Utangulizi
Malengo ya biashara ni malengo yanayo tarajiwa kutimizwa katika kipindi fulani cha muda kwenye biashara fulani
Vile vile malengo haya huwekwa na mfanya biashara kwenye biashara yake ili kupata dira kamili ya biashara anayofanya
Malengo ni muhimu sana kwa mfanya biashara yoyote haijalishi ni biashara kubwa au ndogo bila kujali mtaji pia
Ni muhimu sana kuwa na malengo kwenye biashara unayofanya bila kujali aina ya biashara wala mtaji ulionao
Tena hupaswa kupangwa hata kabla hujaanza kabisa biashara yako au wakati unaandaa mpango wa biashara
Japokuwa malengo haya huweza kubadilika kulingana na sababu kadha wa kadha wakati wa uendeshaji,
Lakini dira nzima ya malengo hutoa muongozo na kuonesha njia kwa mfanya biashara kwenye biashara yake
Sababu kubwa zaidi ya kuweka malengo ni kuongeza mzunguko wa pesa faida na kuipa biashara uhai.

Aina Za Malengo
Kama ilivyo kwenye malengo ya mtu binafsi au yale ya maisha pia malengo haya yamegawanyika katika aina 2
- Malengo ya muda mfupi
- Malengo ya muda mrefu
Malengo ya muda mfupi
Haya ni malengo ambayo yamepangwa kutimizwa katika kipindi kifupi cha muda kwenye biashara
Malengo haya yanaweza kutoka katika malengo ya muda mrefu lakini yaliyo vunjwa vunjwa ili kurahisha utekelazaji
Kwa mfano kama lengo la biashara ni kuwa na faida ya milioni kumi ndani ya miaka 10 maana yake
Ile mipango midogo midogo na mikakati ya kila siku kuhakikisha lengo la kupata milioni kumi linatimia,
Ndio tunaweza kuyaweka katika malengo ya muda mfupi katika biashara.
Malengo Ya Muda Mrefu
Haya ni yale malengo ambayo huwekwa kwenye biashara kwa kuzingatia kipindi kirefu cha muda
Mara nyingi malengo haya huhusisha picha nzima ya biashara au hata maono mazima ya biashara husika
Malengo haya ndio roho na kiini cha biashara nzima na yaliyo beba picha halisi ya mfanya biashara
Hivyo haya sasa ndio hupelekea kuwepo kwa yale malengo ya muda mfupi ndani ya biashara fulani kwa muda fulani
Mfano wa malengo ya muda mrefu inaweza kuwa kufungua tawi lingine la biashara ndani ya miaka 3 ijayo
Au kusambaza kilo 1000 kila siku za mchele ndani na nje ya Tanzania katika kipindi cha miaka 20 ijayo
Na hata malengo mengine yoyote yale kulingana na mipango ya wahusika binafsi wa biashara hio
Kwahio ile mikakati ya utekelezaji wa lengo kila siku au ndani ya miezi kadhaa ndio huwa malengo ya muda mfupi.
Faida Za Malengo
Kama tulivyoona hapo mwanzo kuwa sababu kubwa zaidi ya kuwa na malengo ni kuongeza faida na mauzo
Hivyo kulingana na sababu hizo za jumla hupelekea kuwa na faida zifuatazo kwenye biashara kupitia malengo
- Hutoa dira na muongozo wa biashara, yani husaidia mfanya biashara kupita njia sahihi kulingana na mipango yake ya awali bila kuathiri mchakato mzima wa biashara yake
- Huongeza ufanisi wa biashara, hii pia ni faida kubwa kwani kupitia malengo husaidia kuongeza jitihada na kufanya kazi kwa weledi zaidi hivyo kupelekea ufanisi mzuri
- Huipa biashara uhai , kwa sababu kupitia malengo husaidia kuwa makini na kuboresha mambo mara kwa mara ili biashara kuendelea kuwa bora
- Huongeza hamasa, kwamba hufanya mfanya biashara na waajiriwa wake kupata motisha kwa kufanya kazi kwa juhudi kila wanapoona mambo yanaenda kama yalivyopangwa
- Husaidia kupima mafanikio ya biashara, kwakuwa mara kwa mara mfanya biashara husimama katika malengo yake hivyo huweza kuona kama anapiga hatua au anarudi nyuma
- Husaida kuongeza mauzo na faida, kwa sababu ya ufatiliaji wa mara kwa mara hufanya uwepo wa marekebisho ya haraka kwa kila changamoto inayotokea ili kutimiza lengo
- Hupunguza hatari za biashara, umakini wa mfanya biashara mara kwa mara kupitia malengo aliyo nayo hivyo humsaida kuweka sawa makosa ya mara kwa mara haraka
- Huonesha mchakato mzima wa biashara, husaidia kuwa na mipango ya wazi yenye uhalisia ili kufikia malengo husika
- Huongeza uzingativu wa biashara kwenye kila hatua inayopitia biashara husika na mfanya biashara kwa ujumla.

Hatua Za Kupanga Malengo Ya Biashara
- Jua malengo unayotaka kutimiza
Hapa weka aina zote za malengo ila yatofautishe kila lengo na mipango yake ili kurahisisha mchakato na urahisishaji wa kufikiwa
- Gawanya malengo ya muda mrefu
Lazima ujue kwanza lengo la muda mrefu ni lipi ili isaidie mchakato wa malengo ya muda mfupi
- Vunja vunja malengo ya muda mrefu yawe ya muda mrefu
Hapa sasa utagawanya yale malengo yako yote ya muda mrefu katia vipengle vifupi vifupi kwanza yani usibebe lengo kama lilivyo
- Andaa mikakati na mipango
Baada ya kuwa na malengo ya muda mrefu na mfupi sasa panga mikakati sahihi ya kufikia malengo yako yenye uhalisia zaidi
- Anza utekelezaji kwa vitendo
Kupitia mipango na mikakati uliyo jiwekea sasa ingia katika vitendo halisi na utekelezaji wa hatua kwa hatua
Sifa Za Malengo Mazuri Ya Biashara
Ili malengo yaweze kufikiwa ni lazima pia yawe na sifa zake maalumu ambazo huenda sambamba na lengo
Kuna sifa tano za malengo mazuri ambazo zimeainishwa kama ifuatavyo:
- Yenye muda maalumu, kwamba lazima kila lengo la biashara lioneshe muda wa mwisho wa kufikiwa ili kuongeza hamasa na ufanisi wa kufanikisha
- Yenye uhalisia ,maana yake ni kuwa lazima pia yawe na uhalisia kulingana na ukweli halisi wa mambo na kusiwe na mambo ya kusadikika
- Yenye kupimika, hii pia ni sifa ambayo malengo haya yanapaswa kuwa nayo kwa maana kuwa yaweze kupimika mafaniko yake ndani ya muda fulani
- yanayo fikika, kwa maana kuwa malengo pia lazima yazingatie ufikikaji wake
- Yawe maalumu ,yaani lengo liwe maalumu au moja kubwa bila kuchanganya changanya aina za malengo wakati mmoja na kwenye mipango ya aina moja hii husaidia kuweka mkazo kwa jambo moja kwanza.
Hitimisho
Kwa wafanya biashara wote wadogo au wakubwa suala la kuwa na malengo kwenye biashara ni jambo lisilo kwepeka
Biashara nyingi hufa au kubakia vile vile miaka nenda rudi kwa sababu za kukosa malengo madhubuti
Hii hupelekea biashara nyingi kufanyika kwa mazoea badala ya kukua na kuongezeka thamani yake
Watu wengi hufanya biashara kwa kuangalia faida za muda mfupi ambapo ni chanzo kikubwa cha biashara kutosonga mbele.
🔥🔥 Naihifadhi
Ahsante sana
Ninaendelea kusoma ila nna swl,
Mfn. Kutaka kukuza mtaji wangu maybe uwe double ya uluvyo sasa…hili naliweka kwenye malengo ya muda mfupi au muda mrefu?
Unapaswa liwe lengo la muda mrefu, kisha weka ndani yake malengo ya muda mfupi ili kurahisisha mchakato
Haya ndiyo mambo nakua natafuta 🎉🙏
Karibu sana 🙏
Andiko zuri hili
Ahsante sana 🙏
Naweza kupata mawasiliano yako tafadhali
Ndio bila shaka nitumie ujumbe whatsp 0748029623
Nnimeongeza kitu 🙏
Karibu sana 🙏
Kuna kale kafeeling unakua nako uwe umejiwekea tu malengo twako na utufanikishe 😊😊
Kabisa ni kitu kizuri sanaaa ❤️🌹
Thanks for this 🙏
You’re welcome
Hapa naweza kusoma kwa utulivu sasa. Makala nzuri
Karibu sana 🙏
Andiko zuri, ila mimi ni mgeni hapa. Je unafanya physical consultations kwa sisi wa Dar madam, au unapatikana wapi?
Hello karibu sana, nafanya online consultation and mentorship, nitumie ujumbe whatsp 0748029623