You Can Win If You Want

Jifunze muda sahihi wa kuwaacha waende7 Min Read

Jifunze kuwaacha waende  watu uwapendao ili uweze kupata amani na furaha ya maisha

Watu wengi imekuwa mtihani mzito kukubali kuwa wanapaswa kuwaruhusu wawapendao kuondoka kwenye maisha yao

wakati mwingine kuwaacha waende ni njia ya kuonesha kuwa unawapenda, unajali na kuheshimu maamuzi yao

Watu wengi hujikuta wakikubali uhalisia wa kuwaacha  watu waende baada ya muda mrefu sana kupita bila wao kujua kuwa walipaswa kuwaachilia mapema zaidi

Baki na somo na jifunze kuwaacha waende 

Kuna ambao huja kwenye maisha yako kukutumia kutimiza malengo na mahitaji yao

Huondoka wanapoona huna faida nyingine kwao

Mateso na maumivu unayopitia hayakutakiwa kuwa kwa kiwango hiko

Ila kwavile ulilazimisha kubakiza watu ambao ulipaswa kuwaacha waende muda mrefu kwenye maisha yako

Kila anaekuja katika maisha yako, huja kwa nyakati maalumu na lengo maalumu

Muda wake na lengo linapotimia asili humuondoa kwako

Hakuna anaekuja kwa bahati mbaya hata kama umejuana nae siku moja 

Na hakuna anaelazimika kubaki milele kwako ili wewe uweze kuishi

Unaweza kubaki mwenyewe 

Kitu pekee cha muhimu ambacho binaadamu yoyote hawezi kuishi bila kuwa nacho ni hewa ya  “OKSIJENI”

Watu wote unaowaona katika maisha yako kwa nyakati tofauti iwe umekutana nae njiani, kifamilia (uzao), kimazingira au hata sababu nyingine yoyote

Wote hao wapo kwa nyakati sahihi, lengo sahihi na wanapaswa kuondoka katika wakati sahihi

Kulazimisha wabaki wakati muda wao umekwisha ndio chanzo kikubwa cha msongo wa mawazo,

Kujidhuru, kudhuru wengine, kuchanganyikiwa, Vifo, na madhara mengine mengi ambayo yanaepukika kwa kujua muda wa kuachilia

Sababu za watu kuja kwenye maisha yako

  • Kukufundisha jambo fulani kama fursa, mafunzo ya kimaisha nk
  • Kukuvusha katika nyakati fulani kama nyakati za huzuni nk
  • Kukusaidia kitu fulani kama mawazo au malighafi na hata pesa
  • Kukuinua katika kiwango fulani kama kielimu, kibiashara nk
  • Kukupa furaha ya muda (mrefu au muda mfupi)

Watu wote hao Haijalishi kiasi gani umewazoea, umewapenda, au umuhimu wa kuwa nao ni mkubwa

Kamwe hupaswi kulazimisha wabaki katika maisha yako pale tu muda wao wa kuondoka unapofika

Kuna watu huondoka kwa sababu za kiasili kama “kifo”,

Hupaswi kulia kila siku kwasasabu tu ulifiwa, kumbuka somo walilokuachia shukuru na waache  wapumzike salama

Jua hakuna atakae baki na wewe milele hivyo jifunze kuwaacha waende 

Na wapo wanaoondoka kwa sababu za kimifumo ya dunia kama, 

mahusiano kuvunjika, watoto wako kukutenga, ndugu kukukataa, marafiki kukuchukia, na mambo mengine mengi

Hutakiwi kuumia na kutumia muda wako mwingi kuwafikiria chukua somo walilokuachia na acha waende wakasadie au wakasaidiwe na wengine

Kwenye maisha kila mmoja wetu ana kila kitu cha kumfanya aishi bila utegemezi wa moja kwa moja kutoka kwa mtu mwingine hata kama huyo mtu ni mzazi wako

Tunapaswa kutegemeana ili kuishi lakini sio utegemezi wa ukaribu, mfano tunategemeana katika ufanyaji wa kazi mbalimbali, uzalishaji, huduma za kijamii na kadhalika

Lakini sio utegemezi wa kwamba bila fulani nitakufa na siwezi kuishi

Bila baba au mama siwezi kuishi, bila mwanangu siwezi kuishi, bila mwenza au mpenzi siwezi kuishi, bila rafiki yangu fulani siwezi kuishi au mtu mwingine yoyote

Kwenye maisha unaweza kuishi bila mtu yoyote kuhusika moja kwa moja katika maisha yako

Hivyo jifunze kuwaacha waende muda wao unapofika

Jiandae kwa kupokea watu bora zaidi 

Unaweza kuachwa na mwenza wako, ukatumia muda mwingi kumlazimisha asiondoke kumbe unapoteza muda ambao ulipaswa kujiandaa kwa mwenza bora zaidi atakaekuja mbele yako

Pia ulipaswa kutumia makosa ya mwenza anaeondoka kujifunza na kuwa bora kwa yule anaekuja baadae

Unaweza kulazimisha rafiki abaki kwenye maisha yako kumbe alikuja kukufundisha kuwa usiamini watu kupitiliza, na unapaswa kuchukua somo lako na kungoja rafiki mwingine

Unalazimisha kubaki na wazazi wako kumbe ulipaswa kuacha waende na wewe kujua thamani ya kujitegemea katika maisha yako

Jifunze kuwaacha waende

Kuna wale ambao huja kutunyanyua na kutuandaa kwa fursa za baadae kupitia ushauri, maoni na mawazo yao

Hivo tunapaswa kubaki na funzo na kuwaacha waende muda wao unapokwisha

Ijue thamani yako, wewe ni mtu muhimu sana na hujaletwa duniani kuishi kwenye maisha ya mtu mwingine

Dalili za kujua kama unapaswa kuacha waende

Ukiona baadhi ya dalili hizi katika uhusiano wowote ulionao basi jifunze kuachia nafasi yako kwao

  • Mawasiliano kupungua bila sababu za msingi
  • Kauli mbaya zisizojali hisia zako
  • Waache waende ukiona makosa na maudhi ya mara kwa mara
  • Hakuna tena uchangamfu wa awali
  • Kuonekana kero kwenye baadhi ya vitu
  • Thamani yako inashuka na huoni umuhimu wako kwao tena
  • Kutengwa kwenye mambo ambayo awali ulipewa kipaumbele na kutafutwa wakati wa shida
  • Kutumia nguvu kubwa kuwa karibu yao

Kuna dalili nyingi sana ila hizo ni baadhi ya dalili utakazoona na kupaswa kuacha waende haraka sana kabla hujaumia zaidi

Mawasiliano kupungua bila sababu za msingi

Hapa unaanza kugundua kuwa hakuna idadi simu  wala meseji ulizozoea kuona kwa siku, wiki au mwezi

Unagundua hata unapojaribu kuwatafuta hukupa sababu ambazo hazina mashiko kama vile ubize,

Ipo hivi hakuna mtu ambae yupo bize katika kuwasiliana na mtu muhimu kwake isipokuwa vipaombele

Utaona ukipiga simu haipokelewi haraka na ikipokelewa utapewa dharura kuwa utatafutwa baadae

Meseji hazijibiwi mapema au  hata kutojibiwa kabisa

Kauli mbaya zisizojali hisia zako

Watu wanaotamani ubaki katika maisha yao siku zote hutumia kauli za unyenyekevu na kauli ambazo hazitakuumiza kabisa

Ikitokea wamekukwaza huomba msamaha haraka na hujitahidi kutorudia tena

Ikiwa kinyume na hapo, ndugu yangu waache wende tu kwa usalama wa moyo na maisha yako

Lakini pia wapo ambao hutamka wazi kuwa hawakuhitaji ila kwakua unahisi bado unawahitaji, 

Utalazimisha hisia zako ziamini kuwa ile Kauli ilikuwa ya bahati mbaya tu

Waache waende ukiona makosa na maudhi ya mara kwa mara

Utaanza kuona unakosewa kila mara na hata ukiwaambia hawajali wala kuonesha kuguswa kama awali,

Jua tu hapo muda sahihi wa kukusanya mabegi umefika na waache aende

Hakuna tena uchangamfu wa awali

Ile hali ya uwepo wako kuwa kama baraka kwao itapungua kwa kiwango kikubwa, 

Kiasi cha kuona kabisa kuna shida mahala hapo waache waende

Utaona hata ukiwa nao hakuna furaha wala hali ya kuongea sana kama mwanzo na hata ukiaga unaruhusiwa haraka sana

Kuonekana kero kwenye baadhi ya mambo

Zile nyakati za kwenda kula bata na nyakati za furaha kwao utashangaa huambiwi tena

Wala hualikwi na ikitokea ukauliza utapewa jibu litakalo kufanya ujione wewe ndio mwenye makosa

Thamani yako inashuka na huoni umuhimu wako tena

Utaanza kujiona huna faida tena kwao maana mambo mengi ya awali hushirikishwi

Huulizwi  tena maswali wala kuambiwa kuchangia maoni na mawazo yako hasa katika vitu vya msingi vinavyogusa maisha yao

Kutengwa kwenye mambo ambayo awali ulipewa kipaombele na kutafutwa wakati wa shida

Hapo waache tu waende moja  kwa moja kwa moja wala usiwe king’ang’anizi kabisa

Maana mambo yapo wazi kuwa sasa huna tena ushawishi wala umuhimu wowote

Kitendo cha kulazimisha mambo Ndio maumivu yanakuwa makubwa zaidi

Lakini pia unapoona nyakati zao za huzuni na matatizo wewe Ndio kimbilio Lao na changamoto zikiisha huwaoni unapaswa kujifunza kuwaacha waende

Kutumia nguvu kubwa kuwa karibu yao

Hapa sasa ndio utajihisi kama  hali ya kujipendekeza kwao

Unaweza kutumia nguvu ya pesa au hata muda na maongezi lakini bado muitikio unakuwa mdogo sana na hakuna thamani yako yoyote inayoonekana

Unacho paswa kufanya ni kwaacha waende kwani muda wako kwao umekwisha

Kuendelea kulazimisha wabaki ni kujisababishia maumivu makubwa zaidi kuliko vile ambavyo ungeumia mapema

Utajikuta unapoteza muda wako zaidi, muda ambao ungefanya jambo lingine na kukutana na watu wengine wazuri zaidi

Utatumia pesa na malighafi zako kwa wakati ambao sio sahihi na kwa watu ambao sio sahihi

Na kupelekea maumivu kuzidi kiwango ambacho ungeyapata awali kama tu ungekubali mapema kuachilia waende

Faida za kuacha waende

  • Itakuepusha na majuto makubwa
  • Itakusaidia kutoumia sana na kukupa amani haraka
  • Itakupa nafasi ya kukutana na watu wazuri zaidi mapema
  • Itawapa  nafasi wanaoondoka kufurahia maisha mengine
  • Itawafanya wanaoondoka kukuheshimu zaidi na kuona umuhimu wako ukiwa mbali nao
  • Itawapa  nafasi ya kuchagua kama unafaa kuwa nao au hufai
  • Itakusaidia kupata Msaada wakati mwingine kutoka kwao kwani hmtaachana kwa maumivu na migogoro mikubwa
  • Itakupa nafasi ya kuijua na kulinda thamani yako
  • Itakusaidia kuziona fursa kubwa zaidi mbele yako
  • Utajifunza kutumia muda wako kwa watu wengine vizuri na kujiandaa kwa lolote la baadae

Hitimisho

Usikubali kuishi kwa majuto, usiishi kwenye maisha ya watu wengine wala kulazimisha watu kubaki na wewe. Maisha yanapaswa kuendelea kwa namna yoyote ile iwe wapo au hawapo, hivyo tumia muda wako vyema.Pia soma mbinu za kusahau Mambo ya nyuma na kuanza maisha mapya 

Share this article
Shareable URL
Prev Post

Mbinu za kuacha tabia mbaya usiyoipenda 6 Min Read

Next Post

Njia rahisi ya kujitafuta na kujipata8 Min Read

Comments 1
Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Read next

Huruhusiwi ku copy. Asante.