Kukuza biashara inahitaji mbinu mbalimbali za kuzingatia kila siku na kila wakati
Biashara zote zinahitaji mikakati na mipango ili kuweza kuendelea kusimama imara sokoni
Hivyo nimekuandalia mbinu kadhaa zinazoweza kukusaidia kukuza biashara yako yoyote
Mbinu za kukuza biashara
wazo bora
Anza kuwa na wazo bora ambalo linaendana na,
- Uhitaji, uwe na uhakika kuwa wazo la biashara yako linauzika! yani fanya utafiti wakutosha hata kabla hujaanza biashara na wazo na wazo linalojiuza lenyewe
- Ushindani mdogo, Angalau jihakikishie kuwa hakuna biashara au huduma nyingi zinazoendana na wazo la biashara yako kwanza
Ubora wa bidhaa au huduma
Hata kama kuna ushindani mkubwa basi angalau uwe na huduma na bidhaa bora ambazo zinatatua changomoto za mteja moja kwa moja
Jifunze kujitofautisha kwa washindani wengine, yani usikubali washindani wakuzidi maarifa!
Chunguza wateja wanataka nini na weka zaidi ili kukuza biashara yako
Mfano zingatia
- Punguzo la bei
- Ofa mbalimbali kama, vifungashio vya bure au free delivery nk
- Zawadi mbalimbali kwa wateja nk
Lakini pia kwenye ubora wa bidhaa zingatia
- Bidhaa zinatatua changomoto za wateja moja kwa moja
- Zinadumu muda mrefu
- Zina leta hisia za kipekee kama harufu nzuri ya tofauti
- Rahisi kutumia
- Haimuingizi mteja gharama za ziadi nk
Yani wewe mwenyewe jiulize kitu unachokifanya kama ungekuta mtu mwingine anauza ungeweza kukinunua? Au ungerudi tena kununua?
Chapa bora ya biashara (branding)
Jitahidi kuwa biashara yako iwe na Chapa (brand) ya kipekee
Kiasi kwamba mteja hata kama atanunua kwa mara ya kwanza basi asikusahau na akumbuke kila anapotaka kununua tena
Hapa zingatia Haya
- jina la bidhaa/huduma yako
Usiweke jina gumu sana wala refu sana, lisiwe jina lenye maana mbaya wala maana isiyoendana na biashara unayofanya, usiige jina la biashara ya mtu mwingine - logo
Zingatia uwe na logo nzuri na nyepesi unayotumia kwenye biashara yako hata kama Biashara Ni ndogo, hii itasaidia mteja kukukumbuka haraka na inasaidia kujitofautisha hasa unapotangaza biashara yako mitandaoni - Rangi
Weka rangi nzuri za kuvutia kwenye biashara yako kuanzia kwenye ofisi au duka, logo, majarida, kadi za biashara, bidhaa zenyewe na hata kwenye matangazo hapa itafanya mteja akiona rangi fulani kama anahitaji huduma au bidhaa kama yako kwa wakati huo biashara yako itamjia kichwani - Mfumo mzima wa huduma na bidhaa zako za biashara
Tengeneza ladha yako, kuanzia kwenye namna unavyo pokea mteja, vifungashio, aina ya salamu unayotumia, namna unavyoongea nao, masaa ya kufungua na kufunga biashara yaendane siku zote nk
Yani kichwani kwa mteja ajue kabisa muda gani kila akija anakuta upo wazi,
Ategemee nini pale apoingia mapokezi, atarajie nini wakati anapata huduma yako nk
Hii hufanya mteja kukariri na hata kuwapa urahisi kushawishi wengine wenye uhitaji wa na bidhaa au huduma yako hivyo kusaidia kukuza biashara yako
Masoko na mauzo
Hapa sasa ndio sehemu muhimu kwa biashara yoyote, hata kama huko juu umeharibu ila hapa ndio moyo wa biashara
Hakikisha kuwa biashara yako inatangazwa na unajitangaza kila siku!
“biashara ni matangazo”
Kumbuka hata kampuni kubwa kama Coca-Cola kila siku unakutana na matangazo yao
Ijapokuwa ni bidhaa inayojiuza, ipo dunia nzima na ina soko la uhakika
Hivyo lazima ujitangaze hata kama Biashara yako imeshakuwa kubwa
Kila siku jitahidi kutafuta mbinu mbali mbali za kuonekana katika soko
Tumia njia kama
- Magazeti na majarida
- Email na bulk sms
- Redio na Television
- Mitandaoni kama Instagram na Facebook na lipia ads kwa gharama unayoweza
- Mabango ya barabarani
- Semina za biashara, nenda na bidhaa au huduma yako na jitangaze
- Ingiza bidhaa na huduma mitaani na ongea na wateja uso kwa uso
Hapo utachagua namna ya kujitangaza kulingana na uwezo wako
Lakini njia rahisi zaidi ni mitandaoni kama Facebook na Instagram
Hii unaweza fanya bure tu kwakuwa na Akaunti yako maalumu ya biashara yako na utapata wateja wengi sana
Lakini pia kwenye kipengele cha masoko na mauzo hakikisha
- Una bidhaa inayojiuza
- Namna bora ya ushawishi kwa wateja (lugha nzuri na laini inayoshawishi)
- Timu bora ya wauzaji
hapa kama Biashara yako ni kubwa tafuta watu wenye mafunzo imara waingie mitaani na huduma au bidhaa zako wakiwa na sare zenye nembo ya biashara
Kama huna watu (team) na biashara ni ndogo basi ingia mwenyewe sokoni
Usingoje wateja wakufate ulipo! Andaa kadi za biashara (business cards) au vipeperushi
Kila unaehisi anaweza kuwa mteja muachie kadi yako ya mawasiliano
Huduma kwa wateja
Hapa zingatia kuwa mteja anaridhika na huduma au bidhaa kuanzia anavyopokelewa mapokezi au kwenye simu
- Mteja ahudumiwe haraka na kwa ubora mkubwa
- Majibu mazuri kwa wateja (Kauli) kumbuka “mteja hakosei ” hivo mteja lazima abembelezwe
- Kama unafanya biashara yako mtandaoni hakikisha una jibu wateja kwa wakati na waridhike na kile wanachosikia, usikubali mteja akate simu bila kuona kama amerdhika
Uongozi na usimamizi mzuri
Hapa sasa angalia namna unavyo simamia wafanyakazi wako
Usiwe mpole sana wala mkali sana
Kuwa kiongozi ambae anajua namna ya kufanya wafanyakazi wawajibike wenyewe bila kusukumwa
Wafanyakazi wakiridhika lazima watahudumia wateja vizuri na biashara itakuwa
Wafanyakazi wakikosa mapenzi na kazi yao basi biashara lazima itakufa tu hivyo zingatia
- Sikiliza wafanyakazi wakueleze changamoto zao za kazi na zifanyie kazi haraka
- Wape Nafasi ya kutoa maoni mara kwa mara kwenye biashara
- Kuwa na Kauli za kibinadam na utu kwa wafanyakazi wote na usibague wala kupendelea
- Wape motisha hasa wale wanaofanya vizuri katika maeneo mbali mbali ili wazidi kufanya zaidi na wale wengine wapate hamasa
- Kuwa muwazi hasa katika mambo ya biashara kwa kuweka vikao vya mara
- Wape elimu na mafunzo ya mara kwa mara
Kumbuka kuweka vikao mara kwa mara, kuwasikiliza na kushirikisha kinachoendelea ili kurekebisha mambo mapema
Usimamizi mzuri wa fedha
Hapa ndio kama roho ya biashara ili ikue
Lazima ujue namna ya kusimamia fedha za biashara kwa,
- Kudhubiti matumzi ya biashara yako ya kila siku
- Kupunguza na kuondoa mambo yasiyo ya lazima sana
- Kutofautisha matumzi ya binafsi na matumizi ya biashara
- Kuongeza bidhaa na kununua mapungufu yote kwanza kabla ya matumizi
- Kuhakikisha kuwa biashara inajikuza kupitia faida yake yenyewe
Uvumilivu na Uendelevu
Hakuna biashara inayokuwa mara moja, biashara ni kama mbegu ya zao lolote,
Laizma upande mbegu, uizingatie kwa kuihudumia vizuri ili ikuwe
Na pia kuanza kula matunda ya biashara inataka uvumilivu mkubwa
Usiwe na haraka wala tamaa biashara zote zinapitia changamoto!
Jitahidi kuwa na subra na uwe na malengo ya muda mrefu katika biashara yako.