Utangulizi
Tahajudi au meditation ni kitendo cha mtu kufikia kiwango cha juu cha utulivu wa akili kutokana na sababu yake maalumu
Kitendo hiki huambatana na akili kwasababu akili ndio ina simamia na kuendesha maisha ya mtu yoyote
Ukiweza kuitumia akili yako vizuri basi utapata chochote unachotaka na utaishi kwa kusimamia mazingira yako yote ya ndani na nje ya mwili wako
Hii inaweza kufanywa na mtu yoyote wakati wowote kwa sababu mbalimbali lakini lengo kubwa zaidi ni kupata utulivu na amani ya ndani kabisa kupitia akili na ubongo
Jambo hili lipo sehemu nyingi na asilimia kubwa ya watu wa mataifa mbalimbali hufanya kwa kuambatanisha na mambo ya KIIMANI
Kama Dini na Miungu mfano rahisi ni dini ya buddhism ,Jaininism,Hinduism na hata dini ya kiislamu.

Image by Ralf Kunze from pixabay.
Faida za kufanya tahajudi
Kuna faida nyingi sana za kufanya tahajudi au meditation kwa kila mtu tukiondoa faida na sababu za kidini
Leo tutangalia faida chache zinazoambata na sababu za kiafya.
- Huongeza kiwango cha amani Ijue nguvu iliyo ndani yako
- Huondoa mawazo mabaya
- Husaidia kupata furaha ya ndani
- Huongeza uwezo mkubwa wa kufikiri na kutatua changamoto
- Huboresha afya ya akili
- Huongeza ufanisi wa kazi na maisha na kupelekea mafanikio makubwa
- Huboresha mfumo wa mzunguko wa damu na kupunguza matatizo ya afya kama presha ,moyo,na hata mfumo wa chakula tumboni
Huongeza kiwango cha amani
Kutokana na changamoto za maisha ya kila siku kuna wakati hujikuta amani ya ndani inaondoka na kujihisi hali ya kupoteza muelekeo na hata wasiwasi mkubwa ndani ya nafsi
Ukifanya tahajudi husaidia sana kuweka akili yako sawa na kurejesha hali ya utulivu wa ndani kwa kukuondolea wasiwasi hata kukurudisha katika utambuzi wako binafsi.
Huondoa mawazo mabaya
haya ni mawazo kama kujikataa, kukata tamaa,kujidhuru ,kuhisi kuelemewa na hata hali ya kujiona kama umefika mwisho wa majaribu yako
Na kama huwezi tena kufanikisha jambo lolote mbele yako, ukifanya tahajudi kupitia matatizo yako kwa lengo la kujipata upya
Husaidia kuifungua akili yako upya na kukuondolea uzio wote uliojengeka mbele yako kwenye akili
Utaanza kuona mwanga mpya na njia mbali mbali zitafunguka katika akili yako za kukabiliana na matatizo uliyonayo.
Husaidia kupata furaha ya ndani
kuna nyakati za maisha kutokana na sababu mbalimbali furaha huondoka na kuona kama maisha hayana maana tena
kumbuka furaha yako ipo ndani yako mwenyewe na haihusiani kabisa na mazingira ya nje ,mtu au vitu
Hivyo kupata au kukosa furaha husababishwa na namna unavyofikiri kwa ndani au namna unavyopokea tatizo linalokukabili
Ili kuweza kuwa na furaha lazima uwe na mawazo chanya kila mara na ubadili mtazamo na namna unavyochukulia mambo
Kwahio ukifanya tahajudi husaidia sana kukupa utulivu ndani ya akili yako na ubunifu wa suluhu mbalimbali za changamoto
Ikiwa pamoja na kukupa furaha nyakati zote bila kujali manzigira yako ya nje.
Huongeza uwezo mkubwa wa kufikiri na kutatua changamoto
Kama ilivyo ukweli kuwa akili zetu zimeumbwa zikiwa na majibu ya changamoto zote
kuweza kutatua changamoto huambatana na kiwango cha kufikiri cha mtu binafsi
Kila binaadamu ana asilimia mia moja za akili, ila matumizi ya akili yametofautiana kutokana na uwezo wa kufikiri wa kila mmoja
Sasa tahajudi husaidia sana kuboresha mfumo mzima wa akili ya mtu yoyote na kumuongezea matumizi ya akili yake kwa kila jambo analofanya.
Huboresha afya ya akili
Watu wengi kutokana na sababu mbalimbali za maisha ya kila siku wamekumbwa na tatizo la afya ya akili zao
Kuwa na shida ya afya ya akili sio lazima mtu awehuke kabisa ,kuna watu wengi wapo sawa kwa muonekano wa nje
Na wanafanya mambo yao ya kila siku vizuri kabisa na wengine hata ni viongozi wakubwa ila akili zao zina shida
Utangundua ukiongea nae kwa masaa machache sana kuwa hayupo sawa kichwani hata kama ana maisha mazuri sana
Au hata matendo yake anayofanya huwa hayaendani na umri wake wala nafasi yake katika jamii
Sasa tahajudi husadia sana kuweka akili sawa ni kama vile kuibusti akili au kuifanya ijizime na kujiweka sawa upya
Mfano rahisi ni simu au kompyuta kuna muda inatakiwa kufanyiwa restore au re start ili kuweka mifumo yake sawa ya kiufanisi.
Huongeza ufanisi wa kazi na maisha hivo kupelekea mafanikio makubwa
Kama ilivyo ukweli kuwa tahajudi husaidia sana katika kuweka akili sawa na kuongeza uwezo wa kufikiri
Kwa maana hiyo uwezo wa kufikiri ukiwa juu na hata ufanisi utakuwa juu iwe kwenye kazi unayofanya hata biashara na mafanikio yataongezeka.
Huboresha mfumo wa mzunguko wa damu na kupunguza matatizo ya afya kama moyo,presha na hata mfumo wa chakula tumboni
Hapa sasa kupitia tahajudi magonjwa mengi sana yanayohusiana na msukumo wa damu hutatulika kwasababu tahajudi inahusisha matumizi ya ubongo
Akili na ubongo vikitenda kazi sawa sawa basi maradhi mengi hupungua hasa yenye uhusiano wa moja kwa moja na ubongo
Pia tahajudi inapoleta amani huambatana na kuweka mifumo sawa ya ndani ya mwili hivo hali ya msongo wa mawazo na wasiwasi hutulia na kupelekea maradhi kama presha kutulia.

Maswali yanayoulizwa zaidi
Hapana tahajudi sio uchawi kabisa na haihusiani na imani za ishirikina ila inasaidai kuunganisha mtu kupitia asili yake ya ndani na mazingira yake ya nje
Ndio unaweza kufanya tahajudi (meditation)hata kama hufungamani na imani yoyote
Tahajudi inasaidia kuongeza uwezo wa kufikiri na uwezo wa ufanisi hivyo husaidia katika kuongeza ubunifu mkubwa na kuleta mafanikio kwenye kitu unachofanya
Ndio unaweza kufanya tahajudi sehemu yoyote kikubwa zingatia utulivu wa eneo
Ndio kama utakusudia kusahau maumivu ya nyuma na kutamani kuanza upya tahajudi husaidia kufanya akili yako kukupa mawazo mapya
Mambo ya kuzingatia ili kufanya tahajudi (meditation)
Ili uweze kufanya tahajudi kwa mtu ambae hujazoea na unaanza kujifunza zingatia mambo haya
- Eneo tulivu
- Usiri
- Utulivu wako binafsi
- Nia na jua nini unataka
Eneo tulivu
Hakikisha kuwa eneo unalotumia kufanya tahajudi halina kelele kabisa na ukiweza fanya usiku sana au asubuhi sana au muda wowote unaotaka lakini kusiwe na kelele zozote.
Usiri
Wakati unafanya jitahidi uwe mwenyewe na epuka watu kujua au kuona nini unafanya na ikitokea umeonekana kwa bahati mbaya tafuta namna ya kuoesha kuwa hukuwa unafanya tahajudi.
Utulivu wako binafsi
Hapa ondoa kila kitu kitakachokufanya ukose utulivu mfano simu yako unaweza kuzima kabisa na hata mawazo yako ukayakusanya na kuyapuuza kwa muda mpaka pale utakapomaliza.
Nia na jua unachotaka
Lazima uweke nia moyoni kwanza na ujue lengo la tahajudi yako hii itakusaidia kufanya kwa uhakika na kuona matokeo haraka.
Jinsi ya kufanya tahajudi (meditation)
Kufanya tahajudi sahihi kama bado unajifunza inaweza kuwa changamoto kidogo
Lakini ukiwa na nia ya dhati na kujitahidi kufanya mara wa mara utaweza kufanya kwa usahihi
- Nia
weka nia ya dhati ndani ya moyo wako na sema nini hasa lengo la kufanya tahajudi yako
- Kaa mkao unaokupa uhuru
unaweza kulala chali kwa kuangalia juu ukiwa umejinyoosha na kulegeza mwili wako wote
Au ukakaa mkao ambao utakuwa uhuru wa kukaa muda mrefu bila kuumia wala kujigeuza geuza - Fumba macho yako ya kupumua kwa nguvu mara tatu
Kisha anza kujitahidi kutowaza kitu chochote kingine zaidi ya kile unachotaka
Kwa kujiruhusu kuingia ndani ya mawazo yako na kutawala akili yako tu - Jipe muda
Endelea kutulia na kutafakari kwa kina unachotaka kulingana na nia yako taratibu hata kama utajikuta mawazo yanahama
Endelea kujipa muda ,tulia na fanya angalau kwa dakika kuanzia ishirini na usizidi dakika thelathini - Rudisha mawazo taratibu
Baada ya dakika ishirini au thelathini anza kurudi katika hali ya kawaida taratibu na fumbua macho yako
Hitimisho
Tahajudi (meditation)inapaswa kufanyika mara kwa mara hata ikiwezekana kila siku kwa dakika chache ili kuweza kupata matokeo mazuri
Yani huwezi kufanya mara moja na kuona matokeo sahihi, ila lazima ujitoe na iwe sehemu ya ratiba yako ya kila siku au kila mara
Ikiwa hutoona matokeo haraka usiogope kwani huchukua muda kuanza kujihisi vile umekusudia, jambo la msingi ni kutokata tamaa.