Kujiajiri ni nini?
Kujiajiri ni kitendo cha kuanza biashara yako mwenyewe kupitia wazo ulilonalo kwa lengo la kutengeneza au kuzalisha faida
Unaweza kujiajiri kupitia aina mbali mbali za mawazo uliyonayo na kufanikiwa kufikia mafanikio ya biashara unayotaka wakati wowote
Kujiajiri ni jambo linalowezekana kwa kila mmoja bila kujali uwezo wake, mazingira ,elimu , historia wala muonekano
Watu wengi wamekwama kujiajiri kutokana na uwoga ulio ndani yao wenyewe hivyo kupelekea kuishi maisha ya maumivu kwa kufanya kazi chini ya watu wengine kila siku

Kujiajiri ni njia ya kwanza ya kufikia uhuru wa kifedha ,uhuru wa muda na hata mafanikio ya juu kwa mtu yoyote.
Aina za kujiajiri
- Kujiajiri kama mtu mmoja
- Kujiajiri kama ushirika
Kujiajiri kama mtu mmoja
Hapa mara nyingi huwa mtu mmoja anaeanza kutekeleza wazo la aina fulani na mara nyingi huanza akiwa na mtaji kidogo au hata bila mtaji kabisa
Watu wengi katika kundi hili huaza biashara au utekelezaji wa wazo wakiwa na mapungufu mengi kama mtaji na uzoeufu
Asimia kubwa ya kundi hili huamua kuanza taratibu na kujitanua kidogo kidogo mpaka kufikia lengo kubwa
Na mara nyingi hukutana na changamoto nyingi sana zinazoweza kusababisha hali ya kukata tamaa.
Kujiajiri kama ushirika
Mara nyingi huwa watu kuanzia wawili na kuendelea ambao huwa na malengo yanayofanana na kuamua kuanza utekelezaji wao kwa pamoja
Kundi hili pia linaweza kuanza kwakuwa na uzoefu pamoja na mtaji au bila uzoefu wala mtaji kama ilivyo kwa mtu binafsi
kundi hili pia huweza kupitia changamoto nyingi zenye kuambatana na faida au hasara.
Njia za kujiajiri
- Teknolojia
- Mazingira halisi
Teknolojia
Unaweza kujiajiri kupitia teknolojia iliyotawala hasa katika maisha ya sasa pia unaweza kuanza ukiwa na mtaji hata bila mtaji kabisa
Kupitia teknolojia ni njia rahisi zaidi kwani wazo lolote ulilonalo linaweza kutekelezeka na kufikia watu wengi kwa haraka zaidi na kwa gharama nafuu
Mfano unaweza kuwa na wazo la kufundisha kitu chochote na ukatumia mtandao kama Facebook kuanza utekelezaji na ukupata wateja wengi
Au chukulia wazo la kuimba kupitia kipaji chako ,unaweza kubuni mbinu rahisi na kujitangaza kwa kuonesha kazi zako za sanaa sehemu mbalimbali kama youtube kisha kupata mashabiki
Teknolojia ni njia rahisi zaidi ya kujiajiri kwa mtu yoyote kupitia mawazo ya aina nyingi na,
Bila kutumia gharama kubwa na kwa muda mzuri hata kama umeajiriwa sehemu nyingine.
Kujijairi kupitia mazingira halisi
Mazingira ya nje ya teknolojia na mitandao ya kijamii ,hapa unaweza kuangalia na kutekeleza mawazo kama kilimo na aina zote za mawazo uliyonayo kupitia mazingira yanayokunguka
Uzuri ni kuwa unaweza kuchanganya njia zote kulingana na chaguo la wazo lako na ukafanikiwa kutimiza malengo uliyonayo.
Faida za kujiajiri
Kuna faida nyingi sana za kujiajiri kwa mtu mmoja mmoja na hata jamii kwa ujumla
- Kuwa bosi wako mwenyewe
- Kupanga muda wako binafsi
- Kutimiza ndoto, malengo na kusudi la kuumbwa kwako
- Kufikia uhuru wa kifedha
- Kufanya maamuzi yako binafsi
- Kufurahia kuanzisha kitu chako mwenyewe
- Kujifunza na kuendeleza kipaji,ujuzi na hata taaluma yako
- Kujenga heshima kwako binafsi na watu wanaokuzunguka
- Kutengeneza konekshi na watu mbalimbali
Hasara za kujiajri
- Kukosa pesa hasa kama biashara ndio inaanza
- Kukosa muda na kufanya kazi kwa masaa mengi katika hatua za awali
- Kupoteza watu wengi wa karibu
- Kupata hasara kutokana na ukosefu wa uzoefu
- Kutokueleweka
- Kuchanganyikiwa kwa mawazo ya mara kwa mara
Changamoto za kujiajiri
- Ukosefu wa uzoefu
- Ukosefu wa mtaji
- Ushindani wa biashara zingine na teknolojia
- Kupanda na kushuka kwa kwa bei
- Kutimiza matamanio ya wateja
Njia za kupata wazo la kujiajiri (biashara)
Unaweza kupata wazo la kujiajiri na biashara kupitia vitu vifuatavyo
- Taaluma (professional)
- Uzoefu(experience)
- Shauku(passion)
- Muonekano(appearance)
- Kipaji(brilliant)
- Ujuzi(skills)
- Matamanio(hobby)
- Uhitaji(needs)

Hatua za kujiajiri
Zifuatazo ni hatua za kujiajiri kwa mtu yoyote anaetaka kuanza biashara au utekelezaji wa wazo lake
- Chagua wazo na fanya uchunguzi
Anza kwa kujua nini unataka kufanya iwe kupitia kipaji ,taaluma, ujuzi, uzoefu nk pia chunguza uhitaji wa soko uliopo kwa wakati huo
- Andaa mpango wa biashara
Lazima ujue namna utapata wateja,njia utakazotumia,masoko, mauzo, gharama za uendeshaji,faida,matumizi na mtaji unaohitajika
- Sajili na andaa vibali
Kama biashara unayotaka kufanya inauhitaji wa lazima kuanza na usajili au vibali na kama sio lazima ruka hatua hii
- Tafuta chapa yako
Usiige chapa ya mtu mwingine hata kama amefanikwa zaidi ,badala yake anza na ladha ya peke yako na ubunifu wako mwenyewe
- Chagua njia ya kujiajiri na tafuta eneo
Kama ni kwa kutumia teknolojia au mazingira halisi kulingana na aina ya wazo lako na andaa eneo la biashara yako
- Andaa bidhaa au huduma yako
Kama unataka kuuza kitu ,au kutoa huduma fulani iwe kupitia taaluma ujuzi hata kipaji ni lazima uviandae kabla ya kuanza kutafuta soko
- Tafuta wateja
Biashara yoyote lazima ikusudie kuwa na wateja hivyo tumia njia mbalimbali na ubunifu wa ziada kuhakikisha kuwa wateja wanakuja katika biashara yako
- Fanyia kazi chagamoto
Utakutana na changamoto nyingi sana kwahio lazima kila mara utafute njia sahihi ya kupata suluhu kwa kuboresha unachofanya kulingana na matakwa ya wateja na uhitaji
- Jifunze mara kwa mara
Ili kuweza kuwa bora zaidi na kufikia malengo yako lazima ukubali kutenga muda na kujifunza mara kwa mara unachofanya ili upate mbinu bora zaidi za kufanikiwa
Mambo ya kuzingatia katika kujiajiri
- Huduma na bidhaa bora zinazotatua changamoto ya mteja
- Matangazo na ubunifu wa ziada
- Usimamizi sahihi wa fedha na rasilimali
- Wafanyakazi wenye weledi
- Kanuni sahihi za biashara
Maswali ya mara kwa mara
Ndio unaweza kufanikiwa kujiajiri hata kama bado umeajiriwa na kufikia malengo makubwa, jambo la msingi ni kuzingatia usimamizi sahihi
Ndio inawezekana kujiajiri bila mtaji wa aina yoyote kikubwa ni kuwa na wazo sahihi na kujitoa kwa kuweka nia ya dhati
kuna biashara nyingi unaweza kuanza kwa mtaji kidogo au bila mtaji kama vile kutoa ushauri, uandishi wa mitandaoni,uchekeshaji,kuuza matunda,kuuza nguo za mtumba, usafi nk
Ndio unaweza na ni njia bora zaidi ya kupata uzoefu wa biashara kitu cha kuzingatia ni kuangalia muda sahihi wa biashara na masomo yako.
Comments 3