Kurudisha thamani ya biashara
Kurudisha thamani ya biashara inaweza kuwa jambo kubwa au dogo kulingana na changamoto inayopitia biashara iliyo poteza thamani husika.
Kushuka kwa thamani ya biashara ni hali ya biashara kukosa mvuto kwa wateja hivo kuweza kupelekea biashara husika kuanguka kabisa
Kuna sababu nyingi ambazo hupelekea biashara kupoteza thamani yake.
Sababu za biashara kupoteza thamani
- Kufanya biashara kwa mazoea
- Kutosikiliza changamoto za wateja
- Kukosa mtaji wa kutosha
- Kupoteza ubora wa bidhaa au huduma
- Kutozingatia mifumo imara ya uendeshaji wa biashara
- Kukosa usimamizi sahihi
- Kutokuwa na malengo ya muda mrefu efu ya biashara
- Kukua kwa keknolojia
- Ushindani wa bia zingine
- Kuukosa ubunifu
Kufanya biashara kwa mazoea
Wafanya biashara wengi wamejikuta katika kundi hili la mazoea
Baada ya kupata uhakika wa wateja wengi huanza kuona kama tayari ameshawamiliki wateja na hawawezi kwenda sehemu nyingine
Hii hupelekea kutozingatia mambo mengi hasa madogo madogo katika biashara yake
Mfano rahisi kauli za mazoea kwa wateja kwakua tayari ameshajenga ukaribu wa kupindukia
Au kutomuhudumia mteja kwa heshima na utaratibu unaotakiwa
Badala yake kumuona mteja kama sehemu ya biashara yenyewe.
Kutosikiliza changamoto za wateja
Wateja kila mara hupata changamoto na kutamani zifanyiwe marekebisho
Lakini baadhi ya wafanyabiashara huzarau na kuona kama wateja ni wasumbufu!
Hali hii hupelekea wateja kuchoka na kuamua kutafuta sehemu wanayo weza kupata huduma na bidhaa kwa kiwango wanachotaka.
Kukosa mtaji wa kutosha
Kuna muda biashara zinataka maboresho ya mara kwa mara
Kulingana na mabadiliko ya kasi ya maisha ya kila siku
Lazima mfanyabiasha awe na pesa zakumuwezesha kuendana na kasi ya bidhaa na huduma yake katika soko
Hivo pesa zinapokuwa za shida hata biashara hukosa mvuto na kushuka thamani yake
Mfano pesa za matangazo, mara nyingi ili mteja aweze kuipa bidhaa au huduma thamani lazima aione au kuisikia mara kwa mara
Kuna bidhaa nyingi hazina ubora mkubwa ila zinathaminika sokoni kutokana na ubunifu wa matangazo
Kwahio biashara inapokosa kuonekana na kusikika wateja huisahau hata kama ilikuwa nzuri na yenye bora
Vile vile lazima bidhaa au huduma ipatikane bila kukosa sokoni
Unapokuwa na mtaji mdogo hupelekea usambazaji kuzorota
Hivo wateja kukosa kila wanapohitaji na mwisho huamua kubadili machaguo na kupeleka biashara yako kushuka thamani.
Ukosefu wa ubunifu
Kila biashara inataka ubunifu wa hali juu kila mara ili kukuza na kutunza chapa yake (branding)
Kwahio lazima mfanyabiashara husika awe mbunifu na kujua wateja wanataka nini ili kuboresha thamani ya huduma au bidhaa
Mfanyabiashara akiwa hana ubunifu basi lazima biashara ikose mvuto wake
Ubunifu sio lazima uwe mkubwa sana bali hata kwenye mambo madogo madogo tu
Mfano namna ya kupokea mteja, au hata kuongeza kitu kidogo katika bidhaa na huduma unayotoa.
Kupoteza ubora wa huduma au bidhaa
Mfano mwanzoni ulikuwa unatoa vitu bora sana
Labda bidhaa zinatatua changamoto za wateja moja kwa moja au hata zinadumu muda mrefu
Baada ya kupata soko unaanza kushusha na kupunguza baadhi ya vitu kwa lengo la kubana bajeti yako
Hii ni sababu kubwa ya biashara kupoteza mvuto wake
Lazima uweze kufanya vile vile na hata zaidi ya mwanzo ili kulinda ubora wa bidhaa au huduma yako.
Kutozingatia kanuni bora za biashara
Hapa sasa ndio wengi hukwama zaidi
Yani hawataki kabisa kujifunza na kufanya vitu katika ubora
Kuanzia ngazi ya uzalishaji, uchuuzi, masoko, hata mfumo mzima wa uendeshaji biashara
Ukiwa na nia ya kufanya biashara yako kwa kiwango cha juu basi kubali kujifunza na zingatia kanuni sahihi za uendeshaji wa biashara.
Kukosa usimamizi sahihi
Hasa kwa wale ambao hawana muda wa kusimamia biashara zao
Watu wengi wanaoajiriwa hukosa uchungu Sawa na alionao yule muhusika mkuu wa biashara
Hivyo vitu vingi hukosa kabisa usimamizi mzuri na kupeleka biashara kuyumba
Na mwisho wa siku kupoteza mvuto kwa kushuka thamani kabisa.
Kutokuwa na malengo ya muda mrefu ya biashara
Asilimia kubwa ya biashara zinazopoteza thamani kwa kukosa malengo ya muda mrefu
Yani wengi huangalia malengo mafupi hivo kukosa nguvu ya kuwekeza zaidi katika biashara
Muhusika akiwa na malengo ya kuwekeza miaka mingi katika anacho kufanya
Itamlizimu kuwaza mipango mikubwa na atahakikisha anafanya kila anacho weza kulinda biashara yake
Hii huambataka na uboreshaji wa mara kwa mara wa bidhaa au huduma yake
Usimamizi imara na hata kujifunza vitu vipya kila siku
Ikiwa kinyume na hapo basi muhusika hatoweza kwenda Sawa na malengo makubwa ya biashara
Itampelekea kufanya vitu bila kuzingatia mambo mengi na mwisho wa siku atapoteza thamani ya biashara yake.
Kukua kwa Teknolojia
Kila siku mabadiliko makubwa ya Teknolojia yana tokea
Hii imefanya biashara nyingi kupata upinzani mkubwa kutoka katika ubunifu rahisi na wa haraka kupitia Teknolojia
Na kufanya baadhi ya biashara kukosa thamani tena sokoni.
Ushindani wa biashara zingine
Mara kwa mara hutokea watu wanaoanzisha biashara inayotoa huduma au bidhaa zenye kufanana
Na kusababisha ushindani mkubwa sokoni
Hivyo mteja kupata machaguo mengi kulingana na uhitaji wake
Hali hii husababisha baadhi ya wafanya biashara hasa waliotangulia, kupata wakati mgumu sana kuendesha biashara zao
Maana watu wanaokuja baadae huja wakiwa wamejipanga na tayari wameona pengo katika soko husika
Kwahio hujiandaa kuziba mapengo yote kwa haraka mno kuliko watangulizi.
Madhara ya kupoteza thamani ya biashara
Kuna madhara makubwa ya aina mbili
1.Biashara kupitia changamoto ya soko
2 biashara kuanguka kabisa
Biashara kupitia changamoto ya soko
Hapa ndio kuna zile biashara nyingi ambazo zilivuma sana awali lakini baada ya muda zinapoteza thamani na ladha yake sokoni
Katika hatua hii mfanyabiashara hujitahidi kufanya mambo mengi kuweka Sawa biashara yake lakini hujikuta hali ni mbaya
Hatua hii inaweza kutatuliwa na biashara kurudi hali ya awali
Na endapo ikishindikana huweza kupelekea biashara kuanguka moja kwa moja.
Biashara kuanguka /kufa
Hapa ndio zile biashara ambazo hushindwa kabisa kuendelea sokoni na hupotea moja kwa moja
Kuna ambao hukubali matokeo na kuamua kubadili aina ya biashara
Na wapo ambao hupumzika kwa muda na kurudia biashara yao upya.

Hatua za kurudisha thamani ya biashara
- Kubali thamani ya biashara imeshuka
- Fanya thamani ya awali na sasa
- Weka mabadiliko katika vitu vyote vilivyosababisha kushuka kwa thamani
- Jipe muda
Kubali thamani ya biashara imeshuka
Hapa lazima kwanza ukubali uhalisia na sio kulazimisha akili yako kuona kama upo sahihi
Lazima upokee matokeo kwanza ili ikusaidie kufungua akili kupata suluhu
Ukishakubali matokeo husaidia sana kuingia hatua nyingine ya uokoaji.
Fanya tathmini ya awali na sasa
Unatakiwa sasa ujue awali kwanini bidhaa au huduma yako ilipendwa sana na kwanini sasa huna tena wateja
Unapaswa kuchimba kwa undani makosa yote uliyofanya bila kujidanganya
Ainisha kila jambo na lichunguze hata kama ni kosa dogo
Hapa unapaswa kujiuliza maswali yafuatayo,
- Chunguza mwanzo ulikuwa unafanya nini
- Kwa sasa unafanya nini
- Kwanini uliacha kufanya ulichokuwa unafanya mwanzo
- Malengo yako ya biashara ni yapi?
- Unaamini ukifanya nini utarudisha biashara yako Sawa kama awali?
Ukijiuliza maswali kama hayo yatakupa mwanga wa nini unapaswa kufanya
Weka mabadiliko katika vitu vyote vilivyosababisha kushuka kwa thamani ya biashara
Ukishapata majibu yako yote kwa uwazi ni wakati sasa wa kuanza mikakati mpya
Badili kila kitu bila kutumia nguvu bali akili
Maana katika wakati kama huu hufanya wafanyabiashara wengi kuchukua maamuzi yasiyo sahihi na kujikuta wakijiumiza zaidi kwa kukurupa au kutaka mambo yaende haraka
Hupaswi kutumia nguvu wala kulazimisha kuweka mambo Sawa mapema
Bali tumia zaidi akili upate maamuzi ya busara
Kikubwa zingatia mabadiliko, fanya kama ulivyokuwa unafanya mwanzoni wakati unaanza na wakati wateja wanakupenda zaidi
Rudisha mambo taratibu tu Ila kwa uhakika.
Jipe muda
Baada ya kurudisha mambo kama awali sasa jipe muda
Kumbuka umeshasahaulika sokoni na wengi hawaamini tena katika bidhaa wala huduma yako
Wateja tayari wana nunua na wanamachaguo sehemu nyingine
Hivo inataka muda wakutosha waweze kurudi kwako!
Kuna muda wanaweza wasirudi kama kule wanapata kilichobora zaidi ya walichokuwa wanapata kwako
Tayari ulitoa mwanya wa wateja kutafuta machaguo mengine
Hivo unapaswa kuwa na uvumilivu ili waweze kurudi tena.
Njia mbalimbali zinazoweza kusaidia kurudisha thamani ya biashara yako
Ubunifu
Zingatia ubunifu mpya kila siku na usiwe mvivu wa kuwaza mambo mapya
Jifunze mara kwa mara ujue biashara yako inataka nini na kipi ufanye au kipi usifanye
Elimu haina mwisho hivyo lazima kila siku tumia muda mchache kujifunza mambo mapya kuhusu biashara yako
Itakusaidia kuwa mbunifu zaidi.
Weka malengo ya muda mrefu
Jitahidi ufanye biashara za malengo marefu
Ili uweze kuwekeza na kupata matokeo bora
Achana na biashara zisizo na uhai mrefu
Yani usifanye biashara kwa lengo la kutimiza malengo binafsi
Ila iwe ile ambayo utailea, utaitunza na kuzeeka nayo
Hii husaidia sana kuongeza umakini kwa lengo la kulinda chapa ile ile miaka yote.
Punguza au Acha kufanya biashara kwa mazoea
Siku zote heshimu biashara na wateja
Hata kama ni mteja wa kudumu au umemzoea sana na pengine hata ni rafiki au ndugu yako
Mpatie huduma kama vile umemuona kwa mara ya kwanza
Mpe thamani yake na heshima kama mteja mpya
Yani kama vile ungetamani arudi kwako miaka yote na asifikirie kabisa kutafuta chaguo lingine.
Ongeza ubora
Kwenye bidhaa au huduma unayotoa
Hapa kama shida ilikuwa mtaji tafuta mbinu ya haraka kutatua changamoto hio
Unaweza kukopa pesa kwa watu wa karibu, taasisi hata kuuza Mali yako ambayo haitumiki kwa wakati huo
Tafuta chaguo sahihi ili kulinda chapa yako
Usiogope kupoteza pesa ! Ogopa kupoteza wateja
Ubora huwa chanzo kikubwa zaidi cha kupoteza thamani ya biashara.
Badili jina au chapa ya biashara
Kwakua tayari wateja hawaoni tena thamani ya biashara yako
Unaweza kujikuta unatumia nguvu na gharama lakini bado wasiamini na kurudi
Hivyo badili jina, chapa, na mfumo mzima wa biashara ikibidi hama kabisa eneo la awali
Itafanya wateja kujua ni biashara mpya kabisa na waanza upya kuifikiria.
Hitimisho na mambo ya kuzingatia kulinda thamani ya biashara
- Sikiliza wateja na tatua shida zao
- Sikiliza wafanyakazi na wape nafasi ya kutoa maoni
- Zingatia ubora wa biashara kabla ya faida
- Fanya biashara ya malengo marefu
- Fanya matangazo mengi kila wakati
- Jifunze vitu vipya
- Tumia teknolojia kukusaidia katika biashara
- Epuka kuamini sana watu katika kusimamia biashara
- Fanya tathmini za mara kwa mara ili kuziba changamoto mapema
- Epuka tamaa na mafanikio ya haraka
- Kuwa mvumilivu katika kupata mafanikio na usitake faida za haraka.