Kwanini tunapaswa kujenga heshima?
Kujenga heshima ni jambo la lazima lenye manufaa sana na umuhimu mkubwa kwa kila mmoja
kwani tabia zako ndio huwapa watu wote ishara kamili ya namna ulivyo kwenye maeneo yote
Nimekuandalia mbinu ambazo unaweza kutumia ili kujenga heshima katika jamii yote inayokuzunguka
Tumia mbinu hizi kujenga heshima katika jamii
Kuwa na muonekano wenye heshima
kuanzia mavazi yako na namna unavyo tembea, jitahidi kuwa nadhifu muda wote hata kama juna mavazi ya aina nyingi
Vaa nguo zinazoendana na umri wako pia zinazoendana na mahala unapoenda
Kuwa msafi na jitahidi angalau kujikagua kabla hujatoka ndani ya chumba chako
Jiulize hivyo ulivyo vaa ikitokea ukakutana na mtu unae muheshimu sana utakuwa na uwezo wa kujiamini mbele yake?
Au mavazi uliyo vaa kama angevaa mtu mwingine je bado ungemuheshimu?
Lakini pia jiulize ukikutana na mtu kwa mara ya kwanza atapata tafsiri gani kupitia mavazi yako hata kabla hujazungumza neno lolote?
Chagua marafiki wenye heshima
Ndege wafananao huruka pamoja, huu ni msemo ambao unaaminiwa sana na jamii zetu
Hata kama upo tofauti na marafiki ulionao lakini huwa ni ngumu sana jamii kuamini kuwa hufanyi yale marafiki zako wanayo yafanya
Kama una marafiki wezi jamii huamini hata wewe ni mwizi, ukiwa na marafiki waasherati pia utaonekana muasherati
Hivyo epuka sana marafiki ambao hawana mipaka katika kulinda heshima zao ili na wewe uweze kuwa katika nafasi nzuri sana ya kuheshimika
Simamia majukumu yako ipasavyo
Ili kulinda heshima yako jitahidi sana kusimamia majukumu yako ya maisha, kazi, familia na kila eneo lako ipasavyo bila kusukumwa au kulazimishwa
Kuwa mtu ambae upo makini na kila jambo linalokuhusu na lifanye kwa uhakika wa hali ya juu
Ili hata ikitokea bahati mbaya hujafanya basi watu wengine waelewe haraka tu kuwa ulipitiwa na utafanya bila shida
Watendee wengine vile unapenda wewe kutendewa
Hii ni pamoja na kuheshimu wengine bila kuchagua hali zako za maisha, umri wao, kazi zao, wala kitu kingine chochote
Chukulia watu wote ni Sawa na wanastahili kuheshimiwa hata kama uhalisia wa tabia zao haupo hivo
“Ukiheshimu wengine na wao watakuheshimu”
Jiwekee mipaka, heshimu mipaka ya wengine na jifunze kusema hapana
Usikubali kila jambo hasa kama lipo nje ya ratiba zako au uwezo wako, saidia watu kile unachoweza na sio kila wakati
Lakini pia weka taratibu zako na zifuate chagua mambo ya kushirikisha wengine na mambo yako binafsi na hakikisha hakuna anaevuka mipaka ya maisha yako
Na ikitokea mtu kavuka mipaka kemea mara moja kwa utulivu na hekima
Lakini pia heshimu mipaka ya wengine na endapo hawapendwezwi wewe kuwa sehemu ya maisha yao jiondoe mara moja na usilamishe uhusiano aina yoyote
Jifunze kujitegemea ili kulinda na kujenga heshima yako
Kama umefikia umri wa kujitegemea maisha yako, fanya hivo mara moja
Hakikisha kuwa unasimamia majukumu yako ya maisha bila usaidizi kutoka kwa watu wengine tafuta kazi hata kama utaingiza kipato kidogo
Ikiwa unaona bado huwezi kuishi mwenyewe usilazimishe sana ila wakati,
unajipanga kujitegemea onesha jitihada na saidia majukumu madogo madogo ya nyumbani
Ukikosewa usikae kimya onesha hisia zako na zungumza kwa heshima kukemea hilo
Usiwe mnyonge kiasi cha kuonekana mjinga kila mahala,
Kama umevunjiwa heshima usikae kimya kwa kuogopa cheo cha mtu au umri wa mtu
lakini pia usianzishe ugomvi wala kujibu kwa hasira badala yake mfate pembeni aliyekukosea na zungumza nae kwa nia njema
Jipende na onesha upendo kwa wengine
Hakikisha kuwa unaanza wewe kujipenda na kisha penda watu wote bila kuchagua wala kufanya upendeleo,
Chukulia kila mmoja kama unavyojikulia wewe na jitahidi sana kufanya watu wawe huru wanapokuwa na wewe kwa kuzungumza nao bila kuonesha dharau wala majivuno
Epuka ahadi za uongo na tabia za udanganyifu
Siku zote usiahidi kitu ambacho huwezi kutimiza hata kama ni kidogo,
Kwani watu huwa na tabia ya kutunza kumbukumbu na ikitokea mara kadhaa umeahidi na hujatekeleza basi hukuweka katika kundi la watu waongo
Pia usiwe mtu wa kudanganya danganya mara kwa mara japokuwa kuna muda uongo husaidia kuweka mambo Sawa Ila isiwe kila nyakati
Tumia uongo pale tu inapobidi na pale ambapo ukweli hauwezi kuweka mambo Sawa
Usiongee sana na kuwa wa mwisho kuzungumza
Jitahidi kulinda heshima yako kupitia ulimi wako, kwani kimtokacho mtu mdomo mwake ndicho kilichomjaa moyoni mwake
Kumbuka kauli huwa hazirudi nyuma, hivo kitu kikubwa zaidi katika heshima ni kauli zako
Bora ujulikane kwa kutoongea kuliko kujulikana kama muongeaji ambae hana heshima kwa kauli zake
Jitahidi kusikiliza wengine kwanza kisha wewe toa maoni mwishoni,
Itakusaidia kuzungumza kile ambacho wengine wamekisahau na kukufanya uonekane una akili nyingi
Sikiliza wengine na wape nafasi
Usiwe mtu wa kuona mawazo ya wengine hayana maana hata kama umewazidi akili, cheo au uchumi
Siku zote jua kuwa hakuna mkamilifu na kila mtu ana mawazo tofauti na mwingine hivo kuwapa nafasi wengine husaidia kujenga kitu bora zaidi
Zuia hisia zako
Kuna aina nyingi za hisia kama huzuni, hasira, furaha na nyinginezo,
Ili kulinda heshima yako hakikisha kuwa una chagua aina ya hisia ya kuionesha mbele za wengine
Hususani hisia mbaya kama hasira kwasababu huweza kukupelekea kufanya jambo ambalo litakuvunjia heshima yote uliyo jenga miaka yote
Jitokeze na onekana kwenye matukio muhimu na toa ushirikiano
Matukio kama misiba, harusi, sherehe mbali mbali husaidia sana kujenga na kulinda heshima yako katika jamii inayokuzunguka
Ni vizuri kuhudhuria na unapokosa muda toa kudhuru yako mapema
Lakini kujenga heshima ni pamoja na kushirikisha katika kazi mbali mbali sio kufika na kukaa tu bila kusaidia wengine pale unapoweza
Kubali makosa na omba msamaha
Hakuna binaadam ambae hakosei kwani hakuna mkamilifu, hivyo unapogundua umekosea hakikisha kuwa una kiri kosa lako na kuomba msamaha wa dhati
kisha haraka rekebisha makosa yako hata kama umemkosea mtoto wako au mtu unae mzidi umri na cheo
Epuka ugomvi ili kujenga heshima yako nzuri
Waswahili wanasema muungwana akivuliwa nguo huchutama
Kuna nyakati utakutana na maudhi mengi sana na ambayo yatakupelekea hasira na kutamani kugombana au kurushiana maneno
Hata kama kweli umekosewa jitahidi kuwa na busara na kamwe usigombae na mtu kwa sababu zozote zile
Ukiona jambo ni kubwa na haliwezekani kutatuliwa kwa mazungumzo basi fata sheria
Ugomvi ni adui mkubwa wa heshima hivo jitahidi na kuwa makini sana
Tumia mitandao ya kijamii vizuri
Epuka kutukana, kujibizana, au kuchangia maudhui yasiyofaa mitandaoni hata kama huoneshi sura yako
Kumbuka dunia hii ni ndogo sana na kuna siku lazima kila jambo litakuwa wazi na hivo kushushia kabisa heshima yako
Mtandao kama jamiiforums ni sehemu nzuri sana ambayo mtu huweza kujifunza na kuchangia chochote bila kuonesha sura wala jina halisi,
Hii huwapa watu nafasi ya kuandika mambo yasiyofaa kwakua wana uhakika wa siri zao kutokuwa wazi
Na kusahau kuwa mitandao inatunza kumbukumbu na kuna siku mambo yanaweza kwenda kombo na kuwa wazi hivo kuleta madhara katika heshima yako nzima
Omba msaada
Ukitaka wengine wa kuheshimu zaidi basi waombe msaada hata kama ni Msaada kidogo,
Kwani hakuna ambae hahitaji msaada kabisa kwenye maisha, hata kama una pesa nyingi kuna wakati utahitaji watu wengine wakusaidie mambo kadhaa
Jambo hili litafanya jamii na wanaokuzunguka kufurahia na kuona kuwa hata wao wana umuhimu katika maisha yako.
Hitimisho
Nimuhimu kulinda heshima zetu kwani maisha ni mafupi sana na hatujui kesho yetu itakuwaje
Unae mdharau leo kesho huenda akawa Msaada wako mkubwa kesho
Hivo inatupasa tujifunze kuwa maisha hayana kanuni maalumu na tusidanganywe na mali, vyeo, familia na hata afya za sasa.
pia soma mafanikio.