Utangulizi
Usafi wa ofisini kama ilivyo Biashara ya usafi wa nyumba hazina utofauti mkubwa sana katika namna ya kuanza na kuendesha
Wakati mwingine unaweza kuendesha biashara ya usafi wa ofisini na usafi wa nyumba kwa pamoja kama kampuni moja
Biashara hii unaweza kuanza kufanya ukiwa huna mtaji kabisa, ukiwa na mtaji mdogo , mtaji wa kati na hata mtaji mkubwa
Kila kiwango cha mtaji kitakufanya uanze kwa namna ya tofauti kidogo katika uendeshaji wa biashara yako
Pia inategemea na aina ya vifaa unavyotaka kutumia mfano kuna vifaa vya kisasa na vile vya kawaida
Inapendekezwa kutumia vifaa vya kisasa kwa sababu ofisi ni jengo la biashara na linapaswa kuwa nadhibu na kuvutia muda wote
Vile vile baadhi ya majengo huwa maukubwa na marefu bila vifaa vya kisasa itakuwa ugumu kufikia baadhi ya maeneo
Usafi wa ofisini maana yake kusafisha mazingira yote yanayoizungua ofisi ndani na nje pamoja na thamani zilizomo ndani yake.

Usafi wa ofisi umejumuisha ofisi ndogo , kubwa, hoteli, nyumba za kulala wageni , hospitali na majengo yote ambayo hayahusiani na nyumba za kuishi
Aina Za Usafi Wa Ofisini
Kama ilivyo usafi wa nyumba pia kwenye usafi wa ofisi unaweza kugawanywa katika makundi matatu
- Usafi wa kawaida ambao unahusishwa kusafisha sehemu za ofisi zinazoonekana
- Usafi wa ndani huu maana yake kusafisha ofisi kwa kuzingatia sehemu zinazoonekana na zisizoonekana
- Usafi wa maalumu ambapo uchaguzi wa kusafisha kitu cha aina moja pekee hufanyika mfano vioo tu
Usafi wa ofisi unaweza kwenda mbali zaidi na kuhusisha Upigaji wa dawa za kuua wadudu na usafishaji wa bustani
Ijapokuwa kuua wadudu na kutunza au kusafisha bustani zinaweza kuwa huduma na biashara zinazojitegemea.
Usafi Wa Ofisini Umejumuisha Vitu Gani?
Unaposema usafi wa ofisi maana yake unahusika katika kusafisha maeneo kama
- Sakafu , ardhi na Tiles
- Vioo na madirisha
- kuta za ofisi
- Vyoo
- Masinki
- thamani zake kama viti, meza makabati
- Paa za ofisi NK
Hizo ni baadhi ya sehemu ambazo zinahusika kusafishwa na nyingine zote kuzunguka eneo lote la jengo ndani na nje.
Vifaa vipo vingi sana lakini unaweza kuanza na vile vya muhimu zaidi kwanza maana sio vyote vitatakiwa awali
Ukizingatia soko na tenda kubwa zinaweza chukua muda mrefu kidogo kuanza kwahio usiumize kichwa kutaka kila kifaa awali
Hata kama una mtaji mkubwa sana.
- Fagio
- Mashine za ufyonza vumbi
- Mopu
- Ndoo
- Dawa za usafi
- Sabuni
- Mataulo na vitambaa vya kufutia
- Usafiri wa gari
- Matoroli ya ubebea vifaa vya usafi
- Sponji
- Gloves
- Kemikali za usafi
- Brashi za kusugulia
- Mifuko ya uchafu
- Sare za wafanyakazi
Na vifaa vingine vingi kulingana na mahitaji au mtaji wa muhusika mwenyewe

Namna Ya Kuanza Biashara Ya usafi Wa Ofisini Kama Huna Mtaji
Endapo huna mtaji kabisa wa kuanzia yani chukulia huna pesa yoyote na una wazo la kuwa na kampuni ya usafi
Hivyo naamini kuwa hakuna kinacho shindikina ikiwa una nia ya dhati, moyo wa kujituma na malengo makubwa
Usiogope kuanzia chini wala usione aibu kuonekana dhalili mbele za watu kumbuka jukumu la kubadili maisha ni lako mwenyewe
Hao unao waonea aibu leo hawatakuwa na msaada kwa chochote kwako baadae, ni bora ujaribu ushindwe kuliko kuacha kujaribu kabisa,
Hatua Za Kufuata Kama Huna Mtaji
- Weka malengo ya bishara yako na andika mpango wa biashara vile unataka iwe baadae , usiogope andika kila kitu hata kama kinagharimu mamilioni bila kusahau matarajio yako na mbinu za uendeshaji
- Fanya uchunguzi wa ofisi ndogo zilizo mtaani kwako kwanza , zinaweza kuwa nyumba za kulala wageni, ofisi za mtendaji,vyama vya ukopeshaji,na nyingine yoyote ndogo ya mtaa wako au jirani
- Andaa chapa yako ikiwa ni pamoja na jina la biashara utakalotumia usiogope kabisa kuchagua jina
- Weka nia na dhamiria kwa dhati kutoka moyoni
- Kama una pesa angalau Elfu 15000 Tengeneza kadi za biashara ( business cards) ili iwe rahisi kugawa kwa wateja wakupate haraka
- Kama una simu ya kisasa ( smartphone) fungua kurasa za mitandao ya kijamii kama facebook na jitangaze kwa kuweka mambo ya usafi
- Anza na ofisi ndogo kwakuwa huna vifaa kabisa maana mara nyingi ofisi ndogo huwa na vifaa vyao vya kawaida na hazihitaji vifaa vya kisasa
- Ongea nao na kuwa muwazi hapa sasa unapaswa kujifunza namna ya kushawishi na kuteka hisia za watu kwa maelezo yako
- Ukipata tenda kubaliana nao kwa bei punguzo kwa kipindi cha muda fulani kwakuwa watakupa vifaa vyao
- Anza kazi kwa kujituma na uamifu mzuri bila kusahau ubunifu wa hali ya juu sana kumbuka ndio silaha yako
- Endelea kutafuta tenda mpya kwenye ofisi ndogo ndogo , ukipata zaidi tafuta mwenzako na mshirikiane kisha endelea kuongeza idada ya wafanyakazi huku unajitoa taratibu
- Nunua vifaa kwa kila faida unayopata na simama katika lengo lako la awali usitumie pesa vibaya hata kama unaona ndogo
- Sajili biashara ,tafuta vibali na fungua ofisi iliyo ndani ya uwezo wako baada ya kuona unaweza na hatua umepiga yakutosha.
Ondoa Vikwazo Ndani Ya Akili
Haya mambo sio rahisi wala magumu kama utaamua kutoka moyoni , inaweza chukua muda mrefu au mfupi kuanza kuona mafanikio
Kitu cha kuzingatia ni kufanya kwa ubora na matumizi sahihi ya kufikiri, ondoa vikwazo katika akili yako na waza mambo chanya.
Kuanza kwa hatua ndogo ni bora kuliko kukaa na kusubiri, muda haumngoji mtu.
Jinsi Ya Kuanzisha Kampuni Ya Usafi Kwa Wenye Mitaji
Kama ilivyo katika kampuni ya usafi wa nyumbani hii pia haitofautiani sana , pia unaweza kufanya biashara zote mbili ndani ya kampuni moja
- Fanya uchunguzi
Chunguza soko, ushindani, faida , hasara , gharama za uendeshaji na mengine yote yanayohusu biashara ya usafi wa ofisi
- Andaa mpango wa biashara
Andika mambo yote muhimu kama vifaa , gharama za uendeshaji,malipo ya wafanyakazi,makadirio ya mapato nk
- Sajili biashara
Anzia brela,nenda TRA,kisha tafuta leseni ya biashara ndani ya halmashauri yako na tafuta vibali vinavyotakiwa kama OSHA
- Tafuta ofisi
Andaa mahala itakapokuwa ofisi,weka mpangilio unaotaka na thamani za ofisi
- Tafuta wafanyakazi
Zingatia udhamini wao wa uhakika na uzoefu walionao angalau miaka 2 na hata kiwango cha Elimu kuanzia kidato cha nne
- Jitangaze
Tumia mbinu nzuri kupata oda na tenda kutoka ofisi kubwa , unaweza andaa website an app za kurahisha huduma kwa wateja wa mbali
- Fanya kwa ubora
Mteja aridhike kiwe kipaombele cha kampuni yako kabla ya mambo mengine kuhusu bei utapanga kwa kuangalia gharama za uwekezaji wako, thamani ya huduma unayotoa na mengine
Hitimisho
Biashara ya usafi wa ofisi inaweza kuwa na changamoto kadhaa hasa katika
- Uaminifu wa wafanyakazi maana wengi hukumbwa na tamaa ya kuiba vitu vya wateja hivyo hakikisha una ajiri wafanyakazi kwa kuzingatia dhamana zao
- Ucheleweshwaji wa malipo hasa katika tenda kubwa unapaswa kuwa na jitihada za pembeni na sio kutegemea malipo yaendeshe biashara kwa wakati
- Ushindani kutoka kampuni zingine, hapa zingatia ubunifu wa hali ya juu sana na tafuta udhaifu wa washindani wako.