Ajionavyo mtu nafsini kwake Ndivyo alivyo Maana yake ni kuwa namna yoyote unavyojiona kwa ndani wewe mwenyewe ndivyo ambavyo unapaswa kuwa kwa nje
Hata kama nje yako bado hujafikia hata theluthi ya unavyojiona ndani yako, nafsi yako na ulimwengu wa roho ndio,
Hukupa picha halisi ya vile unapaswa kuwa kwa nje bila kujali vikwazo vingine vyovyote
Haijalishi maisha yako ya sasa wala maisha yako ya nyuma ila kinachoangaliwa ni namna wewe ulivyo ndani yako
Kama unajiona kwa ndani ni kiongozi wa siasa mkubwa hata kama kwa sasa upo kijijini unalima na hakuna anaekujua
Amini kuwa umezaliwa kuwa kiongozi unae muona ndani yako na inawezekana kufikia hilo
Inawezekana kwa sasa unaishi maisha ya kuunga unga na huna muelekeo wowote lakini kwa ndani yako unajiona ni tajiri mkubwa sana basi amini kuwa umezaliwa kuwa hivo
Pengine kwa sasa unafanya mambo maovu sana yaliyo kinyume na maamrisho ya Mungu
Lakini kwa ndani yako unajiona ni kiongozi mkubwa sana wa Dini jua kuwa wito na kusudi lako la kuumbwa lipo hapo hapo.

Bila kujali maisha na mapito yako ya sasa kitu pekee ni kupigania kutimiza kile unachokiona ndani yako
Kama unajiona wewe ni Daktari mkubwa hata kama kwa sasa unauza mahindi amini inawezekana
Pengine kwa ndani unajiona ni muandishi mkubwa wa vitabu hata kama kwa sasa unauza mgahawa amini kuwa unaweza
Endapo kwa ndani unajiona ni Raisi ajae hata kama kwa sasa hujulikani kabisa katika nafasi yoyote ya uongozi jua kuwa umezaliwa kuwa Raisi
Haijalishi ugumu wake wala changamoto zake kikubwa ni kuwa unapaswa kuwa vile unavyojiona kwa ndani ili kutimiza kusudi la kuumbwa kwako
Hakuna jambo rahisi wala hakuna jambo gumu hapa Duniani ila kila jambo linaongozwa na Imani ya mtu
Imani yako ikiwa ndogo jambo lazima litakuwa gumu hata kama linawepesi ndani yake
Na endapo Imani yako ikiwa kubwa basi kitu chochote huwa chepesi hata kama kina ugumu ndani yake.
Umezaliwa Kwa Kusudi Maalumu
Kila mmoja ameletwa Duniani kwa lengo la kufanya kitu fulani ndani ya kusudi fulani kama ajionavyo mtu nafsini
Hakuna aliyeletwa kwa bahati mbaya wala kusindikiza wengine kwenye maisha yake
Wote tupo kufanya kitu maalumu na taswira nzima ipo ndani yetu sisi wenyewe
Yani ndani yako tayari una kila kitu ,maagizo na maelekezo yote ya kufanya na kuishi ndani ya kusudi la kuumbwa kwako
Usiogope ukubwa wa taswira unayoiona kwa ndani kwasababu ipo kwa ajili ya kukutumikia wewe
Iagize taswira yako ikupe kile unataka kutimiza na utaona namna maisha yanajiendesha ndani ya maana nzima ya maisha yako.
Hakuna mtu atakae kuja kukusaidia kwasababu kila mmoja ana twasira yake tayari
Wewe mwenyewe ndio unapaswa kujiinua na kukimbizana na hio taswira ya ndani mpaka itoke kwa nje
Usikubali ubaki kama bunzi kwenye muhindi, maana kama hutaishi ndani ya ulivyo basi ni kama umepoteza maana nzima ya maisha yako
Maisha ni mazuri sana na hayapaswi kuwa na maumivu yoyote ila maumivu huja kwasababu ya kulazimisha kuishi nje ya kusudi lako
Mungu ameshatupa kila kitu na hakuna kitu cha kumuomba tena bali unapaswa kutumia kile ulichopewa na kukimiliki vile unataka ili kikupe vyote vilivyobaki.
Kamwe hutoweza kuwa zaidi ya ujionavyo nafsni kwako, kama unajiona hufai na upo kwa ajili ya kutegemea wengine basi jiandae kuwa hivyo
Hata ukipewa kila kitu cha kukusaidia kama unaona huwezi jua kuwa hutoweza kabisa
Kama unaamini unaweza kuwa aina ya yule aliye ndani ya nafsi yako lazima utakuwa hata kama mzingira yote hayakusapoti kabisa.
- Gundua taswira yako
Kwa kujiuliza ndani yako unajionaje na unataka kuwa nani
- Weka nia
Nia na dhamira ya kuwa lazima ufikie vile unavyojiona kwa ndani bila kujali changamoto za nje
- Andaa mipango
Kupitia taswira yako ya ndani kwa namna yako mwenyewe panga mikakati utaanzaje na utafanyaje kufikia unavyojiona kwa ndani yako
- Anza utekelezaji
Kupitia mipango yako kidogo kidogo kila siku bila kuacha kwa kujisogeza karibu na kila unachokiona kitakufaa na kukusaidia
- Usirudi nyuma
Utakutana na vikwazo vingi vya nje vya kila aina jambo la msingi ni kuendelea na kusimama katika unachokifanya na kukiamini tu.
- Ondoa uoga
- Jiamini
- Epuka kuomba ushauri sana hasa kwa watu ambao hawafanyi kile unachokitaka
- Weka mikakati hata kama unaona itakuwa migumu kuitimiza
- Jenga imani kubwa
- Simamia msimamo wako
- Fanya kila siku angalau kitu kidogo
- Jifunze mambo mengi kuhusu vile unata kuwa na tafuta taarifa sahihi kila mara
- Jisogeze kwa watu chanya wanaofanya mambo yale unayoyataka
- Jikane maisha yako ya nyuma na usikubali mambo ya nyuma yakuendeshe
- Jitoe kwa kila kitu na usikate tamaa kabisa wala usirudi nyuma.
Hitimisho
Amini kuwa Ujionavyo Nafsi Ndivyo Unapaswa kuwa na kuishi maisha hayo unatakiwa kuzingatia maagizo ya ndani yako ili uishi ndani ya maana na kusudi la kuumbwa kwako
Usiige maisha ya watu wengine wala usikubali kupangiwa mambo ya kufanya kwenye maisha yako na watu wengine
Kwasababu kila mmoja ameletwa kwa kusudi tofauti na mwingie kama vile ajionavyo yeye mwenyewe
Ondoa uoga na jiamini kisha pambania kile kilichopo ndani yako tu.