You Can Win If You Want

Ukitafuta Maisha Usisahau Kuishi

picha kutoka pixabay

Ukitafuta Maisha Usisahu Kuishi maana yake ni rahisi tu kuwa changamoto za maisha haziishi na haijalishi unataka kutimiza nini au unafanya nini,

Au una majukumu makubwa kiasi gani na una hali ngumu vipi kitu cha kuzingatia ni kuwa lazima uishi maana muda wa kufa unahesabika

Tumekuja Duniani kuishi na kufurahia maisha yetu kwa namna yoyote, Mungu hakuumba mtu kwa lengo la kuja kuteseka kabisa ila mateso tunayatafutaga sisi wenyewe

Alituumba tuje kuishi na kuifurahia Dunia yake kwa namna kila mmoja atakavyoona bila kuvuka mipaka ya kiumbwaji na maagizo yake .

Maisha yana kila aina ya changamoto na hata siku moja usitarajie utamaliza shida zako zote ziwe kubwa au ndogo

Kadiri unavyopata na kuongeza kipato ndivyo ukubwa wa matatizo na changamoto huongezeka

Na kadiri unavyotatua changamoto ulizonazo au za nyuma ndivyo changamoto mpya huibuka tena

Na kila unapozidi kuchangamana na watu wa aina mbali mbali na kuongeza idadi ya wanao kuzunguka na changamoto pia huongezeka

Vile vile kwa kadiri maendeleo yavyoongezeka na kutanuka kila siku ndivyo mahitaji hutanuka na uhitaji wa vitu huongezeka kwa namna mbali mbali.

ukitafuta maisha usisahau kuishi

picha kutoka pixabay

Ukitafuta Maisha Usisahau Kuishi Kwa Sababu Chagamoto Huwa Haziishi

Hata uwe bingwa wa utatuzi wa changamoto kamwe hutoweza kumaliza kila kitu, iwe kifamilia ,kazi,biashara ,jamii au chagamoto zako binafsi

Haijalishi iwe changamoto ndogo au kubwa ,au changamoto ya pesa na pengine isiyo ya pesa na

Inaweza kuwa inayokuhusu wewe moja kwa moja au changamoro za watu wengine wa karibu yako.

Utamu wa maisha upo wenye changamoto kwa maana kuwa Dunia isingekuwa na ladha yoyote kama kila kitu kingekuwa kimenyooka

Yani zile heka heka za maisha ya kila siku ndio zinakamilisha maana ya Dunia kwa ujumla ila sio mateso!

Lakini pia kila mwanaadamu anapofanikiwa kutatua changamoto zake ndipo furaha yake huongezeka

Na changamoto ndio zinazofanya watu wapambane kila siku kwa njia zote kila wakati na kufanya mambo ya kila aina kwa lengo la kutatua shida zao

Yani hata maendeleo ya mtu jamii na Dunia wa ujumla huja kupitia uwepo wa changamoto na utatuzi wake kwa njia mbali mbali.

Uhitaji unavyoongezeka kupitia matamanio ya watu na changamoto huongezeka kila mmoja kwa namna yake na

Kila utatuzi unapopatikana hupelekea kuibuka kwa changamoto nyingine

Yani maisha hayatanyooka hata siku moja na changamoto zipo katika muundo wa duara yani kazi yake kubwa ni kuzunguka na kuanza upya kila inapotatuliwa

Kwenye kila ngazi kuanzia mtu mmoja mmoja mpaka nchi kwa ujuma

Uwe tajiri au masikini

Iwe ukoo au familia

Kazini umeajiriwa au hata ukijiajiri

Iwe unakaa peke yako na hata Umeoa au kuolewa NK.

Pia changamoto zipo kila mahala kila siku ,mwezi mwaka na hata miaka na kamwe haziwezi kuisha.

Hutoweza Kuishi Ukiendekeza Changamoto

Lazima ifike mahala ujue kuwa mzunguko wa maisha ndivyo ulivyo na kamwe huwezi badili asili yake

Bila kujali ukubwa wa kipato chako au ukamilifu wa maisha usitegemee kuishi bila heka heka za kila siku

Maisha yatakushangaza kila mara kwa kukupa sababu za kuumia na kulia kutokana na mzunguko wake wa kila siku.

Kwahio kama unataka kuishi na kufurahia maisha kitu cha kwanza ni KUKUBALI KUWA HUWEZI KUMALIZA CHANGAMOTO.

Ukisha kubali kuwa maisha na Dunia ndivyo ilivyo basi ni nusu ya tiba yao! yani asilimia hamsini za kumaliza changamoto ni kuzikubali kwanza

Ukizikubali tu basi tayari umesha zishinda hata kabla hujaanza kuzitatua kwa vitendo na ni moja ya silaha kubwa sana ya kuishi maisha ya amani hapa Duniani.

Aina Za Changamoto

Kwa upande wangu naweza kugawa changamoto katika aina kuu mbili kama

  • Changamoto ndogo ambazo tunakabiliana nazo kila siku na kila mara kila mahala na pia hazina madhara makubwa sana na zinatatulika mfano kuchelewa kufanya kitu, kupishana kauli na watu,kuharibu kitu au kazi ,kukosa mteja nk
  • Changamoto kubwa ambazo hutokea mara kadhaa na kuacha alama kubwa kwenye maisha ya mtu moja kwa moja kama kufukuzwa kazi,kufiwa,kufirisika,Talaka nk

Makundi Ya Changamoto

  • Changamoto za kazi
  • changamoto za familia
  • Changamoto za jamii
  • Changamoto za Elimu
  • Changamoto za uchumi
  • Changamoto za KIDINI
  • Changamoto za kitamaduni
  • Changamoto za siasa na uongozi kwa ujumla

Sababu Zinazopelekea Changamoto

Zifuatazo ni baadhi ya sababu zinazoweza kupelekea changamoto kati ya mtu watu hata jamii kwa ujumla

  • Utofauti wa tabia za watu, malengo na kusudi la uubwaji
  • Matamanio ya kila mmoja
  • Uhitaji na mahitaji ya kila siku
  • Sababu za kiasili

Faida Za Changamoto

  • Huogeza kiwango cha maendeleo na mafanikio
  • Huleta hamasa ya utafutaji
  • Huongeza ujasiri na ukomavu wa akili na mwili
  • Hufungulia fursa za maisha mengine
  • Hukamilisha maana nzima ya maisha na Dunia
  • Hutupa mafunzo na uzoefu wa maisha katika maeneo mbali mbali
  • Huongeza ubora na ubunifu wa jambo kupitia uzoefu na makosa

Madhara Ya Changamoto

  • Msongo wa mawazo
  • Hasira
  • Majuto na kufanya mambo nje ya uwezo
  • Kujidhuru au kudhuru wengine
  • Mumivu na kuhisi kuchanganyikiwa
  • Kutokueleweka na kupoteza mahusiao chanya kwa wanao kuzunguka
  • Kutengwa na kupoteza muelekeo wa maisha

Jinsi Ya Kupunguza Changamoto Na Kuishi Wakati Unatafuta Maisha

  1. Kubali changamoto haziepukiki

    Hivyo hatua ya kwanza ishi ukijua kuwa chohote utakachofanya lazima kina matatizo yake na hakuna kitu kilicho nyooka moja kwa moja

  2. Chagua changamoto unayoipenda na kuimudu

    Kama utachagua ndoa jua ina shida zake na ukiwa bila familia kuna shida zake au ukichagua kuajiriwa kuna matatizo yake na kujiajiri pia yapo mengi

  3. Chunguza Tabia

    Ya kila mtu ,kitu au mazingira uliyochagua kuchangamana nayo lazima ujue tabia au uhalisia wa mambo ili uweze kujifunza na kuzoea bila kuteseka

  4. Weka vipaombele

    Kupitia ulichochagua na kujua tabia yake sasa angalia kipi kitakuumiza kichwa na kipi sio muhimu, kipi chakuzingatia na kuanza nacho au kipi kifuate baadae ili kuepuka maumivu ya ziada

  5. Zoea na fanya kama sehemu ya maisha yako

    Unatakiwa kuzoea ulichochagua hata kama ni kibaya na kina kuumiza kitu cha msingi ni kuwa ulichagua kwa hiari yako na kama unaona kushindwa badili chaguo

  6. Tafuta njia ya kupunguza changamoto kila mara

    Hata kama umechagua unatakiwa pia ujaribu kuepeka madhara makubwa zaidi kwa kuangalia namna ya kuepuka kila wakati kitu kinachoweza kuepukika ili kupunguza maumivu na mateso

ukitafuta maisha usisahau kuishi

picha kutoka pixabay

Mambo Ya Kuzingatia Ili Kuishi Wakati Unatafuta Maisha

  • Jiweke wewe kwanza mbele kabla ya mtu mwingine na jipende zaidi kila mara
  • Weka malengo yanayofikika kulingana na uwezo wako kwanza
  • Usifikirie sana maisha yajayo wala kitu ambacho hukiwezi
  • Mara kwa mara fanya mambo unayoyapenda ndani ya uwezo wako
  • Tenga bajeti kwa ajili yako mwenyewe hata kama una familia ya kuhudumia
  • Fanya au acha ila kamwe usilalamike kwa chohote na ona maisha kama sehemu ya kufurahia
  • Fanya kilicho ndani ya uwezo wako tu iwe muda , pesa au kitu chochote bila kuumia wala kuwaza sana
  • Usiogope wengine watakuonaje kama umeshidwa kufanya kitu acha waamini wanachotaka kuamini na fanya unachokiweza tu
  • Epuka tamaa na kutaka kuridhisha watu kwa sababu hata wao hawata kuridhisha au kukuchagua wewe kabla yao wenyewe
  • Jipe furaha na ishi namna unataka bila kujali vikwazo vyovyote ulivyonavyo hata kama bado hujafikia mafanikio yoyote
  • Kumbuka kuna KUFA kwahio usiumizwe sana na mambo usiyoyaweza na fanya unachoweza kulingana na muda wako na rasilimali zako
  • Kataa kutumika kwa faida za watu wengine na ukikubali usilalamike kuonewa
  • Beba funzo tu kamwe usibebe majuto wala maumivu kwa ulichopoteza
  • Usikubali kuchangamana na watu wasio kupenda au kutovutiwa na wewe mara zote furahia maisha na watu wanaoona umuhimu wako
  • Weka mipaka ya maisha yako na simamia msimamo wako
  • Acha watu waamini wanachoamini na wewe usilazimishe wakuelewe.
Share this article
Shareable URL
Prev Post

Orodha Ya Biashara Ndogo

Next Post

Umasikini Huanzia Akilini

Comments 1

Acha Comment Yako

Read next

Huruhusiwi ku copy. Asante.