Utangulizi
Biashara ya Genge ni moja kati ya bidhaa muhimu sana katika matumizi ya kila siku watu kwa wote,
Kwa maana kuwa kila mmoja katika mlo wake wa siku nzima huhusisha mahitaji ya bidhaa za gengeni kama nyanya, kitunguu,mboga mboga,Ndimu nk
Biashara ya genge inaweza kuhusisha pia uuzaji wa mchanganyiko wa matunda aina mbalimbali
Ukiondoa mboga mboga kama mchicha ,matembele,spinachi,sukuma wiki, kisamvu na nyinginezo
Pia unaweza kuuza Samaki, dagaa, viungo vya mboga na vitu vingine vingi kulingana na uhitaji wa watu wa eneo lako na ukubwa wa mtaji.

Biashara hii unaweza kuanza kwa mtaji kidogo sana na kupata faida kubwa kwasababu ni bidhaa ambazo faida inajizalisha
Kujua jinsi ya kuanza biashara bila mtaji kabisa soma hapa
Uzuri ni kuwa soko lake lipo inategemea na ushindani wa eneo na ubunifu wa ziada bila kusahau kipato cha watu wa eneo hilo
Biashara ya genge inaweza kufanyika katika namna tofauti tofauti kama :
Namna Mbali mbali Za Kufanya Biashara Ya Genge
- Kutembeza
- Mtandaoni ( derively)
- Kibandani ( eneo moja)
- Sokoni
- Shambani (Bustanini) nk
Kutembeza
Kama huna aibu unaweza anza kwa kutembeza mahitaji muhimu ya bidhaa za genge mtaani , nenda sokoni chagua baadhi ya vitu vichache kama nyanya na kitunguu ,hoho nk
Pita nyumba hadi nyumba tangaza bidhaa zako kwa ushawishi mkubwa ,
Unaweza tembeza kwa mguu, toroli au hata Baiskeli , inategemea na kile kilicho ndani ya uwezo wako!
Mtaji wa kuanza nao hata elfu 10000 au zaidi inatosha kama utaenda kununua sokoni kwa bei ya jumla na anza vitu vichache tu
Ikiwa huna mtaji kabisa ongea na wenye bidhaa uliowazoea na omba wakupe baadhi ya vitu utembeze
Kisha ongeza bei kidogo tu mfano kama nyanya ni 500 fungu wewe uza 600 au zaidi inategemea na kipato cha wanunuaji
Ukimaliza rudhisha mtaji wa watu na wewe baki na faida yako , kisha endelea na utaratibu huo mpaka mtaji wako utakapokuwa
Hapo zingatia Umanifu wa hali ya juu, kumbuka uaminifu ni silaha kubwa sana.
Mtandaoni ( derively)
Maisha yamehamia mitandaoni kwasasa, hivyo anza kujitangaza kisomi kuwa unauza bidhaa za genge
Weka picha nzuri zenye uhalisia , anza na watu wa maeno ya karibu kupunguza gharama za nauli
Ikiwa utapata mteja unaweza mpelekea mahitaji yake kwa nauli yake kama ni mbali na pia unaweza ongeza bei kidogo
Zingatia ubora wa bidhaa zako na wingi wa bidhaa anazotaka mteja , ndio silaha ya biashara ya genge
Mtaji unategemea na kiwango ulichonacho na hata kama huna fanya kuongea na wafanyabiashara wa bidhaa za genge
Hakuna anaekataa kutoa bidhaa kwa mali kauli kama ana uhakika wa kulipwa maana hata yeye lengo lake ni kuuza!
Au fanya kwa namna nyingine yoyote upendayo wewe binafsi kwenye mawazo yako na rahisi kwako jambo la msingi ni kufanya mauzo!
Kibandani
Unaweza pia kufanya biashara ya genge kwa kutafuta eneo moja lenye muingiliano wa watu wengi
Unaweza kuanza na kibanda cha miti na mbao, fremu ndogo au mahala popote rahisi kulingana na mtaji wako
Pia kama huna vyote au uwezo wa kupata eneo basi fanya hapo hapo nje ya nyumba unayokaa
Weka ,meza ndogo na panga bidhaa zako!
Sokoni
Unaweza pia kuuza bidhaa za genge sokoni kwa bei ya jumla au reja reja ukaanza kwa mtaji au hata bila mtaji
Ukiwa na mtaji, kodi eneo kwa bei rafiki anza na bidhaa rahisi kuuzika kama nyanya na vituguu au chagua bidhaa ya aina moja tu
Mtaji unaweza kuwa angalau sio chini ya laki 150000 laki na nusu maana baadhi ya maeneo hukodishwa kuanzia elfu 20000 kwa mwezi
Unaweza anza na malipo ya miezi mitatu au zaidi, pia gharama za kodi zinaweza kuzidi hapo kutegemea na aina ya soko
Uza kwa jumla au reja reja vile upendavyo na kulingana na aina ya soko ulipo mfano wa Dar es salaam soko la jumla ni kama
Temeke stirio, Vetenari, Kariakoo,Tandika,Buguruni sokoni na kwingineko masoko yote haya unaweza uza kwa jumla au reja reja
Kuna wakulima na madalali wengi huleta mahitaji ya bidhaa za genge sokoni na mara kadhaa huwapa wauzaji kwa mali kauli kisha jioni hupitia mauzo.
Ukishidwa kabisa kupata eneo basi kuwa dalali wa bidhaa hapo hapo sokoni kwanza baada ya kupata uzoefu na watu utachukua eneo lako.
Shambani ( Bustanini)
Hapa sasa unaweza kulima mboga mboga au bidhaa nyingine za genge kutegemea ukubwa wa eneo lako
Vile vile ukubwa wa mtaji wako, kumbuka sio lazima uwe kijijini sana hata mjini kama una eneo unaweza panda mboga
Vile vile bidhaa hizi hazitaki muda mrefu sana kuvunwa unaweza anza na bidhaa zinazochukua muda mfupi
Kisha ukafanya mauzo yako hapo hapo shambani au kwenye bustani yako yaani wateja watakufuta
Au hata unaweza kuuza kwa njia nyingine upendayo.

Vilevile Biashara ya Genge unaweza kufanya katika muundo wa
- Kisasa au
- Kizamani
Yote ni namna ya kuipa thamani biashara yako na kupunguza hasara bila kusahau kuongeza mauzo na kuteka wateja.
Mtaji Wa Kuanza Biashara Ya Genge
Mtaji wa biashara ya genge unategemea namna unavyotaka kufanya biashara yako, kwangu mimi hata bila mtaji kabisa inawezekana
Na unaweza anza kwa mtaji kuanzia elfu tano na kuendelea kiwnago unachotaka mwenyewe
Jambo la kuzingatia ni wateja maana sio kwamba ukiwa na mtaji mkubwa ndio utauza sana!
Mauzo yanategemea sababu nyingi sana nje ya mtaji ulionao. Kumbuka kuna tofauti kubwa kati ya mtaji mkubwa na mauzo mengi
Japokuwa mtaji mkubwa ni moja kati ya sababu inayopelekea kuongeza mauzo na kupata faida nzuri,
Lakini kumbuka kuwa biashara ya genge ina faida na hasara kubwa kama ndio kwanza unaanza na huna wateja
Kwahio fanya uchunguzi na anza na aina ya uuzaji unayotaka kisha chagua kiasi cha kuanza nacho.
Changamoto Za Biashara Ya Genge Na Jinsi Ya Kuzikabili
Hakuna kitu kisicho na changamoto kabisa japokuwa changamoto huzidiana katika biashara na hata maisha
Moja kati ya changamoto kubwa sana ya genge ni bidhaa kuharibika au kuoza kabisa
Kwa sababu bidhaa nyingi za genge ni zile za muda mfupi kama mboga mboga za majani, nyanya , matunda na hata vingine
Hasa kama ndio unaanza na hujazoeleka sana wala huna wateja wa uhakika
Hivyo basi kuweza kukabiliana na changamoto hii unaweza kufanya hivi
- Anza na bidhaa chache
- Uza bidhaa zisizoharibika haraka
- Nunua friji la kutunzia bidhaa kama una uwezo
- Hakikisha una tanua soko lako kwa nguvu na kutafuta wateja mara mara usitegemee wateja wale wale
- Uza kwa punguzo la bei ila zingatia gharama ulizonunulia
- Kopesha bidhaa ikiwa zinakaribia kuharibika
- Ubunifu wa ziada ni muhimu kuteka wateja
- Tafuta eneo lenye washindaji wachache ili kupunguza ushindaji

Mambo Ya Kuzingatia Kwenye Biashara Ya Genge
- Ubunifu
Hii ni silaha ya kwanza kwenye biashara ya genge , angalia namna ya kuteka wateja warudi mara kwa mara na kufanya mauzo kila siku
- Uza vitu vinavyotoka sana
Unaweza weka vitu vya ziada lakini zingatia mahitaji ya watu ya kila siku na mara kwa mara
- Bei nzuri
Panga bei kulingana na kipato cha wanunuzi na usiweke tamaa ya mfanikio ya haraka
- Kauli nzuri
Zingatia kauli nzuri kwa wateja kumbuka mteja ni mfamle na lazima umnyenyekee
- Uchaguzi wa eneo sahihi
Jitahidi kuchagua eneo lenye mzunguko wa watu wengi sana maana watu ndio wateja wenyewe
- Elimu ya genge
Uliza wajuzi na wazoefu wakupe elimu kabla hujafanya uwekezaji wowote pia kuwa mdadisi mara kwa mara
- Nidhamu ya pesa
Bila nidhamu katika matumizi ya pesa itakua ngumu sana kuendesha na kuendeleza biashara ya genge
- Bidhaa nzuri zenye kuvutia
Epuka kuuza vitu vilivyooza kabisa au kuharibika kwa lengo la kupata faida kubwa, uza vitu sahihi na vinavyofaa kwa matumzi.
- Mtangazo
Biashara ni matangazo hata kama unafanya nje ya mlango wako hakikisha kuwa watu wanajua unachouza
Hatua Za Kuanzisha Biashara Ya Genge
- Anza na uchunguzi na udadisi wa kila kitu kuanzia soko mpaka changamoto
- Kisha andaa mpango wa biashara ambao unatoa dira ya biashara nzima kuanzia mwanzo hadi mwisho
- Halafu fanya usajili wa biashara japokuwa sio lazima sana kama ndio unaanza na huna eneo rasmi
- Na mwisho maandalizi ya eneo la kuuzia kama utafanya katika eneo moja.
Hitimisho
Biashara hii kama zilivyo biashara nyingine zinahitaji moyo wa dhati , nia na mapenzi bila kusahau kujituma sana na uvumilivu wa hali ya juu
Kumbuka kuna nyakati bidhaa zinaweza kupatikana kwa urahisi na zipo nyakati bidhaa hupotea sokoni
Hivyo bei zinaweza kupanda au kushuka sana ndio maana ni lazima kufanya uchunguzi kabla ya kuanza biashara yoyote .