Biashara ndogo ni ambazo unaweza kuanza bila mtaji kabisa au kwa kutumia mtaji chini ya laki moja
Orodha Ya Biashara Ndogo
- Usafi wa nyumba
Pita nyumba kadhaa ongea na wateja Kisha wasafishie kwa kutumia vifaa vyao na kwa bei rafiki mpaka pale utakapopata vifaa vyako
- Kufua nguo na kupiga pasi
Kuna watu wanatamani kuwasidiwa kufuliwa nguo zao hivyo unaweza kupita nyumba kadhaa na kujitangaza kisha kuanza kufua na kupiga pasi
- Kuuza makande
Kwa mtaji chini ya elfu kumi unaweza kuuza makande kwa kusambaza mitaani na ukapata faida kuanzia elfu 5 kwa siku
- Kufundisha
Kama umesoma ualimu unaweza kuanza kufundisha watoto hata mtaani kwa makubaliano na wazazi
- Kuuza uji
Watu wengi wanapenda sana uji unaweza uza uji wa ulezi ,uji wa mchele hata aina nyingine yoyote ya uji
- Kuuza karanga za kuchemsha au kukaanga
Hasa maeneo ya mjini na kwenye mchanganyiko wa watu wengi, kwa mtaji chini ya elfu 5 tu na kupata faida nzuri
- Kutoa ushauri wa mahusiano na maisha
Unaweza kushauri watu kile unachokijua kwa fungua akaunti facebook na ukapata wateja
- Blogging
Unaweza kufungua blog na kuandika vitu unavyopenda Kisha kuingiza pesa kwenye Google Ads mfano Kainetics blog anaweza kukusaidia
- Kuuza matunda au mboga mboga
Matunda yana faida kubwa mno,nenda sokoni nunua kwa bei ya jumla kisha tembeza mtaani
- Vitafunio
Kama mihogo, maandazi,chapati ,sambusa au aina yoyote unayoweza hapo hapo nje ya nyumba unayoishi

Orodha Ya Biashara Ndogo Nyingine
Zipo biashara nyingi sana unazoweza kufanya kuanzia leo hii na kuanza kukua kibiashara badala ya kusubiria kupata pesa nyingi
- Udalali wa vyumba nyumba na mashamba
- Kuuza mitumba
- Kupika kwa oda
- Kuuza miguu ya kuku,vichwa na ngozi
- Kuuza kuku wa kukaanga
- Kuuza mahindi ya kuchoma au kukaanga
- Kulea watoto
- Kulea au kutunza wazee majumbani kwao
Mambo Ya Kuzingatia Unapochagua Wazo La Biashara Ndogo
- Chagua wazo unaloliweza zaidi ili kuepuka kuchoka mapema
- Angalia kitu unachokipenda sana itakusaidia kukifanya kwa ubora
- Zingatia uhitaji uliopo yani aina ya wateja na kitu wanachohitaji
- Angalia ushindani na usifanye kitu kinachofanywa na watu wengi
Mambo Ya Kuzingatia Unapoanza Biashara Ndogo
- Uvumilivu na kuwa na subra
- Uaminifu kwa wateja wako na watu wote
- Nia na dhamira ya dhati kwenye unachofanya
- Uendelevu na sio kuacha ukichoka
- Kauli nzuri na kujipendekeza kwa watu
- Kujifunza vitu vipya mara kwa mara
- Ubunifu wa ziada
- Utunzaji wa fedha
- Epuka tamaa na kujilinganisha
- Jitangaze kila siku na tafuta wateja wapya kila siku
- Jiamini toa aibu na ondoa uoga.
Maswali Yanayoulizwa Zaidi
Ndio haijalishi kiwango cha Elimu yako biashara yoyote inaweza kufanywa na mtu yoyote
Ndio unaweza kuanza biashara hata bila mtaji kikubwa zingatia aina ya wazo lako na uhitaji
Biashara ndogo hufa mapema kutokana na kukata tamaa haraka kwa waanzilishi wanapoona mambo hayaendi kama jinsi walivyotegemea
Inawezekana kama una ujuzi na taaluma yoyote ukaigeuza kuwa biashara hata bila mtaji na kufikia kiwango unachotaka
Comments 1