Utawezaje kurudisha thamani yako ?
Kurudisha thamani iliyopotea huweza kuwa jambo lenye changamoto kubwa kutokana na ugumu wa chanzo au hata mazingira
Thamani inaweza kupotea kutokana na sababu mbali mbali za kila siku
Kuna makundi mengi yanayohusiana na upotezaji wa thamani
Thamani inaweza kupotea kwa mtu binafsi, familia hata biashara.
Leo tutaangalia thamani ya mtu binafsi na njinsi ya kurudisha baada ya kupotea
Dalili za kupotea kwa thamani ya mtu
- Kuvunjika kwa heshima na kudharaulika
- Kupoteza mvuto
- Msongo wa mawazo na kuelemewa
- Kutosikilizwa
- Kutokubalika
- Kutopewa kipaombele
- Kupoteza muelekeo wa maisha
- Kupoteza watu wa karibu
- Kukosa Msaada wa haraka
Kupotea heshima
Utajua kuwa thamani yako imeshuka kwa kuona hali ya kuogopwa Inaondoka na kila mtu aliyekuwa anahisi uwepo wako kama awali inaisha kabisa
Utaanza kuona mabadiliko kwa watu wako karibu kama watoto, mwenza, ndugu hata jamii
Watafanya mambo mengi mabaya hata usiyoyapenda mbele yako!
Hakuna anaekujali tena na unaonekana kama haupo mbele yao
Ukiongea kitu, kuomba kitu au kuuliza kitu hutopata kwa haraka au usipate kabisa.
Kupoteza mvuto
Ile hali ya kupendwa uliyokuwa unaihisi mwanzo inaisha
Unaona hakuna tena hisia kati yako na wanaokuzunguka
Hata mke /mume wako, watoto na watu wengine hawakupendi tena na wanakuona mtu wa kawaida kama mtu asiye na maana yoyote kwao.
Msongo wa mawazo
Utaanza kuhisi hali ya kuelemewa sana
Hii hutokana na mabadiliko mengi unayokutana nayo ambayo hukuzoea awali
Inaweza kuwa kazini au nyumbani
Utajikuta kama kuna kitu hakipo Sawa kwenye mwili au moyo wako
Japokuwa kwa mazingira ya nje unaona mambo yanaenda vile vile
Ila kwa upande wako unahisi kabisa kuna mambo yamepungua katika maisha yako ya kila siku
Hii hupelekea kufanya mambo mengi kwa hasira na kuchanganyikiwa mara kwa mara.
Kutokusikilizwa
Hapa utaona kama kila unacho ongea kina puuzwa
Iwe kazini hata nyumbani! Watu hawana muda na maneno yako tena
Hata ukijitahidi kuonesha kuwa upo sahihi hakuna atakae kujali
Hata kama utakuwa sahihi kweli!
Kutokukubalika
Hapa utaona hali ya kutengwa na kuonekana kama nuksi kwa wengine
Iwe mke /mume, watoto, marafiki nk
Utajihisi kabisa hali ya kuwekwa nyuma kwenye mambo mengi
Hutoshirikishwa katika mambo muhimu ambayo mwanzo ulipewa kipaombele
Hutoambiwa vitu vya msingi wala vitu vya furaha kwa wengine
Mara nyingi utajiona kama mtu wa kujipendekeza kwa watu.
Kupoteza muelekeo wa maisha /watu wa karibu na kukosa Msaada wa haraka
Hapa sasa utaona unakosa ramani za maisha yako
Utajihisi kama watu wa karibu yako wametafuta watu wengine
Utajina kama huna maana tena wala huna Msaada wowote unaouhitaji kwa haraka.
Sababu/chanzo cha kupoteza thamani
Tabia
- Tabia
- Changamoto za mara kwa mara
- Kuishi kwa mazoea
- Sababu za kiasili
- Kuyumba kimaisha
- Kutoheshimu /thamini wengine
- Kutosimamia majukumu yako ipasavyo
Tabia
Hapa kuna tabia kama za ulevi, matusi, kejeli, ugomvi dharau nk
Tabia hizi husababisha mara nyingi watu wa karibu yako kukuchoka
Kuna muda watu hukuvumilia kwa kuamini utabadilika,
Lakini muda mrefu ukipita bila kuona mabadiliko huanza kukuzoea na mwisho kuku dharau na kukucha kabisa!
Changamoto za mara kwa mara
Hapa kuna zile changamoto za maisha ya kila siku
Hufanya watu kuchoka shida zako
Kila wakat kulalamika, kuomba misaada, kutegemea wengine na hata kusimulia matatizo yako
Watu huchoka na kuona hawaoni furaha ya maisha yao mengine zaidi ya shida zako
Yani wengi hukupenda pale na wewe una furaha binafsi na unawapa furaha wao
Asilimia kubwa ya watu hawapendi kusikia matatizo ya wengine na husikiliza kwa kejeli tu.
Kuishi kwa mazoea
Hali ya kila siku kuishi kama jana!
Hubadiliki wala kukubali mabadiliko
Kila siku unaishi maisha ya mazoea wakati wengine wanatafuta namna ya kuanza upya na kuboresha mambo yao
Hufanya watu kukuchoka na kukuona kama mzigo!
Hata kama ni mwenza wako au watoto epuka kuzoeleka
Yani ishi maisha ya mtu asijue ukirudi utakuja na nini au ratiba gani.
Sababu za kiasili
Kuna nyakati hufika za watu kuondoka katika maisha yako na wewe kupoteza thamani kwao
Nyakati hizi ni pale hujafanya kosa lolote
Hujawaudhi wala kuvuka mipaka
Lakini bila kujua chanzo unashangaa tu Huna tena thamani mbele yao!
Kuyumba kimaisha
Mfano kufirisika au kupoteza kazi
Uchumi wako ukitetereka lazima na wewe thamani yako ishuke
Wengi huja katika maisha yako sababu kuna kitu wanapata kutoka kwako!
Inawezekana hata huyo mke au mume wako na marafiki wapo na wewe sababu za pesa zako!
Au kuna kitu wanategema utawasaidia
Na siku wakiona huna tena kile wa nachotaka kutoka kwako hukushusha thamani yako yote.
Kutoheshimu!/kutothamini wengine
Kuna ile hali ya mtu kuona wengine kama hawana maana kwao!
Hii husababishwa na Elimu, Mali na pesa
Hivo watu huzoea hio hali na baada ya muda hukuchukulia kawaida kwao.
Kutosimamia majukumu yako ipasavyo
Mfano kutohudumia familia kama chakula, mavazi, ada nk
Kutowajibika kama mke au mume
Kutowajibika katika jamii inayokuzunguka
Kutojua nafasi yako na majukumu yako ya kazi na,
Kutofanya kazi zako inavyotakiwa hupelekea hali ya kuchokwa na kushuka kwa thamani yako!
Usaliti wa mara kwa mara
Hii huwa chanzo kikubwa hasa kwa wanandoa na marafiki
Hali ya kuanzisha mahusiano ya kimapenzi au kirafiki na watu wengine tofauti na mwenza wako au rafiki yako wa dhati
hupelekea maumivu makali kwa mwenza wako na rafiki aliye kuamini sana
Na baada ya muda huamua kushusha thamani kwenye moyo na maisha yake!
Utegemezi
Sana kwa wale ambao hawana kazi na hawataki kujishughulisha kwa lengo la kujisimamia katika majukum yao
Kuna watu hupenda kuishi kwa kutegemeana wenzao kwa kisingizio cha hana kazi!
Hii husababisha baada ya muda kuchokwa na kudharaulika mwisho wa siku kushuka kwa thamani yako.
Hatua za kurudisha thamani iliyopotoea
Kubali thamani yako imeshuka
- Kubali thamani yako imeshuka
- Tafuta chanzo
- Weka mikakati na badili tabia
- Usitumie nguvu kubwa ya maneno fanya kwa vitendo
- Jipe muda
Kubali thamani yako imeshuka
Usilazimishe kujipa thamani kwa watu ambao tayari hawakuthamani
Itafanya wazidi kukuzarau!
Kubali hali yako iliyopo kwa wakati huo na itakusaidia kukupa mwanga wa kutibu tatizo na kurudisha thamani iliyopotoea.
Tafuta chanzo
Huwezi kutibu tatizo bilaa kujua chanzo
Anza kutafuta kwanini hauthaminiki tena? Ili ujue namna ya kuondoa tatizo kwanza
Mfano labda ni tabia za usaliti, ulevi na hata uongo.
Weka mikakati na badili tabia
Baada ya kujua chanzo cha kushuka kwa thamani yako
Sasa jiulize ufanye nini ili upandishe thamani!
Badili kila kitu ambacho kilipelekea wengine kukudharau
Jiwekee malengo ya mabadiliko yako binafsi
Amua kuwa mtu mwingine kwa faida yako mwenyewe kwanza.
Usitumie nguvu kubwa
fanya kwa vitendo
wala usiongee kitu, kuwa unataka kubadilika nk
Maana utawafnya wakuone mjinga zaidi
Wewe Fanya kwa vitendo tu halafu acha wenyewe waone mabadiliko yako.
Jipe muda
Kumbuka hauthaminiki tena! Huna mvuto wala ushawishi
Kwahio itataka muda wa kutosha kuaminisha wengine na wajiridhishe kuwa umebadilika
Hivo hupaswi kamwe kufanya kwa haraka
Endelea taratibu kufanya mambo yako mpaka pale hali itakaporudi kama zamani
Na kuna muda hali inaweza usiweze kurudi na kuwa kama zamani
Yani thamani iliyopotoea kuna muda hairudi kama awali kwahio punguza matarajio.
Njia mbalimbali za kurudisha thamani iliyo potea
- Jitegemee na tafuta kazi
- Jipende wewe kwanza na jipe kipaombele
- Heshimu na thamini wengine
- Simamia majukum yako ipasavyo
- Epuka tabia mbaya kama ulevi, uzinzi nk
- kuwa muaminifu kwa wengine
- Weka mipaka ya maisha yako
- Kuwa msiri na Epuka kulilia watu shida zako au kuomba misaada ya mara kwa mara
Jitegemee au tafuta kazi
Epuka kukaa nyumbani kwenu au kwa ndugu yako yoyote bila kazi
Ikiwa umeshatimiza umri wa kujitegemea hasa kama ni mtoto wa kiume
Na kama kuna ulazima wa kukaa kwa ndugu zako basi angalau changia mahitaji madogo madogo.
Jipende wewe kwanza na jipe kipaombele
Epuka kuishi kwa mazoea!
Anza kujipa thamani kwa kujipenda mwenyewe kabla wengine hawajakupenda
Jipe furaha, vaa pendeza, jitoe sehemu mbalimbali na jiheshimu
Ukiwa mtu unaejijali basi wengine pia watakuja na kukupenda na itakusaidia kurudisha thamani iliyopotoea.
Heshimu na thamani wengine
Kama jinsi unataka wewe kuthaminiwa
Basi lazima pia uthamini wengine!
Usitegemee kuthaminiwa ikiwa unadharau wengine hata kama umewazidi kila kitu.
Simamia majukumu yako ipasavyo
Hakikisha kuwa kila jukumu linalokugusa unasimama nalo
Usiwe mtu wa kutegea wengine wakusaidie yale uliyopaswa kufanya wewe
Kuanzia majukumu ya familia mpaka kazi lazima uyafanye kwa uhakika wote bila kusukumwa au kupigiwa kelele.
Epuka tabia mbaya ni njia nzuri ya kurudisha thamani iliyopotoea
Tabia kama ulevi, uzinzi, uasherati na ugomvi ni chanzo kikubwa cha kudhaurika
Jitahidi uwe na adabu binafsi na kwa watu wanaokuzunguka
Heshimu Kauli zako na usiwe mtu wa kuyumbishwa yumbishwa.
Acha usaliti!
Ikiwa umemsaliti mtu jua kabisa hawezi kukuamini tena
Na itafika muda atakutoa katika moyo na kukushusha thamani
Jitahidi kuwa muaminifu ili uaminiwe pia.
Weka mipaka ya maisha yako
Jitahidi sana watu wasikuzoee kupitiliza
Jiweke mipaka na usikubali watu waivuke
Hii iambatane na kusema hapana kwa vitu ambavyo vipo kinyume na wewe
Pia heshimu mipaka ya wengine.
Kuwa msiri na epuka kuomba misaada ili kurudisha thamani iliyopotoea
Misaada ya mara kwa mara huchosha na kufanya wengine kukudharau
Jitahidi kutunza shida zako na kuzitafutia ufumbuzi wewe mwenyewe bila kuhusisha wengine
Itakusaidia sana kujenga na kurudisha thamani iliyopotoea
Maana hata wengine pia wana shida zao.