Ipo njia rahisi ya kujitafuta na kujipata katika maeneo yote ya maisha
Tumia njia hii kila unapohisi hujafikia kiwango cha maisha unayotaka
Maisha yana mchakato mkubwa kwa kila mmoja wetu katika namna tofauti,
Kila mtu hapa duniani ana kila kitu kinachotakiwa ili afanikiwe
Haijalishi utofati wa rangi, mipaka ya nchi, utofati wa maumbile hata asili
Utofati wa maisha ni kama alama za vidole
Kila mmoja ana alama zake za vidole ambazo hazifanani na mwingine, lakini matumizi ya mkono mzima ni yale yale na uumbwaji wa mkono ni uleule
Kama alivyo mzungu, muafrika, muhindi, na watu wa nchi zingine zote
Haijalishi mtu ana mafanikio makubwa kiasi gani au ana nafasi kubwa kiasi gani kumbuka unaweza kumfikia au kumzidi
Lakini kwa njia tofauti na yake, bila kujali sababu zingine za kimazingira na kijografia
Mafanikio ni kama channel ya redio na mawimbi ya sumakuumeme

Kuna mchakato mkubwa ambao hufanya channel ya redio kusikika na kwa ufupi tu ni kuwa ili channel iweze kushika na kusikika basi lazima kuwe na redio yenyewe, mawimbi ya sumaku umeme, antenna, namba za mawimbi nk
Hivo ili channel isikike lazima mawimbi ya sumaku umeme yasafirishwe na kupokelewa na antenna husika
Katika maisha yako pia ili uweze kufanikiwa jambo lolote lazima uwe katika “mawimbi sahihi ya mafanikio yenyewe” yani malengo ni kama redio,
Kwahio lazima uwe na antenna ambayo ni kama njia au mbinu na pia ukae katika mawimbi yanayonasa mafanikio yako na uwe na namba za malengo yako
Najua ni ngumu kidogo kuelewa Ila utaelewa taratibu endelea kusoma
Chukulia mfano unataka kusikiliza channel ya BBC, lakini umeweka channel namba ya TBC ukweli ni kuwa utaendelea kusikia TBC ileile,
Au unataka kusikiliza BBC na umeweka namba sahihi za channel lakini umekaa sehemu ambayo mawimbi ya sumaku umeme hayafiki, hivyo utasikia chenga za redio tu
Ndio maana hukuta watu wanahamisha redio zao sehemu tofauti tofauti ili kushika mawimbi sahihi ya channel wanazotaka
Au mfano mwingine rahisi ni kutumia mitandao ya simu
Kama unataka kutumia mtandao wa vodacom ni lazima uwe sehemu ambayo vodacom inakamata mawimbi yake kupitia mnara wake
Sasa chukulia upo kijiji kama magarama kigoma, kule mnara pekee wa mtandao uliopo ni halotel
Halafu wewe unataka vodacom uhalisia ni kuwa hutofanikisha lengo hata kama una vocha ya milioni moja
Kwahio hapo kuwa na vocha kwenye line ya mtandao hata kama ni kubwa sio shida, Ila shida ni je mnara na mawimbi ya mtandao huo upo?
Kwahio maamuzi yatabaki mawili uhame ukatafute mawimbi kwa kusogea eneo sahihi au utumie mtandao uliopo eneo hilo
Ndio maana pia watu hujaribu kuinua simu zao juu au kuhamishia sehemu mbalimbali kwa lengo la kukamata mawimbi sahihi ya mtandao husika
Hivyo katika maisha pia lazima upate mawimbi sahihi kwanza Ndio uone mafanikio
JARIBU MAMBO MENGI KADIRI UWEZAVYO ILI UPATE SUMAKU UMEME NA MAWIMBI YA MAFANIKIO YAKO
Usiogope kujaribu
Maisha sio kitu tuli, Ila maisha ni kitu kinachofaa badilika badilika (life is not static but life is dynamic)
Usikariri maisha ya aina moja, jua kuwa maisha yanabadilika kulingana na sababu nyingi sana
Hutakiwi kukariri au kukaririshwa kitu kile kile kwasababu zozote
Unapaswa kujaribu mambo mengi sana kama unataka kujitafuta na kujipata
Jua kitu gani unataka kujipata na Jaribu kwa mbinu tofauti tofauti mpaka upate mawimbi yako
Hujarogwa wala huna mikosi Ila tu hujapata mawimbi yako ya sumaku umeme katika kukuletea mafanikio
Watu waliofanikiwa sana katika maeneo kama familia, uchumi, taaluma, uongozi, ujuzi na vitu vingi
Sio kwamba ni watu wenye bahati sana au watu maalumu sana Ila tu wamejipata kwa kujua channel zao zilipo
Hivyo unapaswa kujaribu mambo mengi sana kwa muda maalumu ili uweze kujipata katika hatua za kujitafuta
Na kama umejitafuta na tayari umejipata basi epuka kuhamisha mawimbi yako ya sumaku umeme kwani yakipotea ni ngumu sana kuyarudisha
Chukulia mfano mzuri kwa watu unaowajua iwe mtaani au watu maarufu ambao walifanikiwa kujipata lakini wakajitoa katika channel zao kiutani tu
Wakajikuta wamepotea mazima, baada ya muda wanajaribu kurudi tena katika nyakati zao wanashindwa
Ijapokuwa wanafanya mambo yale yale kama mwanzo lakini hayawapi mafanikio tena
Ni watu wachache sana ambao hufanikiwa kurudi katika mawimbi yao baada ya kuyapoteza.
Kitu cha msingi ni kuchunga sana ulichonacho kama unahisi tayari umejipata
Mbinu za kujitafuta na kujipata katika kazi
Fanya kazi katika njia tofauti tofauti kila siku mpaka utakapo gundua njia rahisi zaidi
Ambayo ukiifanya inakupa matokeo ya haraka na unawahi kumaliza haraka
Iwe kazi za nyumba, shuleni kama kujisomea,kazi za kuajiriwa au kazi binafsi
Kila siku kuwa mbunifu na fanya vitu vipya unavyoona vinafaa bila kuogopa
Lakini pia kama umeajiriwa Jaribu kutafuta kazi tofauti endapo unahisi hio uliyonayo bado haijakufanya ujihisi umejipata
Usiogope kuomba kazi mbali mbali au kufata kazi ambayo umepata fursa mpya
Kujifuta na kujipata katika biashara yako
Kila siku Jaribu mbinu mpya inayokujia akilini, kama ni bei panga na pangua bei zako,
Badili aina ya matangazo na fanya matangazo mbali mbali mpaka upate eneo ambalo ukilifanyia matangazo linakupa matokeo makubwa na wateja wengi
Mfano mitandaoni labda Facebook
Kama ni bidhaa Jaribu kuchukua mizigo sehemu tofauti tofauti mpaka upate sehem ambayo ina bei rafiki na bidhaa zinazopendwa na wateja nk
Lakini pia Jaribu kufanya biashara mbali mbali mpaka upate biashara ambayo ina faida unayotaka na kukupa uhuru unao taka
Kujitafuta na kujipata katika muonekano
Badili muonekano wako kila mara mpaka utakapoona ukiwa na mavazi fulani unajisikia vizuri zaidi
Inawezekana ukiwa na muonekano fulani watu wanakusifia mno
Inaweza kuwa aina ya nguo, viatu, mkato wa nywele au namna unavyosuka nywele zako, pengine aina ya pafyumu, mafuta nk
Kikubwa Jaribu vitu vingi mpaka utapopata kile ambacho kiko bora kwa upande wako na hapo sasa utakuwa katika mawimbi sahihi ya muonekano
Kujitafuta na kujipata katika mazingira
Hama mtaa, kijiji, wilaya, mkoa hata nchi kama uwezo unao, usikae sehemu moja kama jiwe bali unapaswa kuhama hama mpaka utakapopata mawimbi yako ya mafanikio
usikubali sababu zozote zikuzuie hata kama ni familia
Kuna muda mawimbi yako ya sumaku umeme yapo kigoma Ila wewe ulazimisha kukaa tabora
Hapo hata kama una sababu kubwa kiasi gani kama hujajipata eneo uliolopo hama
Au mume na mke mtarajiwa yupo mwanza Ila wewe unakazana kutafuta mwenza dar es Salaam
Jaribu kuhama!
Kujitafuta na kujipata katika mahusiano
Usilazimishe kubaki kwenye mahusiano yasiyokupa furaha, amani na kujihisi umepungukiwa katika mapenzi
Badili aina ya wapenzi mpaka upate mpenzi anaekufanya ujihisi umejipata i
Zingatia na kuwa makini kuna maradhi usije kusema (Mwajuma muhasu kakufanya upate HIV au kaswende)
Usikae kwenye ndoa inayokufanya ulie kila siku eti kisa watu watakuonaje au kwasababu za watoto
Kumbuka maisha ni yako mwenyewe na unapaswa kuyafurahia kwasababu ni zawadi ya muda mfupi sana
Hivyo Basi njia rahisi ya kujitafuta na kujipata ni kujaribu mambo mengi sana mpaka upate kitu bora kwako
Iwee chakula, usafiri, ununuaji wa vitu, ujuzi elimu, hata njia unayotumia kupita kila siku n.k
Kiufupi kila kitu hata kama ni kidogo kifanye kwa njia mbalimbali mpaka upate njia ambayo utaifurahia
Kuwa na subra na uvumilivu
Sio sasa ufanye kitu siku mbili uache kisa unajitafuta, kumbuka kila jambo linataka uvumilivu kwanza
Na hata mawimbi ya redio au mtandao wa simu lazima uvute muda kidogo kabla huja hama eneo lingine
Ili kuona kama hapo ulipo patakamata mawimbi au hapatakamata yani ukiwasha redio ukisikia chenga huwezi kukimbiza sehem nyingine haraka
Lazima ukae kwa muda kidogo kuhakiki kama kweli hapo sio mahala sahihi
Pengine kuna sababu nyingine zinaweza pelekea mawimbi yasishike Ila ukawa sehem sahihi
Jambo la msingi ni kuwa mvumilivu na jipe muda kwanza sio unafungua biashara miaka 2 unafunga
Unakuwa na mpenzi miezi 2 unabadili,
umepata kazi mwaka mmoja unaacha aise hapo utakuwa unakosea
Kikubwa usikae muda mrefu sana sehemu ambayo sio sahihi Ila pia usiondoke haraka
Kwenye kujitafuta na kujipata Usiogope kukosea
Kaa ukijua kuwa hata MUNGU anakoseolewa, viongozi wa wanakosolewa na kusemwa vibaya
Kwahio hata wewe Usiogope kabisa fanya kama Huna masikio wala huoni
Wewe songa mbele tu wataelewa baadae
Pia kwenye kujitafuta usiogope kupoteza iwe pesa, Mali, ndugu, kazi, au kitu chochote kumbuka kuwa ukishajipata utavirudisha vyote au utapata vilivyo bora zaidi
Kitu pekee cha kuogopa ni kupoteza muda maana muda haurudi nyuma
Kumbuka watu wengi hawajajipata sio kwasababu hawakuwa na uwezo huo bali “uoga “wa kupoteza ndio uliwarudisha nyuma
Ndio maana baba na babu zetu wengi wameishia kuwa masikini wakutupwa
Imgawa walikuwa na njia nyingi za kujaribu Ila uoga wa kujaribu uliwakwamisha
Baki ulipo kama imani yako inaamini mafanikio yapo hapo
Kama unaamini utafanikiwa bila kujaribu kitu kipya hata kama bado hujajipata basi tulia zako tu
Muhimu ni imani iwe kubwa, usilalamike, usihuzunike wala kuumia wakati unaendelea kusubiri matumaini yako
Mfano upo kwenye ndoa au mahusiano mabaya lakini unaamini atabadilika hata ipite kila 10 basi tulia nae
Ila tu usiwape watu heka heka za vikao vya usulihishi kila siku,
Usisumbue watu kuomba ushauri kila siku wakati wewe ndio unae amini katika huyo mtu
Kama unaamini katika kazi au biashara yako japo bado unateseka nayo na hakuna faida yani ni kama unapoteza muda
Ila unaamini ipo siku utajipata basi endelea kujitafuta hapo hapo
Maana imani ni Ufunguo wa Mafanikio.