You Can Win If You Want

Kanuni ya sababu, faida na hasara kumi (10)

Kanuni ya sababu, faida na hasara 10 imelenga kutoa hamasa kwa wale wenye changamoto katika kufanya maamuzi au  kuchukua hatua katika malengo yao. Kanuni hii imelenga wale wenye changamoto ya kufanya maamuzi, kuanza au kuendeleza malengo yao,

Uvivu wa aina zote na mambo yote yanayopelekea mtu kukwama na kushindwa kupiga hatua.

Kanuni ya sababu, faida na hasara 10 inatoa muongozo, urahisi, hamasa, na utendaji wa mambo kwa watu wote na aina zote za changamoto na malengo.

Jinsi Ya Kutumia Kanuni Ya ‘Sababu, Faida Na Hasara Kumi (10)’

Unaweza kutumia kanuni ya sababu, faida na hasara 10 katika nyakati na maeneo yafuatayo;

  • Kufanya maamuzi magumu na sahihi
  • Unapohisi uvivu wa aina yoyote
  • Unaposhindwa kuanza utekelezaji wa jambo
  • Unapohisi kuchoka na kutamani kuacha unachokifanya
  • Unapoona mambo yanazidi kuwa magumu

Tumia Kanuni Ya ‘Sababu, Faida Na Hasara Kumi (10)’ Kufanya Maamuzi Magumu na Sahihi

Kila mmoja wetu kuna muda hutamani kufanya maamuzi ya aina fulani katika maisha yake, lakini kuna namna hujikuta anakwama na kushindwa kufanya chochote,

Sio maamuzi yote huwa sahihi na si kila maamuzi yanapaswa kushirikisha wengine kukupa Ushauri.

Epuka kuomba Ushauri kupitia mitandao kama Instagram kwani unaweza kupata Ushauri ambao sio sahihi na kuharibu maisha yako yote.

Unapokuwa katika nyakati ngumu tumia kanuni ya sababu, faida na hasara 10 kukusaidia kwa kuorodhesha;

“Sababu 10” “Faida 10” na “Hasara 10”

Za kwanini unataka kufanya maamuzi hayo.

Mfano Wa Kwanza

Kwanini unataka kumuacha mke au mume wako, faida zipi utapata na hasara gani utapata, japokua mna watoto na mmeishi miaka mingi.

Anza kuorodhesha sababu bila kufoji wala kujidanganya, andika kile kilicho sahihi mfano:

  • Hakuna upendo kati yenu tena
  • Kushindwa kumudu majukumu ya kazi
  • Ugomvi wa kila mara
  • Uvunjivu wa heshima wa wazi
  • Usaliti
  • Ulevi kupindukia
  • Afya ya akili na mwili (kuwaza sana)
  • Dharau, kejeli na masimango ya wazi
  • Changamoto za fedha na uwezo duni
  • Kukosekana kwa hisia za mapenzi kwa ujumla

Hivyo unaweza orodhesha sababu zako zingine zozote lakini hakikisha zina uzito na hukwami kwami katika kuzitaja pia Ndio kweli sababu zinazokusumbua moyoni,

Ukimaliza orodhesha faida 10 utakazopata baada ya kuachana mfano;

  • Kupata muda wa kujitafuta upya
  • Kurudisha amani na furaha upya
  • Kurudisha heshima
  • Kuweka Sawa afya
  • Kuepuka kesi na kifo cha kujitakia
  • Kupata mwenza sahihi kwa baadae
  • Kuepuka maradhi yasiyotibika
  • Kulea watoto katika misingi mizuri bila kushuhudia ugomvi wa wazazi
  • Kupata muda mzuri wa kufanya kazi na kukua kiuchumi
  • Kumpa mwenza nafasi ya kujitafuta kwenye mahusiano mengine

Kila jambo lina faida na hasara zake hivyo lazima ujue hasara ya maamuzi unayotaka kufanya mfano;

  • Watoto kukosa malezi ya wazazi wawili kwa pamoja
  • Kukosa muelekeo wa mahusiano kwa kipindi fulani
  • Kushindwa kumudu baadhi ya vitu ambavyo hukuvizoea kabla kufanya peke yako
  • Maumivu ya kuachana na kuzoea upweke
  • Jamiii na wazazi kutokukuelewa katika hatua za mwanzo za kuachana
  • Kuwepo kwa chuki baina ya familia zenu
  • Kugawana Mali
  • Maumivu kwa watoto
  • Kushuka kiuchumi
  • Historia mbaya isiyofutika katika maisha yako

Ukiona unakwama katika kuandika sababu 10, faida 10 basi Acha mara moja maamuzi yako kwa wakati huo au ukiona hasara ni nyingi kuliko faida na sababu pia Acha kufanya maamuzi yako.

Kanuni hii itakusaidia kufanya maamuzi sahihi kwa wakati sahihi bila kuhitaji Ushauri kutoka kwa watu wengine.

Tumia Kanuni Ya ‘Sababu, Faida Na Hasara Kumi (10)’ Kwenye Jambo Lolote

Mfano unataka kuacha kazi, kubadili kazi, kugombana na mtu, kuanza au kufunga biashara, kununua kitu chochote cha gharama kubwa, kuanzisha uhusiano na mtu, kuhama eneo au nchi, kuanza mazoezi au kuacha mazoezi nk

Unapohisi uvivu na kutaka kuacha unachokifanya tumia kanuni ya sababu, faida na hasara 10. Pia soma Alama za nyakati na mafanikio

Share this article
Shareable URL
Prev Post

Dawa ya msongo wa mawazo

Next Post

Wazo la biashara ya makande

Acha Comment Yako

Read next

Huruhusiwi ku copy. Asante.