You Can Win If You Want

Mbinu Za Kuongeza Mauzo Ya Biashara

kuongeza mauzo ya biashara

Utangulizi

Kuongeza mauzo ya biashara ndio lengo kuu la kila mfanyabiashara kwa maana ya kuongeza mzunguko wa pesa katika biashara

Lakini pia kuongeza mauzo ya biashara ndio chanzo kikubwa cha kupata faida na mafanikio ya biashara yoyote

Mzunguko mzuri wa pesa kwenye biashara ndio silaha ya kwanza ya uhai wa biashara yoyote mahala popote.

Mbinu za kuongeza mauzo ya biashara
Photo by Monstera Production on Pexels.com

Haijalishi ukubwa au udogo wa biashara kitu cha msingi ni kuhakikisha biashara inapata uhai kupitia mauzo yake

Kuna ambao huanza kwa mitaji kidogo, mitaji mikubwa au hata bila mitaji kabisa lakini wote mwisho wa lengo ni kuongeza mauzo.

Njia Za Kuongeza Mauzo Ya Biashara

Kama unapata changamoto za mauzo kwenye biashara yako na unatamani kuongeza mauzo na mzungoko wa pesa basi jaribu kutumia njia hizi

  • Boresha matangazo, sio kila tangazo linaweza kukupa mteja! tumia bidhaa au huduma inayopendwa zaidi kwenye matangazo unayofanya ili kuvuta wateja watakaonunua bidhaa na huduma zingine.
Jinsi ya kuboresha matangazo ili kupata wateja zaidi
  1. Fanya biashara kwa chapa (brand) usifanye biashara kizamani badala yake ifanyie brand kuanzia logo,ofisi,matangazo na hata vifungashio ili kuongeza mvuto
  2. Jitangaze kisasa , tumia mitandao kurahisisha kufikia watu wengi mfano facebook na mitandao mingine badala ya kungoja wateja wakutafute
  3. Tenga bajeti ya matangazo, matangazo ni sehemu ya bajeti ya lazima kwenye biashara kwahio tenga fungu kubwa kwa ajili ya matangazo . NK
  • Ongeza ubunifu , tafuta silaha ambayo itamfanya mteja aache kununua kwa mtu mwingine na aje kununua kwako mfano zawadi ndogo kwa wateja, nyoongeza, ladha au hata harufu ya bidhaa zako.
  • Uza bidhaa au huduma za ziada, mfano kama una duka la uwakala wa huduma za kifedha weka na huduma ya kusajili laini au kuuza vocha
  • Weka mvuto kwenye biashara mfano kama unauza bar weka wahudumu wenye sura na maumbile yenye kuvutia , au una ofisi weka msichana mdogo mapokezi NK.
  • Zingatia bei kulingana na kipato cha wateja, mazingira na ubora wa bidhaa au huduma yako
  • Uza kwa ofa, wateja wengi hufurahia sana wakiona kuna ofa mblimbali na hii ni moja kati ya siri kubwa sana kwenye biashara kama unataka kuuza kwa wingi.
Vitu Vya Ofa Vinavyoongeza Mvuto Wa Mauzo
  • Ofa ya bei , hapa weka punguzo kidogo la bei kwenye huduma au bidhaa unayouza
  • Vitu vya mafungu mfano kuanzia viwili au vitatu kwa bei ya chini, unaweza kupanga bidhaa au huduma zako kwa mafungu na kuweka bei ya chini kidogo kwa atakae nunua kwa mafungu na bei ya juu kwa atakae nunua kitu kimoja
  • Vitu vya bure vya ziada mfano nunua tatu upate 1 bure
  • Huduma za bure kabisa mfano Tunatoa USHAURI BURE au ULIZA MASWALI BURE hii italeta watu wengi sana na baadae utawageuza kuwa wateja kwenye bidhaa au huduma yako
  • Vitu vya kujaribu au kuonja ,hii husaidia wateja wenye mashaka kwenye bidhaa au huduma na humfanya arahisishe maamuzi yake
  • Vitu vya Nyoongeza, muongezee mteja zaidi akinunua kitu mfano nyama nusu mpe nyoongeza ya finyango(vipande) mbili za nyama.
mbinu za kuongeza mauzo
Photo by Mubashir Hussain on Pexels.com

Mbinu Nyingine Za Kuongeza Mauzo Ya Biashara

  1. Rahisisha huduma kumfikia mteja kwa urahisi zaidi mfano derivery
  2. Onesha kuwa umebobea kwenye kitu unachofanya na una uhakika kwenye kile unachouza
  3. Teka hisia za mteja kabla na baada ya kuingia eneo la biashara yako
  4. Rahisisha njia za malipo hasa kwa wafanya biashara wa mitandaoni yaani mfanye mteja aweze kulipa kwa njia rahisi kwake
  5. Zingatia kauli nzuri hasa unapoongea na mteja na shikilia kauli ya mteja ni mfalme
  6. Uza bidhaa au huduma zenye uhitaji kulingana na aina ya wateja ulionao
  7. Boresha ubora wa huduma na bidhaa unazouza kwa kuzingatia mirejesho ya wateja na ifanyie kazi mara kwa mara
  8. Jitahidi kuwa muaminifu ,mkweli na muwazi pia punguza ujanja ujanja kwenye biashara hasa ujanja usio na faida ya kumbakiza mteja
  9. Zidisha ukarimu kwa wateja wote
  10. Hudhuria mikutano na semia za mauzo
  11. Wape motisha wafanyakazi mara kwa mara kama unao
  12. Jifunze mara kwa mara maarifa mapya kuhusu biashara unayofanya.

Hatua Za Kuongeza Mauzo Ya Biashara

  1. Fanya uchunguzi wa soko

    Elewa aina ya wateja na uhitaji wao kisha chunguza kipato cha wateja unaotaka na mazingira unayofanyia biashara pia chunguza washindani wako na mbinu zao

  2. Tengeneza mpango wa mauzo

    Mpango wa mauzo hutoa ramani nzima ya mauzo ya biashara yako kuanzia mwanzo mpaka mwisho bila kusahau njia zote na ubunifu wa ziada

  3. Andaa silaha yao

    Baada ya kufanya uchunguzi wa uhitaji na udhaifu wa washindani ,unapaswa kujua kipi sasa utafanya ili kuziba pengo na kuvuta wateja waje kwako

  4. Tenga bajeti nzuri ya matangazo

    Siku zote biashara ni matangazo na wateja hununua zaidi stori kuliko ubora wenyewe yaani mteja hununua zaidi anachokiona au kusikia

  5. Mfanye mteja arudi kwako

    Hii ni hatua ya mwisho kwa kila mteja jitahidi kila anapopata uhitaji wakati mwingine basi akukumbuke wewe , huduma au bidhaa yako na alete wateja wengine.

Namna Ya Kuteka Hisia Za Mteja Ili arudi Kwako Na Kuongeza Mauzo Zaidi

  • Mpe ukaribisho wa bashasha na tabasamu kubwa
  • Msikilize shida yake na mpe ushauri kulingana na uhitaji wake kwanza
  • Msaidie uchaguzi wa bidhaa au huduma anayotaka
  • Onesha kuguswa na changamoto yake kuliko anavyoonesha kuguswa yeye
  • Muoneshe msisitizo wa ubora wa huduma au bidhaa zako ikibidi kwa mifano hai ila usidanganye kupitiliza
  • Jiamini na furahia wakati unampa huduma au bidhaa
  • Muoneshe na mshawishi anunue bidhaa au huduma nyingine zaidi
  • Muhudumie kwa namna ya zaidi ya alivyotarajia
  • Muage kwa namna ya ushawishi wa yeye kurudi tena siku nyingine.
njia za kuongeza mauzo ya biashara
Photo by RDNE Stock project on Pexels.com

Hitimisho Na Mambo Ya Kuepuka Unapotaka Kuongeza Mauzo Ya Biashara

  • Imani za kishirikina ,uchawi na waganga
  • Kumsema vibaya mshindani wako mbele za wateja
  • Ugomvi na washindani wako au majirani
  • Kisirani na kumfanya mteja kujiona kama anakulazimisha kununua kwako
  • Haraka na kutaka mafanikio ya njia za mkato hasa kuchakachua bidhaa na huduma kwa sababu zozote zile.
Share this article
Shareable URL
Prev Post

Wazo La Biashara Ya Udobi ( Dry cleaning and laundry)

Next Post

Wazo La Biashara Ya Viazi Na Mihogo Ya Kukaanga

Acha Comment Yako

Read next

Huruhusiwi ku copy. Asante.