Utangulizi
Biashara ya sandwiches inaweza kuwa biashara ngeni kiasi kwa wakazi wengi wa Tanzania hususani maeneo ya mikoa nje ya Dar es salaam
Lakini ni biashara nzuri sana na rahisi zaidi kufanyika hata kwa wasio na mtaji mkubwa sana au wenye mtaji mkubwa
Pia haihitaji ujuzi mkubwa sana wa upishi, kwani ni rahisi sana mtu yoyote kutengeneza sandwiches.
Biashara hii ya sandwiches ni nzuri mno kwa upande wa kutengeneza faida na soko lake lipo wazi na hakuna ushindaji
Ukweli ni kuwa sandwiches kama ilivyo burger na pizza, ni vyakula vigeni kiasi kwa watanzania walio wengi ,
Kutokana na tamaduni za vyakula vya Tanzania vilivyo zoeleka zaidi toka enzi na enzi za mababu zetu.
Hivyo basi vyakula hivi vigeni pia ni muhimu sana hasa kutokana na muingiliano mkubwa wa watu wa mataifa mengine,
Bila kusahau hatupaswi kuzoea maisha ya aina moja au kula vyakula vile vile kila siku pasipo na kuchanganya aina nyingine.
Sandwiches huliwa zaidi kama kitafunwa na wengine hupendelea wakati wa jioni kama kiburudisho au chakula kamili.

Sandwiches Ni Nini?
Neno sandwiches lisikuchanganye kabisa na kuhisi ni kitu kikubwa sana cha kifahari au kitajiri kupitiliza
Sandwiches ni mkate wa kawaida tu ,huu huu unao ujua uuzwao dukani kwa mangi (yaweza kuwa skonzi au slaces)
Ndio , ni mkate huo ambao unauzwa kuanzia elfu moja au chini ya hapo kwenye maduka au mitaani na hata sokoni.
Tofauti ni kuwa ili mkate huo uitwe sandwiches basi huongezewa udambwi udambwi au naksh naksh kufanya upate ladha zaidi,
Vitu kama nyama ,kuku ,mayai,mboga mboga au salad na vingine vingi huongezewa ili kufanya mkate upate ladha nzuri.
Kuna aina nyingi sana za sandwiches kutokana na uhitaji wa mlaji au tuseme tamaduni za nchi mbali mbali,
Ila sandwiches maarufu zaidi ni zile za nyama ,kuku na salad mbali mbali mbali.
Biashara ya sandwiches ni rahisi sana hata kufanyia nyumbani au mahala popote pale ambapo kuna wateja,
Mara nyingi vyakula vya aina hii hupendwa zaidi na wanafunzi wa vyuo maeneo ya mijini na wafanyakazi wa ofisi mbali mbali
Pia waweza kuchanganya biashara ya sandwiches na biashara ya pizza au burger na hata zote kwa pamoja
Kwani ni aina ya vyakula vinavyoendana na hata watumiaji wa vyakula hivi hupendelea aina zote hizi kwa pamoja.
Mahitaji Ya Biashara Ya Sandwiches
Kama tulivyoona awali kuwa biashara hii inaweza kufanywa katika muundo au mtindo wowote kulingana na mfanya biashara,
Inawezekana kufanyia nyumbani, barabarani au hata kwenye eneo maalumu na fremu au kibandani
Hivyo mahitaji yake pia huweza kutofautiana kati ya mfanya biashara mmoja na mwingine au kiwango cha malengo.
Hapa tutaangalia mahitaji ya msingi zaidi kama ifuatavyo:
- Mkate wa kawaida ( inaweza kuwa skonzi au slesi)
- Nyama ya kuku, mayai au nyama ya kawaida (nyama sio ya kusagwa)
- Nyanya na vitunguu ( pia sio lazima)
- Majani ya salad au tango
- Chees ( sio lazima kwa sandwiches zote)
- Zaituni ( pia sio lazima kwa baadhi ya sandwiches)
- Mashine ya kutengenezea sandwiche ( sio lazima) kama huna unaweza kutumia kikaangio cha chapati cha kawaida
- Jiko (hufaa zaidi la umeme au gas kwa ajili ya kutengeneza haraka mteja anapotokea)
- Vifungashio
- Kisu
- Sahani
- Eneo ( pamoja na viti ,meza etc) kwa wanao kodi fremu NK
ZINGATIA: Mahitaji haya ni yale ya msingi zaidi na huweza kupungua au kuzidi kulingana na mfanya biashara husika.

Aina Nyingine Za Sandwiches
kuna aina nyingi sana za sandwiches na sio zote zinataka nyama wala kuku au mayai kabisa.
Zipo sandwiches za salad pekee kama nyanya ,vitunguu na hata majani kama lettus tu na wengine huweka vitu kama,
Zaituni pekee , chees au kitu kingine chohote kile muhimu ni mkate lazima uwe na vikorombwezo na sio mkate mtupu.
Wapo ambao hutumia chapati badala ya mkate na wengine hutumia chapati nyeupe (isiyo na mafuta kabisa)
Bila kusahau wengine huweka chips chombeza kidogo kwenye mchanganyo wa sandwiches zao na wengine hawapendi kabisa
Kila mmoja ana mapenzi yake na hata wewe unaweza kubuni aina yako ya sandwiches kulingana na mapenzi ya wateja wako.
Biashara ya Sandwiches Kwa Wasio Na Mitaji Mikubwa
Inawezekana kabisa kufanya biashara hii pasi na uhitaji wa mtaji mkubwa sana, muhimu ni wateja tu
Biashara yoyote ile kitu cha msingi zaidi ni uwepo wa wateja kabla ya kuwaza ukubwa wa mtaji au vitu
Kwani wateja ndio silaha ya biashara , unaweza kuwa na mtaji mkubwa sana na bado usiuze kabisa biashara yako.
Hivyo kama una uhakika wa wateja wanaoweza kununua sandwiches ,unaweza kuanza hata nyumbani kwako!
Vifaa vyote vya kutengeneza sandwiches hupatikana nyumbani tukiondoa mashine ambayo sio muhimu sana.
Anza na sandwiche za kawaida tu ambazo hazina ulazima wa kuku wala nyama kama huna uwezo huo kwanza,
Kisha baada ya kuzoea na kupata wateja wa uhakika kwa baadae unaweza kukuza na kutanua biashara au kupitia aina nyingine za sandwiches.
Mtaji wa elfu 15 tu unatosha au hata kubaki kwa anaeanza biashara nyumbani kwake kwa vifaa vya nyumbani.
Biashara Ya Sandwiches Kwa Wenye Mitaji Mikubwa
Kama una mtaji na unataka kufanya biashara hii kwa utofauti, basi unaweza kusoma hapa kujua zaidi,
Utaratibu ni ule ule kama ilivyo biashara ya burger na pizza na pia unaweza kuuza vyote kwa pamoja.
Biashara hii ni nzuri sana kwa wenye mtaji unao eleweka kwani ni rahisi kuona faida kupitia wateja wenye uwezo mkubwa,
Kwa maana kuwa kuuza eneo la wateja wenye pesa ni tofauti kabisa na kuuza mitaa ya kawaida au uswahilini.
Kujua zaidi uchanganuzi wa biashara hii, njia za kuuza na masoko, faida na hasara zake bonyeza hapa.

Mambo Ya Kuzingatia Kwenye Biashara Ya Sandwiches
- Usafi wa hali ya juu
- Mzunguko mkubwa wa wateja wenye uhitaji
- Kutotengeza sandwiches kabla ya oda ya mteja ( huharibika haraka na hufaa kuliwa ya moto)
- Bei rafiki mfano sandwiches ya kawaida inaweza kuwa kati ya shilingi mia 500 na ile nzuri yenye vitu vingi zaidi ikawa kati ya elfu 3000 na kuendelea kulingana na kipato cha wateja
- Ubunifu wa ziada ( unaweza kujifunza zaidi you tube).
Hitimisho
Hakuna biashara isiyo na changamoto wala vikwazo au hasara kabisa, hivyo usitarajie faida pekee
Biashara hii kama zilivyo biashara zingine zote pia ina changamoto zake na faida zake au hata hasara kwa ujumla
Muhimu ni kuwa mtatuzi wa changamoto za biashara ili kwenda sawa pasi na kukata tamaa wala kuacha biashara yako.
Uvumilivu na ubunifu ni muhimu sana kwenye biashara yoyote ile kumbuka hakuna biashara nzuri wala biashara mbaya,
Ubaya na uzuri wa biashara hutegemea na mfanya biashara mwenyewe.