You Can Win If You Want

Ijue Nguvu Iliyo Ndani Yako

Maana ya nguvu iliyo ndani yako

Nguvu iliyo ndani yako ni nguvu ambayo hukusaidia kutimiza malengo na kusudi la kuumbwa kwako katika namna ya tofauti na kipekee

Kila mtu ameumbwa na nguvu kubwa ndani yake ambayo hupaswa kuitumia katika kufanikisha jambo lolote analotaka

Kazi ya nguvu iliyo ndani

Nguvu iliyo ndani Ndio ambayo humpa mtu muongozo katika kufanikisha jambo lolote na kuwa vyovyote anavyotaka hapa duniani,

Kila mmoja ameumbwa na kila kitu ambacho hupaswa kukitumia na kufanikiwa kwa janbo lolote

Nguvu iliyo ndani huanzia katika akili, nafsi, mwili na mazingira ya nje, Jambo lolote likiwezekana akili basi huwezekana pia katika maisha ya nje.

Wote tumeletwa Duniani tukiwa na kitu cha kutimiza hivo hakuna ambae amekuja”kusidikiza wengine!

Ajionavyo mtu nafsini kwake ndivyo alivyo

Kauli hii ni ya kawaida sana lakini ina maana kubwa mno katika mafanikio ya kila mmoja,

Yani  vile ambayo unajiona ndani yako Ndivyo unapaswa kuwa kwa nje  bila kujali vikwazo vyovyote vilivyopo

Kama ndani yako unajiona kuwa ni mwanasiasa mkubwa hata kama kwasasa unashona viatu,  Amini Ndivyo unapaswa kuwa mwanasiasa unayemuona akilini mwako,

Nafsi yako haidanganyi

Kama unajiona ni msanii mkubwa japo kwa sasa labda unauza mahindi, Amini kuwa wewe ni msanii na unapaswa kuwa msanii

Vyovyote unajiona hata kama Bilionea mkubwa tambua kuwa unapaswa kuwa hivo hata kama kwa sasa upo kijijini kibondo unalima mahindi!

Ndio maana hatupaswi kamwe kujinenea wala kujiwazia mambo mabaya kabisa maana hayo mambo hutengeneza uhalisia wa nje!

Akili ina uwezo mkubwa wa kutengeneza uhalisia wa ndani na nje na kuwa katika namna moja inayofanana.

Ijue nguvu iliyo ndani yako

Maisha hayana maana, yape maana yako!

Hapa duniani maisha tunayoishi hayana maana yoyote ikiwa tu utaamua kuishi bila maana. Lazima uchague maana ya maisha yako ndio utayafurahia,

Kama utaamua kuishi kwa kusindikiza wengine na kujiona huna chakufanya basi maisha lazima yawe machungu kwa upande wako

Hujaletwa Duniani kuwa mzigo wala tegemezi kwa wengine, bali umekuja kufanya kitu tofauti na wengine!

Jua maana ya maisha yako

  • Ukiona maana  ya maisha yako  inakamilishwa kwasababu ya ndoa basi pambania ndoa
  • Ukiona maana ya maisha ni kusaidia wengine na ndio unapata furaha basi fanya hivo
  • Ukiona maisha ni kipaji chako au ujuzi wako  basi pambania kipaji chako na ishi humo humo ili kuiona Dunia yako
  • Ukiona maisha ni starehe yani bila starehe bado Huna amani, basi ishi humo maana Ndio maana ya maisha yako ilipo na umeamua iwe
  • Ukiona maana ya maisha ni kuwa huru na kujitegemea kivyako basi simama humo ili kupata furaha ya maisha

Tafuta maana ya maisha yako

Kila mtu anapaswa kuwa na maana ya maisha yake na kuishi  ndani ya maana hio ili kuepuka “mateso” na “majuto”.

Hujaletwa dunia kuteseka, maumivu yote tumejisababishia wenyewe kwa kutaka kuishi nje ya maana ya maisha na nguvu iliyo ndani yetu

Kwanini watu huteseka na kupitia maumivu katika maisha yao?

Kuna sababu kuu mbili za watu kuteseka na kupitia maumivu katika maisha yao ya kila siku

  • Kujaribu kuishi nje ya nguvu iliyo ndani yao na
  • Kuishi nje ya maana ya maisha yao halisi

Kujaribu kuishi nje ya nguvu iliyo ndani yao

Mfano mtu anajiona kwa ndani kuwa anapaswa kuwa daktari, lakini kutokana na sababu za maisha yake ya wakati huo anaona hawezi kusoma!

Hivo anaamua kuishi kwa kuamini kuwa hawezi kuwa daktari zaidi ya kuwa muuza mitumba!

Mwisho wa siku anateseka katika kiwango ambacho hakupaswa kuteseka, na anaishia kuona maisha kama “Jahanam

Maumivu na mateso unayopitia ukiwa ndani ya nguvu iliyo ndani yako huwa hayafanani na yale utakayopata Ukiishi nje ya nguvu,

Haupaswi kuteseka

Mateso unayopata wakati wa kulazimisha kufikia nguvu ya ndani yako ni tofauti kabisa na yale unakayopata ukiwa nje ya nguvu yako

Kwasababu Ulimwengu upo tayari kukupa kila kitu unachohitaji kupitia  nguvu ya sumaku umeme, mawimbi,na nyakati zako  kupitia nguvu iliyo ndani yako

Ukijua kilichopo ndani yako kwa Imani na kuamua kukiishi bila kujali vikwazo vya nje basi,

Ulimwengu utakutengenezea njia yako na utakusogeza karibu na sumaku umeme, mawimbi na kunasa mafanikio yako!

Kuishi nje ya maana ya maisha yao

Haya maisha hayana maana kabisa, wala hayapo kukupa maana. Maana ya maisha yako unayo wewe mwenyewe hivo lazima uitafute.

Tafuta maana ya maisha yako ili kuepuka mateso ya Dunia, kama unaona maana ya maisha ipo katika kitu fulani yani bila hicho hujaishi basi ishi nacho

Utajuaje kuwa unaishi maisha yenye maana na nguvu iliyo ndani yako

Kila mara, siku, wiki, mwezi hata mwaka fanya tathmini ya maisha yako kwa kujiuliza maswali yafuatayo,

  • Ikitokea umekufa gafla, je utaridhika na maisha uliyoishi duniani au utakuwa bado unayadai maisha  yako?
  • Ukirudishiwa miaka kadhaa nyuma, je bado ungeishi maisha hayo hayo unayoishi sasa na kuyafurahia?
  • Kama ungeambiwa uchague kitu kimoja unachokihitaji sana ili ufanikiwe kwenye maisha, je ungechagua kitu gani?
  • Ukiondolewa vikwazo vyote vinavyokuzuia kufanikiwa! Je unahisi ungekuwa nani? Na ungefanya nini?
  • Kama utaishi miaka 10 ijayo, mambo unayofanya sasa hivi utakuwa na ujasiri wa kuyatazama na kufurahia bila majuto yoyote?
  • Ukiyatazama maisha yako yote ya nyuma je unayafurahia na umeridhika kwa yote uliyofanya au bado una majuto fulani?

Ukigundua kuna majibu tofauti na kile unachotaka anza kubadilika na rekebisha makosa maana muda haurudi nyuma.

Aina ya nguvu iliyo ndani yako

  • Nguvu ya asili, hii ni nguvu ambayo mtu huzaliwa nayo na mara nyingi nguvu hii hujidhihirisha toka mtoto akiwa mdogo
  • Nguvu ya kutengenezwa, hii hutokana  na mazingira kama uzoefu wa maisha, Elimu, msukumo wa jamii nk

Nguvu ya asili

Nguvu hii mtu huzaliwa nayo moja kwa moja  na mara nyingi nguvu hii huambatana na vipaji vya asili,

Mtoto huwa na uwezo wa kufanya mambo kadhaa kama kucheza mpira, kuimba, uandishi, utundu wa utengezaji vitu nk

Wazazi wengi huwa chanzo cha kupoteza nguvu hii kwa watoto wao bila kujua, kwa kuwakataza mara kwa mara kuacha kufanya wanayo yafanya hivo kuwajengea hofu na uoga hata wanapokuwa watu wazima!

Ni watoto wachache sana ambao hufanikiwa kuishi ndani ya nguvu zao na kuzitumia mpaka wanapokuwa wakubwa

Wazazi hupaswa kuchunguza uwezo wa watoto wao na kuwajenga  ili waweze kuishi ndani ya nguvu zao maana Ndivyo wanapaswa kuwa toka Ulimwengu wa roho

Nguvu ya kutengenezwa

Nguvu hii huja kutokana na sababu mbali mbali za maisha kama vile

  • Elimu, kupitia Elimu mtu hujengewa nguvu na uwezo ndani yake  kama wanasheria, madaktari, walimu nk.
  • Uzoefu wa maisha, kama Matukio mbalimbali na historia kadhaa za nyuma humfanya mtu kupata nguvu na kujengeka ndani yake kama Biashara, kuna watu hawakuzaliwa na vipaji vya biashara ila maisha huwapa vipaji kutokana na nyakati  fulani
  • Msukumo wa jamii, kuna muda jamii hufanya mtu kujengeka nguvu ndani yake kutokana na tabia au muonekano wa mtu , mfano watu wanaokuzunguka huweza kuona unafaa kuwa mwanamitindo kutokana na muonekano wako na huanza kukupa sifa au majina ya wanamitindo na baada ya muda utajikuta unajenga nguvu na kuamini katika Mitindo

Utaijuaje nguvu iliyo ndani yako na kuitumia kukupa mafanikio?

Kuna watu huwahi kujua nguvu zao na wengine huchelewa sana kujua nguvu zao

Hivyo inawezekana sana mpaka unakuwa mtu mzima usijue unapaswa kuwa nani na kufanya nini!

Hio ni hali ya kawaida sana, Usiogope na wala usihisi kama umechelewa maana kila mmoja ana wakati wake wa kufanikiwa

kuna mifano ya watu maarufu wengi ambao  walichelewa kujua nguvu zao lakini leo hii wamefanya mambo mengi makubwa kama HARRY POTTER.

Mambo yanayosaidia kuijua nguvu iliyo ndani yako

  • Kupitia vitu unavyopenda sana kufanya inawezekana ikawa ujuzi au kipaji
  • Angalia kitu ambacho wengine hukusifia mno mara kwa mara hata kama hawakufahamu au hata kama utakifanya kwa mara ya kwanza  lazima usifiwe
  • Sauti  na taswira ya ndani yako, hapa mara nyingi kuna ile sauti ambayo hukwambia wewe ni nani mara kwa mara hata unapojisahau au picha fulani ya mtu unaemtaka huwa inakujia mara kwa mara
  • Vitu Unavyoviweza sana, hapa angalia kitu gani unakiweza mno yani hata usipojiandaa lazima tu utakifanikisha mfano masomo yako.

Kutumia nguvu iliyo ndani na yako na kufanikiwa

  • Ijue nguvu yako Amini na amua kuitumia kwa nia ya dhati
  • Ikubali na ipokee nguvu yako bila kujiwekea vikwazo vyovyote vya nje
  • Kila siku fanya kitu kimoja hata kama ni kidogo kuelekea ndoto ya nguvu yako uliyonayo
  • Tafuta njia yako na kila siku jifunze kitu kipya kupitia nguvu unayoiona ndani yako
  • Jikubali, jiamini na usijilinganishe na mtu yoyote hata kama amekuzidi vile unavyotaka kuwa

Ijue nguvu yako ya ndani , amini na amua kuitumia kwa nia ya dhati

Kitu cha kwanza ili uweze kutumia na kufanikiwa kupitia nguvu yako, ni lazima uijue nguvu yako kwanza,

Wewe ndani yako unamuona nani? Msanii, mfanya biashara, muandishi? Mwanasiasa? Mkulima? Mkufunzi? Muhandisi? Au unajionaje kwa ndani kabisa ya moyo wako?

Lazima kwanza uwe muwazi kwa ndani, kisha jihakikishie kuwa Ndivyo unavyojiona.

Amini kuwa inawezekana kuwa vile unavyojiona kwa ndani, dhamira kuwa vile vile na weka nia kuwa lazima uwe vile. Imani ni Ufunguo wa Mafanikio Yoyote na ufunguo wa nguvu iliyo ndani yako

Ikubali na ipokee nguvu yako bila kujiwekea vikwazo vyovyote vya nje

Ukishajua nguvu yako ya ndani, sasa ikubali kwa kwa mikono yote, Haijalishi kwa wakati huo unafanya nini,

Usijewekee vizuizi wala vikwazo kabisa, wewe kubali lazima iwe na itakuwa!

Kama ndani yako unajiona kuwa wewe ni mfanyabishara mkubwa wa nguo, hata kama kwa sasa Huna hata shillingi moja ya mtaji simamia nguvu yako!

Kama ndani yako unajiona ni mwanariadha mkubwa hata kama hujawahi kuikimbia umbali wa kilometre moja, wewe Amini hivo hivo.

Vyovyote ujionavyo kwa ndani amini inawezekana hata kama kwa sasa unafanya kitu tofauti kabisa

Kila siku fanya kitu kimoja hata kama ni kidogo kuelekea ndoto ya nguvu yako uliyonayo

Ukisha ipokea nguvu yako ya ndani bila kikwazo chochote sasa anza na utekelezaji na usiwe na haraka!

Usikubali siku iishe kabla hujafanya kitu chochote kuelekea kutimiza ndoto ya nguvu yako ya ndani,

Badili muonekano, tabia, na punguza baadhi ya marafiki ambao hawaendani na vile unavyojiona kwa ndani,

Mfano unajiona wewe ni mwanasiasa wa baadae, sasa anza kujiunga na chama ukipendacho,

                    Jiweke karibu 

Jisogeze karibu na shughuli za chama hata za mtaani kwako na jiweke karibu na wanasiasa walio mtaani kwako kidogo kidogo na jenga urafiki au mazoea nao

Fatilia mambo yote ya siasa za ndani na nje hata kwenye mitandao au redio, kila siku au mara kwa mara

Andaa mipango na mikakati yako na namna utakavyokuwa mwanasiasa bora  na mambo utakayo wasaidia wananchi.

Ongeza kasi ya ufatiliji kidogo kidogo mpaka utapofikia kilele chako

Tafuta njia yako na kila siku jifunze kitu kipya kupitia nguvu unayoiona ndani yako

Kila mtu ana njia zake, na wewe tafuta zako za kipekee na kamwe usimuige mtu yoyote!

Ishi ndani ya nguvu yako ya ndani kwa misingi na njia unazo ziamini wewe mwenyewe bila kuiga kwa yoyote

Pia jifunze mambo mengi na mapya kila siku kuendana na vile unavyotaka kuwa

Jikubali, jiamini na usijilinganishe na mtu yoyote hata kama amekuzidi vile unavyotaka kuwa

Kila mmoja ana wakati wake ndio maana kuna watu wengi mabingwa na maarufu walivuma sana na kupotea,

Kuna” kifo”, maradhi, changamoto za maisha na hata nyakati kuisha za watu walio kwenye vilele fulani

Hivyo kamwe usiogope wala kuumiza kichwa kwa aliye kutangulia maana kila mmoja ana wakati wake!

Linganisha maisha yako ya sasa na ya nyuma, ya leo na jana Ila kamwe usikubali kujilanganisha na mtu yoyote

Kwanini watu hawafanikiwi kupitia nguvu wanayoiona ndani yao?

  • Kukosa imani ya kile wanachokiona ndani yao
  • Uoga wa kushindwa kuwa vile wanavyojiona ndani yao
  • Kujinganisha na wengine waliowazidi na kuona hawawezi kuwa kama wao
  • Kupuuza wajionavyo kwa ndani na kufanya mambo mengine
  • Kutaka mafanikio ya haraka na njia za mkato na kujikuta wakifanya mambo nje ya walivyo kwa ndani
  • Imani potofu na mazoea ya jamii kama vile mwanamke anatakiwa kukaa na kulea familia!

Hitimisho

Kila mmoja ana nguvu ndani yake, ameumbwa kwa lengo na kusudi maalumu hapa Duniani na anauwezo wa kuwa vile anavyotaka yeye! Anza sasa kuchukua hatua.

Share this article
Shareable URL
Prev Post

Wazo la biashara ya makande

Next Post

Biashara ya wafanyakazi wa majumbani

Comments 5

Acha Comment Yako

Read next

Huruhusiwi ku copy. Asante.