You Can Win If You Want

Uoga Hauzuii Kifo, Unazuia Kuishi

Haijalishi utaogopa kiasi gani kumbuka kuwa muda wa kufa ukifika utakufa tu

Hata kama utafanya mangapi yawe mazuri au mabaya bado hayawezi kuzuia kifo chako

Kadiri unavyo ogopa kifo ndio hofu huweza kusababisha kukifikia mapema pengine hata kabla ya muda!

Lakini wakati huohuo kumbuka kuwa uoga wako unaweza kuzuia wewe kuishi!

Kuishi maisha ya furaha na kusudi la kuumbwa kwako

Kuishi maisha ya amani na kuvuka vikwazo bila pingamizi

Kuishi maisha yaliyo sheheni maana halisi ya maisha yako

Uoga unaweza kukufanya ushindwe kabisa kuishi na ukakiharakisha kifo ambacho hakihitaji jitihada za lazima kufikiwa…

Uoga wa kushindwa, uoga wa kuchekwa, kuharibu, uoga wa kufirisika na hata kupoteza

Bila kusahau uoga wa kusalitiwa, uoga wa kukataliwa na hata kukimbiwa

Vyote hivyo vinashinikizwa na hofu ya aibu ambayo unaitengeneza kwenye akili hata kabla ya kutokea!

Kumbuka kuwa uoga sio jambo kubwa kama unavyolichukulia akilini

Uoga ni hali ambayo unaizalisha wewe mwenyewe kupitia hofu isiyokuwepo..

Uoga ni adui mkubwa sana unae andamana nae kila wakati

Amua leo kumvua na kumpinga huyo uoga wako ambae anakushawishi kwa nguvu zote urudi nyuma kila mara

Kumbuka uoga hautazuia kifo chako bali uoga una kuzuia kuishi maisha yako.

Share this article
Shareable URL
Prev Post

Wazo La Biashara Ya Kuuza Smoothie (Juice Laini)

Acha Comment Yako

Read next

Huruhusiwi ku copy. Asante.