Imani na mafanikio huenda sambamba na ndio siri kubwa zaidi katika mafanikio yoyote hapa Duniani
Imani ni hali ya kuamini katika jambo lolote unalotaka kulifanya hata kabla hujaanza utekelezaji rasmi
Lazima uanze na imani kwanza ili kukupa urahisi katika harakati za kutafuta mafanikio yako
Tafsiri rahisi ya mafanikio ni hali ya kutimiza lengo au malengo fulani katika harakati za maisha ya kila siku
Malengo yametofautiana kati ya mtu mmoja na mwingine hivo hivo tafsiri ya mafanikio imetofautiana baina ya mtu mmoja na mwingine
Lakini pia mafanikio yanaweza kuwa madogo au makubwa kulingana na lengo na uhitaji wa muhusika
Mfano wa aina za mafanikio
- Kununua gari ya aina fulani
- Kuhitimu masomo
- Kuanza familia
- Kuanza biashara
- Kusafiri au kutembelea eneo
- Kununua nyumba au kiwanja na mifano mingine mingi kulingana na lengo la mtu husika
Watu wengi wameshindwa kupata mafanikio katika malengo yao kwasababu,
wamekosa imani katika mambo wanayofanya, Imani ni siri iliyopo katika hatua za mwanzo kabisa katika kuanza safari ya kuyatafuta mafanikio
Imani na mafanikio
IMANI
ni neno dogo Ila limebeba maana kubwa sana katika maisha na mafanikio
Kabla hujaanza kufanya jambo lolote liwe kubwa au dogo kwanza amini
Lazima uamine kutoka ndani ya moyo kwa dhati bila kusita sita wala kuwa na mashaka
Imani yako lazima iwe kubwa kuliko hata jambo unalotaka kufanya
Hakikisha kuwa una maono makubwa na uhakika wa hilo jambo kwanza na hata ikitokea umelikosa basi ni Sawa na kukosa pumzi yako yenye thamani kubwa.
Faida za imani katika mafanikio
- Hufungua mlango wa kwanza wa Mafanikio
- Huongeza hamasa katika ufatiliaji wa lengo
- Huchochea juhudi za upambanaji
- Husogeza mawimbi ya mafanikio karibu na muhusika wa lengo
- Huonesha njia sahihi ya lengo la muhusika na kumfanya asikwame katika jitihada zake
- Hukuondolea vikwazo vyote na hukutenga mbali na mtu au mazingira yanayoenda kinyume na unacho amini hivyo kukuweka katika nafasi kubwa zaidi ya kufanikiwa
- Imani Huongeza mapenzi kwa kile unachofanya au unachotaka na kadiri unavyokipenda kitu ndivyo utakavyo kifuatilia na kutamani kuwa nacho karibu
- Imani Huongeza uvumilivu kwa kile unachokiamini siku zote huwezi kukiakatia tamaa, utahakikisha unasubiri na kuvumilia mpaka pale utakapoona matunda yake
Kadiri imani ya mtu inapokuwa juu basi na hamasa pia huwa juu hivyo kufanya mafanikio kufikika kiurahisi
Hakuna Mganga wala mchungaji au hata shekhe anaeweza kukuponya kwa dawa, maombi au dua zao isipokuwa kinachokuponya ni imani yako pekee
Kama hutoamini kitu hata kama kina ukweli ndani yake basi hutoweza kuuona ukweli huo kamwe
Ukiamini kitu hata kama hakipo kabisa basi ubongo wako utatengeza picha halisi ya kitu kile na kukufanya uone katika uhalisia ule ule na kadiri unavyooa picha katika imani yako ndivyo ambavyo hukusogeza karibu na kitu chenyewe kwenye maisha yako halisi
Ndio maana ukiamini umerogwa hata kama hujarogwa utaanza kuona dalili zote za uchawi na baada ya muda utaanza kuona vitu vinavyofanania na ushirikina katika maisha yako halisi
Imani na mafanikio huenda sambamba
Kabla hujaanza chochote kile Anza kuamini kwanza na kama ukihisi mashaka yoyote basi Acha kwanza
Mpaka pale utapokuwa tayari na kujihakikishia kuwa moyo wako upo na imani kubwa kuliko hata jambo unalotaka kulitimiza
Hakuna uchawi wala miujiza katika mafanikio bali uchawi wako mkuu na muujiza wako mkuu ni imani yako pekee
Pia soma imani.
Comments 1