazo wa nguvu na utaona namna utakavyopata matumaini mapya.
Pia soma mafanikio