Utangulizi
Biashara ya chips ni biashara maarufu sana nchini Tanzania , bila kusahau chips ni chakula pendwa kwa watu wengi sana
Chips ni biashara isiyo chuja kabisa miaka na miaka na inazidi kupata umaarufu zaidi kadiri siku zinavyo zidi kwenda mbele.
Biashara hii licha ya kuwa na ushindani mkubwa sana kila mtaa ,bado soko lake ni kubwa zaidi na wateja wapo kila mahala.
Utamu na urahisi wa kupata chips wakati wowote imefanya biashara hii kupendwa zaidi na walaji (wateja) wengi
Bila kusahau urahisi wa bei yake imeongeza mvuto zaidi kutokana na wakazi wengi kuwa na kipato cha kawaida.
Ladha na utamu wa kipekee wa chips huchanganya watu wengi sana hususani asilimia kubwa ya wadada hupagawa zaidi.
Kuna visa vingi vya wadada walio pata mimba zisizo tarajiwa kisa sahani moja tu ya chips yai na soda kutoka wa wanaume wenye uchu,
Hii ni moja ya ishara kwa namna gani chips hupendwa zaidi na watu wengi nchini Tanzania kwa ujumla hasa wanawake.

Biashara ya chips imeenea sana maeneo yote ya mjini hata baadhi ya vijiji kutokana na kupendwa na watu wengi,
Wazee kwa vijana, watoto kwa watu wazima na haichagui jinsia wala umri wa mtu kwenye suala zima la kupendwa.
Vile vile mahitaji ya kutengeza chips hupatikana kwa urahisi sana ukizingatia viazi ulaya (mbatata) hulimwa zaidi Tanzania,
Hii imefanya urahisi zaidi wa biashara hii ya chips kuenea sana na kupendwa zaidi na watanzania wengi.
Aina Za Chips
Aina za chips zimegawanyika kulingana na mahitaji mbali mbali ya walaji au wahitaji ambao ndio wateja wenyewe
- Chips kavu, hii huwa chips ambazo hazija changanywa na kitu kingine tofauti na viazi vilivyo kaangwa pekee
- Chips yai ( chips zege) aina hii ya chips ni viazi vilivyo changanywa na mayai
- Chips kuku hii huwa chips ambazo huliwa na kuku ( kipande cha kuku)
- Chips mishikaki ( nyama)
- Chips sausage
- Chips samaki NK.
Mahitaji Ya Biashara Ya Chips
Mahitaji ya biashara ya chips ni kama ilivyo kwenye biashara nyingine yoyote hutegemea zaidi mfanya biashara husika,
Kwa maana ya malengo yake, mazingira, kiwango cha mtaji na mengineyo ambayo hayawezi kulingana kati ya mfanya biashara mmoja na mwingine.
Hivyo hapa tutaangalia mahitaji muhimu zaidi kama ifuatavyo:
- Jiko la mkaa na mkaa au jiko la umeme au hata jiko la Gas
- Karai la kukaangia
- Kijiko kikubwa cha kukaangia na kuchuja mafuta
- Kabati la kiio ( linalo onesha ndani)
- Meza ya kuwekea kabati na vyombo vingine
- Viti na meza ya kulia chips au benchi
- Eneo la biashara kama kibanda, fremu au ( hata nyumbani)
- Viazi
- Mafuta
- Chumvi
- Viungo vya salad (kachumbali)
- Bakuli kubwa
- Ndoo au beseni na kisu
- Tomato sause
- Chill source (pilipili)
- Mayonise ( sio lazima)
- Mayai
- Mishikaki
- Kuku
- Samaki
- Sausage
- Chumvi
- Kikaango kidogo,bakuli dogo na kijiko cha chakula
- Sahani ( vifungashio)
NB: Kuna vifaa vingi sana vya kisasa vinavyotumika kwenye biashara ya chips kwenye kumenya viazi au kukaanga chips haraka zaidi ( fryer).

Biashara Ya Chips Kwa Wasio Na Mtaji Mkubwa
Kuna watu wengi sana mitaani hasa kina mama huuza chips kwa mtaji mdogo sana na hupata faida kubwa ,
Kuna chips huuzwa kwa kipimo mpaka cha shilingi mia tatu tu mitaani hususani maeneno ya wanafunzi wa shule za msingi na uswahilini.
Hivyo kuwa na mtaji mdogo sio tatizo ikiwa eneo ulilopo kuna wateja wanaoweza kununua biashara yako,
Uzuri ni kuwa biashara hii wateja hawakosekani kabisa hata maeneo ya uswahilini bado watu wengi hupenda kula chips.
Kwa maana hii , kama una uwezo wa kupata jiko na karai pamoja na vifaa vingine ambavyo hupatikana nyumbani tu,
Basi uhakika wa kuanza biashara hii ni mkubwa sana bila kujali pesa nyingi sana za kuanzia au vifaa vingi.
Kuhusu kabati sio lazima kwa sababu kuna watu wengi huuza chips mitaani bila kabati kabisa bali hutumia deli linalo onesha ndani
Na mara nyingi chips za nyumbani ( mitaani) hupata wateja haraka sababu ya bei ya chini zaidi na huwa hazikai sana .
( Unaweza kutembelea mitaa mbali mbali kujifunza kwa kina dada au kina mama wauzaji wa chips za mitaani)
Mtaji wake hauzidi elfu 15, kwa sababu vifaa vingine vyote hutumika vile vya nyumbani vya kila siku na pesa hii hununua vitu muhimu tu
Mfano wa vitu muhimu ni viazi, mafuta ,mkaa NK au vingine ambavyo havipo nyumbani kwako kwa wakati huo.
Kumbuka:
Asilimia kubwa ya chips hizi hazihitaji vitu kama kuku,nyama wala mayai zaidi ya kachumbali pekee au tomato sauce tu
Bei huwa kati ya shilingi mia tatu kwa kipimo cha awali na kupanda kulingana na ukubwa wa kipimo anachotaka mteja
Unaweza kuanza hapo hapo nyumbani kama kuna mzunguko wa watu wengi kisha baada ya kukuza mtaji ukafanya kwa ukubwa zaidi.
Biashara Ya Chips Kwa Wenye Mitaji Mikubwa
Raha ya biashara hii ni mtaji mzuri kwa sababu huleta urahisi wa kuweka mahitaji mengi pendwa kwa wateja,
Na hata urahisi wa kuona faida kulingana na ukubwa wa bei au hata utanuzi wa biashara kwa kiwango cha kuvutia zaidi.
Tukindoa kodi ya eneo la kufanyia biashara na gharama zingine za matengenezo kama eneo linataka ukarabati,
Mtaji mzuri huwa kati ya shilingi laki 3 za Tanzania na kuendelea kwa maana kulingana na eneo au malengo ya mfanya biashara
Vibanda vingi vya mitaa ya kawaida ya chips mtaji wake hauzidi laki 3 na vile vibanda vizuri zaidi huwa ziaidi ya laki 3.
Mtaji ukiwa mzuri pia faida huonekana kupitia ununuzi wa vitu kwa bei ya jumla kama viazi na mafuta kuliko kununua kwa reja reja kila siku,
Pia kusajili biashara ni muhimu sana na hata kuwa na vibali muhimu vya Serikali husaidia kufanya biashara kwa amani.
Mambo Ya Kuzingatia Kwenye Biashara Ya Chips
- Eneo lenye mzunguko wa watu wengi sana mfano mitaa ya wanafunzi wa shule na vyuo, stendi za dala dala, sokoni, vijiwe ya boda boda na hata sehemu za night clubs na bar mbali mbali nk
- Usafi kuanzia eneo zima la biashara, vyombo vyote na usafi wa wapishi bila kusahau wahudumu kama wapo ( usafi ndio uchawi wa biashara hii )
- Kauli nzuri ( mara nyingi wateja wa chips hupenda muuzaji mchangamfu na mwenye utani kiasi) hasa kina dada
- Kachumbali nzuri ( Hii ni lazima na sio hiari maana wateja karibia wote hutaka chips zenye kachumbali )
- Uwepo wa vinywaji kama soda , juie na maji huvutia zaidi wateja ( kama huna chukua kwa muuzaji wa jirani au duka la karibu)
- Uwepo wa vyakula vya ziada vyote kama kuku, samaki ,mishikaki ,mayai , sausage NK
- Upishi makini ( viazi venye ladha na vitamu vikauke kiasi)
- Epua mazoea ya kupitiliza na wateja hasa wanawake kama wewe ni mwanaume (watakufirisi)
- Fanya huduma ya kupelekea wateja walipo ( free derivery kwa wale wa karibu na kwa haraka zaidi)
- Uza kwa bei kulingana na kipato cha wateja wa eneo hilo
- Uharaka wa kuhudumia ( wateja hawapendi kusubiri chips muda mrefu)
- Zingatia muda mzuri wa kuanza biashara hasa kuanzia sa sita mchana na kufunga usiku mwingi kulingana na eneo au hata kukesha kabisa
- Usirudie mafuta ya kukaangia chips muda mrefu kwa lengo la kubana bajeti (badili mafuta ili chips zisiwe nyeusi)
- Uza Chips za moto ( epuka kuuza chips za baridi wala kurudia chips zilizo lala jana ).

Changamoto Za Biashara Ya Chips
Licha ya faida nzuri na kubwa , biashara hii pia ina changamoto nyingi sana kama :
- Gharama kubwa za uendeshaji ( gas, mkaa, wafanyakazi nk)
- Ushindani mkubwa
- Kupanda kwa bei ya mafuta
- Kupungua kwa msimu wa viazi NK
Hitimisho
Kuweza kufanikiwa katika biashara ya chips pia kama zilivyo biashara nyingine, huhitaji uvumilivu na subra sana
Kwa maana inataka muda kwa wateja kuzoea na hata kuamini katika ubora wa chips zako zaidi na kuanza kuitana wao kwa wao
Hivyo ubunifu haupekukiki kabisa ili kuleta mvuto kila siku kwa wateja wapya na wale wa zamani kuendelea kununua,
Zingatia zaidi uchunguzi wa soko na mahitaji kabla ya kuwekeza pesa kwenye biashara hii ili kupunguza haraza zaidi.