Utangulizi
Kufanya biashara bila mtaji kabisa inawezekana bila shaka yoyote ile inategemea aina ya Biashara, mazingira na namna ulivyojiandaa
Mtaji kwa maoni yangu ni kitu chochote unachoweza kutumia kuanza au kuendeleza biashara au wazo la biashara
Kuna watu wengi sana ambao wamefanikiwa kuanza biashara nyingi bila mtaji kabisa hata mimi nimewahi kufanya biashara kadhaa bila mtaji wowote
Ili biashara na mauzo yafanyike kunapaswa kuwepo na mteja, bidhaa au huduma basi vitu vingine vyote ni vitu vya ziada tu.
Aina Za Mitaji
Hivyo kwa maoni yangu pia nina amini kuna aina kuu mbili za mitaji ambazo ni
- Pesa na
- Rasilimali kama vyombo , vifaa, mashine , eneo Nk
Kwahio unaweza usiwe na vyote au ukawa na kimoja wapo kwa uwingi au kwa uchache lakini bado unaweza kufanya biashara
Hakuna kinachoshindikana na kujua zaidi namna ya kufanya biashara bila mtaji soma hapa
Makundi Ya Biashara
Lakini pia kuna aina kuu mbili za makundi ya Biashara ambazo zimejumuishwa aina za biashara zote Duniani
- Huduma na
- Bidhaa
Yani kila biashara inaweza kuwa katika kundi la Bidhaa au huduma haijalishi ukubwa au udogo wake.
Miundo Ya Biashara
- Mtu binafsi yaani mtu mmoja
- Washiriki (ushirikiano) wanakuwa zaidi ya mtu mmoja
- Shirika ambapo watu wananua hisa kwa pamoja kwenye kampuni fulani na inaendeshwa kwa sheria.

Njia Za Kupata Wazo La Biashara
Sasa ili uweze kufanya biashara lazima uwe na wazo la biashara , ambapo unaweza kupata wazo kupitia vitu vifuatavyo
- Taaluma
- Maarifa
- Uzoefu
- Ujuzi
- Kipaji
- Vitu unavyovipenda
- Vitu unavyoviweza NK
Ukiwa na kitu kimoja kati ya hivyo kinatosha kukupatia wazo la biashara ya kufanya lakini pia kupitia vitu hivyo,
Unaweza kupata kazi ya kukuingizia kipato kwa kuajiriwa na kulipwa na watu wengine
Hivyo basi orodha ya vitu vyote hapo juu vinaweza kukupa wazo la biashara yako mweyewe au kazi ya kuajiriwa na mtu mwingine.
Mifano Ya Biashara Za Kufanya Bila Mtaji Kabisa
- Kufundisha
- Udalali wa vitu
- Usafi wa nyumba
- Usafi wa ofisi
- Kukusanya takataka
- Bloging
- Ushauri wa mahusiano
- Ushauri wa biashara
- Ushereheshaji
- Kulea watoto
- Kulea wazee Nk
Njia Za Kufanya Biashara Bila Mtaji
Ikiwa hujajua namna ya kuanza biashara bila mtaji soma kwa kubonyeza link hii
Hivyo basi ili uweze kufanya biashara bila mtaji kuna njia kadhaa zinazosaidia sana kufanikisha hilo ambazo ni kama :
- Uza huduma badala ya bidhaa yani ni rahisi kuuza huduma maana zinahitaji maarifa ya kichwani zaidi kuliko bidhaa za kuonekana
- Uza bidhaa za wafanya biashara wengine badala ya kuumiza kichwa kutaka kuwa na bidhaa zako anza na bidhaa za wengine kisha tafuta wateja
- Chukua kwa mali kauli kwa wafanyabiashara wa jumla kisha rudisha pesa baada ya mauzo na faida
- Shirikiana na watu , kama marafiki zako muunganishe nguvu na mawazo ya pamoja kumbuka umoja ni nguvu usifanye mwenyewe
- Tumia vifaa vya mteja hasa kama unafanya biashara za huduma
- Fanya biashara za kumfikia mteja alipo badala ya mteja kukufikia ofisini
- Azima vitu vya watu wengine kama vifaa , vyombo , eneo Nk
Siri Na Mbinu Za Kufanikiwa Unapofanya Biashara Bila Mtaji
- Tumia njia za bure za kujitangaza hasa zile ambazo zinataka matangazo ya mdomo kwenye makundi ya watu au makundi ya biashara mtandaoni kama una simu janja
- Penda kujifunza mara kwa mara na usiwe mbishi wala mgumu kutafuta maarifa mapya hasa mbinu za kuuza na kushawishi
- Ongeza uhusiano mzuri na watu yaani tanua muingiliano chanya na watu zaidi mara kwa mara
- Jifunze kwa wafanyabiashara waliofanikiwa na fatilia historia zao mara kwa mara hasa wale ambao walianzia chini
- Jitume na weka imani kwenye kitu unachofanya bila kujilinganisha na wengine waliokuzidi
- Jitolee na jipendekeze kwa watu wengine ili mambo yako yaende yani jifanye mjinga kwa malengo
- Zidisha ubunifu na ujanja wa kupindukia ili mteja akuamini sana pia usiige wengine tafuta ladha yako binafsi
- Zingatia nidhamu na uvumilivu
- Ondoa aibu na ongeza uwezo wa kujiamini.