You Can Win If You Want

Jinsi Ya kukuza Mtaji Wa Biashara

jinsi ya kukuza mtaji wa biashara

Utangulizi

Kukuza mtaji wa biashara yoyote ni kitu cha msingi na lazima ili biashara ipate uhai wa kukua na kuendelea

Hakuna biashara inayolenga kupata hasara wala kuishia njiani kwa namna yoyote ile , ila changamoto huweza kupelekea hayo

Changamoto za biashara ni adui mkubwa sana kwa wafanyabishara wengi, japokuwa mara kadhaa huwa haziepukiki

Ukitaka kuzijua changamoto za biashara na jinsi ya kukabiliana nazo soma hapa.

Kuna watu huanza biashara bila mitaji kabisa, wapo wanaoanza kwa mitaji kidogo na wale ambao huanza wakiwa na kila kitu

Lengo lao wote kwa pamoja ni kupata faida, kuongeza mauzo na mwisho kabisa kukuza mitaji yao na kufikia malengo makubwa.

Namna Ya Kukuza Mtaji Wa Biashara

Hivyo basi tukiondoa tofauti zote za ukubwa na udogo wa awali na kubaki kwenye lengo la kukuza mtaji ,njia zifuatazo husaidia zaidi.

kukuza mtaji wa biashara
Photo by Ylanite Koppens on Pexels.com

  1. Ongeza kiwango cha mauzo

    Ili kupata faida kubwa lazima ufanye mauzo mengi ili mzunguko wa pesa uongezeke na kadiri mzunguko unavyoongezeka ndivyo mtaji huongezeka

  2. Tafuta wawekezaji

    Kuna watu wengi wana pesa na hutafuta biashara za wengine kuwekeza pesa zao kwa lengo la kuzalisha faida zaidi

  3. Tumia akiba yako

    Kama una pesa zako binafsi za pembeni usiogope kuwekeza kwenye biashara yako kwanza kabla ya matumizi mengine binafsi

  4. Omba msaada kwa watu wa karibu

    Endapo una ndugu jamaa au marafiki usiogope kuomba msaada wa namna yoyote uweze kukuza mtaji wa biashara yako kwanza

  5. Tafuta mikopo

    kuna tasisi mbali mbali zinazokopesha wafanyabiashara wanaotaka kukuza mitaji yao ikiwa wamekidhi vigezo kuanzia ngazi ya mitaani mpaka Benki mbali mbali

  6. Shirikiana na wafanyabiashara wenzako

    Wale wanaofanya biashara kama yako jenga uhusiano mzuri kwa lengo la kusaidiana pale unapokwama bidhaa kwako unaenda kuchukua kwake

  7. Tafuta mtaji wa ubia

    Kuna wabia wengi ambao huingia ubia na wafanyabiashara kati ya kampuni na kampuni au kampuni na biashara fulani kwa lengo la kusaidiana

  8. Rudisha faida kwenye mtaji

    Kila unapopata faida tenga fungu kubwa lirudishe katika mtaji kwanza kabla ya matumizi mengine kwa kuangalia mapungufu yaliyopo mara kwa mara

  9. Jiunge na vikundi vya watu wengi

    Ambapo watu wengi zaidi huchangiana pesa kidogo kidogo na kuwekeza kwa mfanyabiashara mfano vikundi mbalimbali kama vikoba au mifuko ya wajasiriamali

  10. Jenga uhisiano bora na wafanyabiashara wa jumla

    Sehemu ambazo huwa unachukulia mzigo jenga mazoea chanya ya kibiashara ili uweze uchukua bidhaa kwa mali kauli mara kwa mara

  11. Fanya biashara ndani ya biashara yako

    Ongeza aina nyingine ya huduma au bidhaa ndani ya biashara yako ili kutanua mauzo na kusaidia kupunguza baadhi matumizi kutoka kwenye biashara kuu.

Mambo Ya Kuzingatia Ili Kukuza Mtaji Wa Biashara

Unapokuwa katika jitihada za kukuza mtaji wa biashara yako bila kujali ukubwa au udogo wake lazima pia uzingatie mambo yafuatayo:

  1. Mpango wa biashara , huu ni lazima kwenye biashara maana unatoa dira ya biashara mwanga na mbinu za kupambania malengo ya biashara
  2. Nidhamu ya matumizi ya pesa , kumbuka bila kuwa na udhibiti wa matumizi sahihi ya pesa maana yake ni ngumu sana kuweza kuongeza mzunguko wa mauzo ya biashara
  3. Bajeti sahihi ya biashara na matumizi ya kila siku kwa kuzingatia kupunguza matumizi na gharama za uendeshaji mara kwa mara
  4. Jitihada binafsi, kumbuka mtu pekee ambae anaweza kunusuru biashara yako ni wewe mwenyewe kwahio lazima kuzidisha jitihada na hamasa kila siku
  5. Uhusiano bora na watu kuanzia wateja,wafanyabiashara wenzako mpaka jamii nzima kwa ujumla wake.

Hitimisho

Mafanikio ya kukuza mtaji pia yanahitaji subra na uvumilivu wa hali ya juu sana kwasababu biashara hukua katika misingi yake

Hivyo inataka muda kuweza kusimama imara na kuyaona mafanikio ya kweli kwa maana hio lazima subra iwe juu zaidi na kuepuka kukata tamaa .

Kusoma mbinu za kupata msaada wa mtaji na wawekezaji soma hapa.

Share this article
Shareable URL
Prev Post

Siri Za Kufanya Biashara Bila Mtaji

Next Post

Wazo La Biashara Ya Kulea Wazee Na Watu Wazima

Acha Comment Yako

Read next

Huruhusiwi ku copy. Asante.