Utangulizi
Kubadili maisha milele inawezekana kabisa bila kujali kwa sasa upo katika kiwango gani na unataka mabadiliko ya kiwango gani
Maisha ni zawadi ya kila mtu kutoka kwa Mungu na lazima kuyaishi katika kiwango cha juu sana kama inavyopaswa.
Akili ndio kiini kikubwa cha maisha ya mtu yoyote kupitia mawazo yake hivyo ili kubadili maisha lazima kubadili akili,
Kwa maana ya kubadili namna ya kufikiri au hata namna ya kuchukulia mambo katika mtazamo chanya badala ya mtazamo hasi.
Linapokuja suala zima la kubadili maisha milele kwanza kabisa hupaswa kuanza kwenye akili kwa maana ya upande wa kufikiri
Bila kusahau imani na dhamira ya dhati ni muhimu sana kwa sababu safari ya kubadili maisha sio safari ndogo wala nyepesi,
Inataka kujitoa na kuamua kwa dhati kutoka ndani ya moyo wa mtu husika bila kulazimishwa na mwingine.

Hivyo katika makala hii tutaangalia mambo ambayo husaidia zaidi kwenye namna ya kubadili maisha ya mtu yoyote milele.
Mambo 10 Ya Kwanza Upande Wa Maisha Binafsi Yanayo Saidia Kubadili Maisha Milele
- Badili mtazamo na kuwa chanya kwenye mambo yote yanayo kuzunguka na kamwe usiwaze mambo mabaya hata kama kweli yapo na jisamehe pale ulipo jikosea kisha amua kuanza upya
- Amka mapema sana kila siku na anza siku yako kwa matumaini makubwa sana na imani ya kufanikisha kila utakachofanya
- Fanya mazoezi ya viungo mara kwa mara na kuweka kama sehemu ya ratiba ya maisha ya kila siku ukiweza anza angalau nusu saa kila siku mpaka utakapo zoea
- Tandika kitanda mara tu baada ya kuamka asubuhi na safisha mazingira yote ya chumba au nyumba unayoishi
- Panga chumba na ondoa makorokoro kwenye nyumba unayokaa hasa ambayo hayana maana wala faida, punguza vitu ndani ili kubaki na vichache vyenye matumizi muhimu tu
- Fanya tahajudi kila siku usiku au asubuhi sana angalau dakika 20 au zaidi ili kufanya akili kufikiri vizuri zaidi
- Panga malengo na fanya tathmimi ya malengo yako mara kwa mara kabla ya kulala na hakikisha umefanya angalau kitu kidogo kinacho kusogeza karibu na malengo yako kila siku
- Tenga muda wa peke yako ili uweze kuzungumza na nafsi yako na kujua hasa kitu gani unataka kwenye maisha unayoishi
- Kula chakula chenye mlo kamili na kunywa maji mengi kila wakati
- Jinenee maneno mazuri hata pale unapoona mambo ni magumu sana au kukutisha kwenye safari ya kubadili maisha yako milele.

Mambo Kumi Ya Pili Kwenye Maisha Na Watu Wengine
- Epuka ugomvi na mtu yoyote yule wala usipende kabisa kurushiana maneno pasipo na msingi wowote, jifunze kusamehe hata kama hujaombwa msamaha
- Usilazimishe mtu kukuelewa au kukubaliana na mawazo yako ,elewa kuwa kila mmoja ana haki ya kuwaza tofauti na mwingine na hilo sio tatizo kabisa
- Usilinganishe maisha yako na maisha ya mtu yoyote kamwe, weka akili yako yote kwenye njia na malengo yako tu kitu kikubwa ni kujifunza kwa walio kutangulia sio kushindana nao au kuwaonea wivu ukishindwa kabisa basi fanya kama huwaoni
- Epuka kuambatana na watu wasio na mawazo chanya au wenye tabia tofauti na tabia zako au zile tabia nzuri zaidi
- Tafuta marafiki wapya wanaojituma na kuwaza fursa za maisha na wenye mawazo chanya kuhusu mafanikio hata kama bado hawajafanikiwa
- Usilazimishe kushinda kila mashindano hasa yale yasiyo na faida zozote kwa maana kuwa sio kila kitu lazima ushinde
- Kumbuka kukataliwa ni mtaji na utumie vyema kufika mbali zaidi
- Kwepa kabisa watu wenye msongo wa mawazo na wanaopenda kulalamika kila saa watakuambukiza nguvu hasi
- Heshimu mipaka wanayo kuwekea watu kwenye maisha yao na usilazimishe kupendwa pale unapo chukiwa
- Usipoteze muda kuchukia mtu yoyote kwani utajiumiza wewe mwenyewe kubali uhalisia na endelea na maisha yako bila chuki.

Fungu La Mambo 10 Mengine Kwenye Kubadili Maisha Eneo La Kipato
- Tafuta kazi ya kufanya hata kama ina malipo kidogo na kama unayo basi ifanye kwa mapenzi yako yote na jitihada zote
- Angalia namna ya kujiajiri na kufanya kitu wewe binafsi nje ya kazi ya kuajiriwa unayofanya
- Jifunze ujuzi mpya unaoweza kukulipa zaidi kulingana na maisha yanavyoenda nje ya ujuzi au taaluma uliyo nayo
- Soma sana vitabu na mambo yanayokujenga zaidi kifikra angalau dakika 10 mpaka 30 kila siku
- Chunguza fursa mpya mara kwa mara usiache siku ipite kabla hujajua uchumi wa Dunia au nchi yako unavyoenda ili kuboresha kipato chako
- Tafuta namna ya kuingiza pesa ukiwa umelala au kuingiza pesa bila kutegemea uwepo wako eneo la biashara au kazi unazofanya
- Jifunze mambo mapya kila wakati kuhusu taaluma na ujuzi ulionao ili kuongeza thamani zaidi kwenye kitu unachofanya
- Wekeza kwenye vitu vinavyopanda thamani kila upatapo pesa au fursa ya uwekezaji
- Panga bajeti nzuri na mara kwa mara kagua kipato na matumizi unayofanya ili kuhakikisha upo salama zaidi
- Weka akiba ndogo ndogo kwani akiba ya leo ndio msaada wako wa kesho.

Mambo Mengine Yanayo Saidia Kubadili Maisha
- Usafi wa mwili na mazingira
- Kuwa na mavazi mazuri hata kama machache kuliko mengi yasiyo na maana
- Kushukuru mara kwa mara na kuona changamoto kama fursa ya kukua zaidi
- Kutozingatia sana mambo yasiyo na maana hasa yale madogo madogo hata kama yanakera na kuumiza
- Kupunguza matumizi ya mitandao ya kijamii au kuacha kufuatilia kila jambo mitandaoni hasa yale yasiyo na faida
- Kupanga malengo makubwa yanayo tisha sana lakini kufanya utekelezaji kidogo kidogo bila haraka wala presha kubwa
- Kuzuia hisia za hasira kupitiliza NK.
Hitimisho
Kuna mambo mengi sana ambayo husaidia kubadili na kuboresha zaidi maisha ya mtu yoyote aliye amua kubadilika haijalishi yuko wapi
Kimsingi hakuna kitu kinacho shindikana kabisa na kila mtu ana uwezo wa kuishi maisha anayotaka kwa namna anayotaka
Inataka jitihada na subra za dhati kufanikisha jambo lolote kwenye maisha pasi na kukata tamaa wala kuishia njiani
Haipaswi kurudi nyuma moja kwa moja, ila unaweza kupumzika kidogo pale mambo yanapokuwa magumu kisha kuendelea baadae.