Msaada wa mtaji unaweza kuwa jambo Rahisi au Gumu kutoka kwa mtu mmoja na mtu mwingine hasa katika Dunia ya sasa
Maisha ya sasa kila mmoja anaangalia maslahi ya upande wake na sio Rahisi kuamini na kumsaidia mtu mwingine Haraka,
Hasa kama hana uhusiano wa moja kwa moja na muombaji, au kama jambo halina manufaa sana kwa upande wake
Lakini pia ugumu huja kutokana na historia za UKOSEFU WA UAMINIFU kwa wanaosaidiwa, Yaani watu wengi wanaoomba msaada huenda kinyume na maubaliano
Hali hii imefanya watoaji wengi kuchoka na kusitisha misaada hasa kwa watu wasio wajua kabisa .
Hivyo basi vijana wengi wamekwama wakiwa na Mawazo mazuri ya Biashara lakini hawana msaada wa mtaji
Kama wewe ni miongoni mwa watu wanaotaka msaada wa mtaji na umetoka katika Familia masikini jua kabisa kuwa unapaswa kuweka jitihada za ziada.
Ikiwa ukoo wako hauna uwezo , namna ya kukupa msaada wala huna kazi ya kukuingizia kipato cha kujitosheleza kutunza pesa,
Unapaswa kujitoa sana bila kuchoka wala kukata tamaa kwa ajili ya kutengeneza maisha yako na kupambania wazo lako.
Maisha Hayana Huruma
Maisha hayana huruma na mtu hata kama una kila sababu za kuhurumiwa!!!
Endapo hutofanya kitu kwa ajili ya maisha yako jua kuwa na maisha hayatofanya kitu kwa ajili yako.
Lazima udhamirie na uache kutia huruma za kwenye maisha na kujiona kama umelaaniwa au umetengwa
Watu hawana muda wala huruma kwa mtu kisa ni masikini ikiwa hawanufaiki kwa chochote kupitia umasikini wako
Kama hutojiinua na kujipambania elewa kuwa hakuna atakae kupambania kamwe , Maisha yako ni jukumu lako mwenyewe

Utawezaje Kupata Msaada Wa mtaji Haraka?
Mbinu Ya Kwanza
Kama bado hujapata wazo la Biashara ya kufanya soma hapa ujue njia unazoweza kutumia kupata wazo
Ikiwa una wazo lako na unataka msaada wa mtaji kutoka kwa watu iwe wa karibu yako au wa mbali basi jitahidi kufuata hatua hizi.
Andaa wazo lilochambuliwa
Hakikisha kuwa kitu unachotaka kufanya umekiandaa kwa mfumo wa maandishi yani mpango wa biashara
Pia onesha kwa uwazi kabisa namna ambavyo mtoaji atanufaika na kupata faida kupitia swala lako
Usioneshe kama unataka faida kwanza mpe yeye kipaombele na changanua wazo lako kwa ukweli na mapana
Onesha faida , hasara , changamoto, mtaji husika wote , makadirio ya mauzo kwa miaka angalau 3 ya awali, masoko na mengineyo
Usioneshe uongo wa aina yoyote kuwa mkweli na jiamini kwa nguvu zako zote.
Fanya Uchunguzi Wa Watu Au Taasisi Zinazoweza Kukusaidia
Huwezi kuomba msaada kwa watu usiowajua yani lazima ujue unaanzia wapi na kumalizia wapi
Na kabla hujasema watu hawana msada hakikisha kuwa umechunguza ndege wako kabla hujarusha manati yako
Sio kila mtu utakae kutana nae anaweza kukupa msaada kwahio chunguza kwanza uwezo wa mtu, Imani yake , Huruma , Uhitaji wake na hata historia yake ya utoaji
Pia lazima uchunguze kiwango cha uchumi wa mtu kama kinakidhi kukusaidia maana sio kila mtu anaweza kupunguza bajeti yake
Kumbuka Uwekezaji kuna kupata na kukosa sasa Mtu hawezi kutoa kitu chake cha mwisho ikiwa anajua anaweza akapata hasara
Ila ukipata mtu mwenye uwezo mkubwa angalau jambo halitokuwa na ugumu sana.
Orodhesha Watu Wote Wanaoweza Kukusaidia Au Taasisi Za Misaada
Hapa usiogope weka Idadi kubwa kadiri utakavyoweza, andika ila anaekujia kichwani iwe anakujua au hakujui kabisa
Angalia watu wenye uwezo kiuchumi angalau wanaoweza kukupa kiasi unachotaka bila kutumia nguvu sana
Usidharau mtu lakini angalia ambae angalau una uhakika na uchumi wake
Anza ngazi ya Familia yao , Marafiki, Mtaani, Kata , Wilaya, Mkoa na hata Nchi nzima au nje ya nje kupitia watu au Taasisi
Wanaweza kuwa viongozi , Walimu wako wa sasa au waliopita, Marafiki zako, Mjirani zako, au mtu yoyote unaemjua hata kama hakujui
Usiogope muonekano wa nje wa mtu hata kama anaonekana mgumu kuingilika wewe andika kila mmoja kwa namna yake
Andika majina na namna ya kumpata iwe ana kwa ana , namba ya simu,akaunti za mitandao ya kijamii na hata Email kulingana na ukaribu wako wa kumfikia kirahisi.
Weka Nia Na Dhamira Ya Dhati Kutoka Moyoni
Siku zote penye nia pana njia na hakuna kinachoshindikana chini ya jua hata kama kitachelewa
Tia nia ya dhati kabisa na dhamiria kuwa hutokubali mpaka ufanikiwe, kumbuka sio rahisi kupata pesa ya mtu kwa urahisi
Jitihada , ubunifu na uvumilivu unahitajika sana kuweza kufanikisha, hivyo bila nia na dhamira ya dhati utashindwa kutimiza lengo lako.
Anza Na Watu Wa Karibu Kufikika
Hasa wale ambao umewazoea sana au angalau wanakujua, hawa ni kama ndugu , marafiki , viongozi wako wa ibada , mtaani na hata walimu wanao kufahamu vizuri
Kisha kama lengo litakuwa bado utafuata wale ambao unawajua ila wao hawakujui kuanzia ngazi ya mtaa wako na kuendelea
Usianze na watu wa mbali sana ikiwa watu wa karibu yako wapo kisa aibu au uoga kumbuka maisha hayataki UOGA.
Tumia Njia Sahihi Ya Kumfikia
Njia ya ana kwa ana ndio njia sahihi zaidi na njia bora ya kuomba msaada wa mtaji au msaada mwingine wowote
Ni mara chache sana mtu kukukatalia jambo ikiwa umeonana nae macho kwa macho na kumueleza shida kwa kinywa chako
Lakini kama njia hii haiwezekani kutokana na Ratiba ya mtu , uzito wa kumfikia na hata umbali basi tumia nji ya Kumpgia simu, kutuma ujumbe au Email
Na kama huna vyote basi Muandikie kupitia kurasa wake wa mtandao wa kijamii anaotumia.
Vaa Vazi La Uhitaji
Epuka kuto kujitosheleza kiuhitaji, yaani kama kweli una nia na uhitaji wa dhati lazima utajionesha tu machoni au hata kwenye maandishi yako
Mtu anaetaka msaada wa kweli hujulikana na ambae hana nia pia huonekana kwa macho rahisi sana
Hivyo kuweza kushinda moyo wa mtu haraka lazima uwe na vazi la uhitaji rohoni na ndani ya moyo wako wote.
Vazi la uhitaji hujionesha machoni kupitia mambo haya
- Namna unavyoongea
- Unyenyekevu wako
- Jinsi unavyosisitiza
- vile unavyo jiamini
- Uvumilivu, usikivu na umakini wa ufatiliaji
- Namna ulivyo na jitihada na kutoonesha hali ya kukata tamaa nk.
Anza Kumkabili Mmoja Mmoja
Usiwe na haraka sana jitahidi kuanza na mmoja baada ya mwingine nenda na mpango wako wa Biashara mkononi lakini usiuoneshe kwanza
Ikiwa ni maongezi ya ana kwa ana ongea kwa mdomo kwanza Jieleze kwa kujiamini na Usioneshe hali ya hofu
Hakuna Binaadamu tofauti na mwingine yani wote tupo sawa tumezidiana Umri, vyeo na uchumi tu
Hivyo si sahihi kumuogopa mtu yoyote kupindukia bali jenga heshima pekee.
Akivutiwa na wazo lako basi Muachie mpango wako wa Biashara wa maandishi kisha subiri jibu lake
Endapo ni kwa njia ya simu anza maongezi kwanza kisha akiomba mpango wa Biashara ndio mtumie baadae
Na kama ni kwa njia ya Email ,sms au akaunti za mitandaoni anza kujitambulisha kisha Eleza shida yako kwa ufupi na subiri jibu lake
Ikiwa haitojibiwa mkumbushe mara tatu katika vipindi tofauti kisha tuma mpango wa Biashara yako moja kwa moja.
Watu wengi wana pesa na hutafuta mahala pa kuziwekeza ziweze kuzalisha kwahio usiogope kwamwe kuomba msaada.

Mbinu Ya Pili
Oesha uwezo wako kwanza
Hapa ili kupata msaada wa mtaji anza kwanza na ulichonacho kupitia uwezo wako binafsi wewe mwenyewe kwanza
Ni rahisi sana kupewa msaada ikiwa utaonekana kwa macho jitihada zako za kila siku , watu hawapendi kupoteza pesa zao
Na hakuna mtu ambae atafurahia kuona anapata hasara au kuamini kitu ambacho hakipo mbele yake
Ila ni rahisi sana kwa watu kuongezea kile wanachokiona kimeanza hata kama kina uchache ndani yake
Hivyo lazima uoneshe kwa vitendo kwanza uwezo wako kisha ufanye wengine wakupe sapoti unayotaka
Anza na ulichonacho , anzia ulipo na tumia vile vilivyo ndani ya uwezo wako kwanza onesha nia jitihada na dhamira ya dhati
Kisha itakupa urahisi wa kushawishi wengine kukusaidia na kuonesha sapoti zao na hata wasipokusaidia utapata namna ya kusimama imara mbeleni
UKITAKA LIFTI YA KWENDA KIGOMA HUWEZI KUIPATA UKIWA CHUMBANI KWAKO; NI LAZIMA USOGEE ULIPO USAFIRI WA KWENDA KIGOMA.
Chukulia mfano unataka kwenda mahala popote lakini huna nauli ya kukufikisha uendapo , sasa kukaa chumbani kwako na,
Kulia sana au kumuomba Mungu ukiwa ndani hakutoweza kufanya muujiza wowote wa safari ya usafiri kuja kukufuata!
Jisaidie Wewe Kwanza
Hata Mungu anataka kwanza UJISAIDIE KISHA NAE AKUSAIDIE yaani hakuna mahala utafika kwa kulala ndani kisa huna nauli
Wala hakuna usafiri utashuka kutoka ndani ya machozi yako wala Nyumba ya ibada unakokesha kuomba Dua bila kuchukua hatua.
Ila ukiinuka na kuanza kutembea mpaka zilipo gari au usafiri wa mahala unataka kwenda basi kuna uwezekano mkubwa wa kupata msaada
Inuka tembea kwa mguu taratibu kufuata njia ya sehemu unakoenda huku ukisimamisha usafiri kwa hisia na sura ya uhitaji
Au fika zilipo gari husika na anza kuomba wahusika au wanaokuzunguka ukiwa hapo hapo mbele ya usafiri
Huku ukiwaelezea wanao husika sababu ya msingi kwanini wakupe lifi?
Ukifanya hivyo nina amini kuwa Lazima utapata msaada au hata utapewa njia ya rahisi ya kufika uendako kwa msaada mwingine
Na hata ukikosa kabisa basi utakuwa umejifunza kitu katika hilo na itakujengea uzoefu wa nini chakufanya wakati mwingine,
Hii ni tofauti kabisa na kama ungekaa ndani tu bila kufanya chochote kwa kusubiria miujiza au kulia sana na kuhisi umepungukiwa
Anza kuonesha uhitaji kwa vitendo kisha utapata msaada unaotaka au njia sahihi ya kukufikisha uendeko
Hata Mungu ni rahisi sana kukusogezea msaada baada ya kuona nia yako kupitia vitendo unavyofanya
Mguu Uliotoka Mtume Kauombea
Hii ni Imani ya Waumini wa Dini ya Kiislamu , yaani ina maana kuwa ukitoka ndani ya nyumba yako na kwenda kujitafutia Riziki yako,
Tayari unakuwa na baraka za Mungu kupitia Mtume wake na Mungu atakusaidia katika jitihada zako.
Hivyo basi tukirudi katika uhalisia wa mada hii ni kuwa ili kupata msaada wa mtaji anza na kidogo ulichonacho
Kipende na kitumikie kwa jitihada zako zote huku ukiendelea kutafuta watu wa kukusaidia mbeleni
Kuna uwezekano mkubwa hata wakaja wenyewe kukusaidia bila wewe kuwatafuta kumbuka watu wana pesa na wanatafuta pakuziweka ziwazalishie
Mbinu Ya Tatu
Saidia Wengine Na Wao Wakusaidie
Kumbuka msemo wa kiswahili kuwa MKONO MTUPU HAULAMBWI maana yake ni kuwa watu watakusaidia ikiwa na wao umewasaidia
Hakuna mtu ambae hataki msaada hata kama ana mafanikio makubwa unavyodhani, kila mmoja hutamani kupata msaada kutoka kwa wengine
Sio lazima msaada uwe pesa bali hata mawazo na mambo madogo madogo au hata zawadi ndogo inayoonesha upendo na thamani ya mtu
Usipende kupokea tu au kutaka kusaidiwa huku ukiwa na mkono wa birika yani chako chako na cha wenzio pia chako!
Tafuta namna ya kumsaidia mlengwa wako kwanza unaetaka msaada kutoka kwakwe katika namna yoyote rahisi kwako
Unaweza kumpa mbinu au ushauri wa kufanya jambo lake vizuri au kujisogeza karibu pia Kumsaidia mambo madogo madogo
Hata majukumu yake ya kazi , nyumbani na popote pale ili aone faida na thamani yako kwanza kabla hujaanza kuomba msaada .
Toa ili upewe zaidi toa muda wako, nguvu zako ,maarifa yako na hata zawadi ndogo ndogo kwa ufupi ni kuwa JIPENDEKEZE UNAPOWEZA.
Mambo Ya Kuzingatia Unapoomba Msaada Wa Mtaji
- Epuka kuomba msaada kupitia kurasa za mitandaoni
- Epuka kulazimisha sana kusaidiwa kutoka kwa mtu mmoja
- Kataa roho ya kukata tamaa na kuchoka
- Usiombe vitu visivyo na tija
- Usimchukie aliyekataa kukusaidia sio laizima kukubaliwa ombi na anaweza kukusaidia wakati mwingine
- Usiamuamini aliyesema atakusaidia kwa maneno matupu.
Hitimisho
Kwenye haya maisha usitegemee bahati nasibu ikufuate , inuka na pambania bahati yako kwa kuivuta ije kwako kwa vitendo
Usingoje msaada ukufuate ulipo simama na pambania msaada unaotaka kwa vitendo
HAKUNA KITU KINACHOTOKEA KWA BAHATI MBAYA TENGENEZA MAZINGIRA ILI VITU VITOKEE.
#REMEMBER YOU CAN WIN IF YOU WANT (UNAWEZA KUSHINDA IKIWA UNATAKA)
Comments 1