
Moja kati ya kanuni kubwa zaidi ya kupata amani ya maisha ni kusamehe kwa moyo mmoja
Haijalishi umekosewa kiasi gani huko nyumba, leo au wakati ujao..
Bila kujali maumivu, mateso na hasara ulizopata samehe kwa moyo mmoja
Usiweke vitu moyoni wakati huo huo unateseka kwa mambo ambayo hayana faida tena
Usibebe mzigo wa mateso kwa vitu ambavyo havina maana tena
Usishindwe kusonga mbele kwa sababu ya mambo yasiyo na tija yoyote
Acha maisha mengine yaendelee na fanya kama hakija tokea kitu kabisa
Wakati mwingine mzigo wa kumbu kumbu na visasi Ndio chanzo cha mateso na maumivu kwenye maisha yako
Kukumbatia mambo yaliyopita huweza kuwa chanzo kikubwa cha kikwazo kwenye mafanikio yako
Sio lazima uombwe msahama ndio usamehe, kumbuka sio wote huhesabu kosa palipo na kosa,
Kuna mwingine akikukosea kwake ndio faraja yake ilipo
Kwanini ujiumize kwa sababu ya mtu au watu ambao hawaoni tatizo kwenye tatizo?
SAMEHE, sahau na endelea na maisha yako mengine
Usimchukie mtu kwa sababu zozote zile wala usilipize ubaya wowote
Acha hatma Iamue yenyewe..
Usipoteze muda wako kuweka vitu ambavyo vitakujazia nafasi ya kupokea yaliyo bora zaidi
Makosa ya zamani, ya sasa na hata yajayo hayapaswi kuishi ndani ya akili yako
Tumia muda wako kuanzia sasa kuachilia visasi, chuki na hasira zote ulizonazo na kamwe usiruhusu kubeba chuki zijazo kwenye moyo wako tena.
Samehe, sahau na anza upya maisha yako.