You Can Win If You Want

Mbinu za kusahau mambo ya nyuma na kuanza maisha mapya

Unawezaje kusahau mambo ya nyuma? 

Kuna mbinu mbalimbali zinazoweza kukusaidia kusahau mambo ya nyuma na kuanza maisha mapya

Kila mmoja wetu katika maisha yake na kwa nyakati tofauti huumizwa na mambo ya zamani, mabaya, magumu, mazito na hata historia mbaya katika maisha yake

Inaweza yalitokea muda mrefu uliopita au yametoka siku chache zilizopita

lakini hakuna binaadam ambae hajakumbukwa na aina yoyote ya maumivu yanayomtesa

Au yaliyowahi kumtesa na bado yanampa wakati mgumu kila anapokumbuka

Watu wengi wamejikuta watumwa wa maisha yao ya zamani

Wameshindwa kabisa kusonga mbele na wanateseka kila siku bila kujua au kwa kujua

Kuna watu wameshindwa kutimiza ndoto zao mpya kwa sababu ya mabaya yao ya nyumba na wanaishi katika hali ya kujilaumu kila siku

Kwanini unapaswa kusahau mambo ya nyuma? 

Maisha ya zamani haijalishi yalikuwa na ubaya kiasi gani ila hayana nafasi tena katika maisha yako ya sasa

Lazima ujifunze kusahau, kusamehe na kuanza upya kwa kuangalia kilicho mbele yako tu na kutumia nyuma yako kama mafunzo

Inawezekana umeachana na mwenza  uliyempenda na kumuamini sana,

Umesalitiwa na mtu wako wa karibu sana, umefiwa na watu wa muhimu sana, umepoteza mali zako nk

Pengine umefirisika katika biashara yako, umefukuzwa kazi, umepata ajali mbaya na kukusababishia ulemavu wa kudumu,

Ulifanya vitendo vibaya kama vile uasherati kupindukia na umeambukizwa magonjwa ya kudumu, mapenzi ya jinsia moja 

Na mambo mengine yoyote yanayokufanya uwe na majuto makubwa na unatamani kusahau kila kitu cha nyuma 

Haijalishi ulifanya au kufanyiwa nini kitu cha msingi ni kusahau na kuanza maisha mapya na kutengeneza kesho iliyo bora kuliko jana

Vyovyote ilivyokuwa amini kuwa wewe ni mtu wa thamani sana na unaweza kuanza hapo hapo ulipo na kutengeneza mwisho wako uliobora zaidi

Kuna watu wengi ambao wamefanya mambo makubwa sana lakini historia zao za zamani zilikuwa mbaya na hata wao wala jamii zao hawakutegemea kama wangekuwa walivyo sasa

Zifuatazo ni baadhi ya mbinu  unazoweza kutumia na kusahau mambo ya nyuma na mambo mabaya ya zamani

  1. kubali uhalisia na amini inawezekana kusahau kila kitu
  2. Futa kumbukumbu zote za zamani
  3. kuwa muwazi kwa wanaokuzunguka na usione aibu
  4. Samehe waliokukosea na jisamehe mwenyewe pia
  5. Beba lamawa za matatizo yaliyotokea hata kama hukuhusika moja kwa moja
  6. Chukulia kama funzo na mpango wa mungu katika maisha yako yajayo
  7. Jipende na badilisha muonekano wako wa mwanzo
  8. Tafuta kitu  chanya cha kukupa furaha
  9. kata mawasiliano na wanaokukumbusha au kukusababishia maumivu na hama eneo unaloishi sasa /badili kazi unayofanya
  10. Jiweke bize muda mwingi na tafuta muda mzuri wa kupumzika na kuwa peke yako ikibidi fanya sana meditation
  11. Jiweke karibu na watu wenye mawazo chanya na marafiki wapya pia Jaribu kufanya vitu vipya
  12. Usizuie hisia zako (lia sana kama unataka kulia) Ondoa mawazo hasi na usiongelee tena mabaya ya nyuma
  13. Usilipize kisasi
  14. Tafuta mtu wa kuongea nae
  15. Jipe muda zaidi
  16. Anza upya
Kusahau mambo ya nyuma na kuanza upya ni pamoja na kukubali uhalisia uliopo 

Kama umefanya kila ulichoweza kwa nguvu na juhudi zote lakini hakuna kilichobadilika  hivyo,

Kabla hujaanza hata kuwaza kupona maumivu na mateso yako, lazima ukubali kuwa kila kitu kimeisha na huwezi kubadilisha uhalisia uliopo

kutokukubali ukweli hupelekea mateso ya kuendelea kuwa mtumwa wa maisha ya zamani

Haijalishi wewe ndio sababu au kuna sababu tofauti na wewe kitu cha msingi ni kukubali ukweli uliopo kwa sasa na kupokea kwa moyo mmoja

Kubali maradhi yako, kubali umeachwa na kupotezewa muda, kubali umefirisika na umepoteza kila kitu na kubali kila jambo linalokutesa lipokee kama lilivyo kwanza

Kuwa muwazi kwa wanaokuzunguka na usione aibu

Kitendo cha kusema ukweli kwa watu wako wa karibu kama ndugu na marafiki hukupa ahueni na kuona kama umetua mzigo mkubwa moyoni

Lakini pia hufanya wanaokuzunguka wajue maumivu unayopitia na kukupa sapoti ya mawazo na msaada mwingine wowote

Vile vile huwafanya waache kukuuliza maswali ya mambo yako ya zamani na kuangalia maisha yako ya sasa

Ila kama jambo lako ulikuwa unalifanya kwa siri na hupendi wengine wajue basi sio lazima kumshirikisha mtu yoyote kwani huweza kuibua maswali mengi yatakayo kusababishia maumivu zaidi

Samehe waliokukosea na jisamehe mwenyewe pia

Unapaswa kusamehe kutoka moyoni na kuachilia kila kitu na acha kiende kwa moyo mmoja

Hii itakusaidia kusahau na kuanza upya haraka sana

Jisamehe wewe mwenyewe na samehe wengine wote hata kama hawajakuomba msamaha 

Beba lamawa za matatizo yaliyotokea hata kama hukuhusika moja kwa moja

Hii ni mbinu nzuri sana ya kusahau mambo ya nyuma kwani hukufanya ujione wewe ndio chanzo cha tatizo

Mfano umefukuzwa kazi, badala ya kuona kama bosi wako au mtu yoyote kakusababishia hebu waza kuwa wewe ndio ulishindwa kufuata sheria na kanuni za kazi yako

Chukulia mfano umezalishwa na kuachwa, badala ya kuwaza mwanaume alokuacha ni mbaya na alikudanganya, 

Hebu waza kuwa wewe Ndio chanzo na hukupaswa kuamini maneno yake na kubeba ujauzito kabla ya ndoa

Badala ya kuwaza maisha yako yaliharibika baada kifo cha aliyekuwa mtegemezi wako,

Sasa waza kuwa wewe ndio chanzo kwa kushindwa kusimamia maisha yako kwani kila mmoja wetu anapaswa kusimamia maisha yake yeye mwenyewe

Futa kumbukumbu zote za zamani

Kila kinachokukumbusha maisha ya nyuma kifute

Kama ni mitandao ya kijamii acha kutumia kwa muda

Kama ni picha futa zote, kama ni nguo, vitu au kitu chochote kile ambacho ukikiangalia kinakupa kumbukumbu mbaya basi  kiondoe karibu yako

Jipende Na badilisha muonekano wako wa mwanzo

Kusahau mambo ya nyuma na kuanza upya

Hata kama huna pesa, amua kubadilika  kama ulikuwa unanyoa  aina fulani ya mtindo wa nywele zako badilisha mtindo

Kama ulikuwa unapenda kuvaa nguo za aina fulani badilisha aina ya mavazi 

Ikiwa ulikuwa mnene sana anza diet na punguza mwili wako, hii itakusaidia kujiona mtu mpya na kukufanya kuwaza mambo mapya ya maisha

Lakini pia usisahau kujali afya yako kwa kula vizuri mlo kamili

Tafuta Kitu Chanya cha kukupa furaha na hobi mpya

Jichunguze kitu gani huwa kinakufanya ujisikie vizuri sana kila unapokifanya na ongeza bidii kukifanya mara kwa mara

Kusikiliza na kucheza muziki, kuangalia filamu, kuogelea, kusikiliza podcasts nk

Lakini kamwe usifanye mambo mabaya kama njia ya kujitibu kwani utaishia kuangamia zaidi 

Matumizi ya vilevi kama pombe, bangi, madawa ya kulevya sio mazuri kabisa kwani hukupa furaha ya muda mfupi na matatizo ya milele

Safiri sehemu mpya ambazo hukuwahi kufika kabla hata kama ni mkoa au wilaya hio hio unayoishi

kata mawasiliano na wanaokukumbusha au kukusababishia maumivu na hama eneo unaloishi sasa /badili kazi unayofanya

Hii itakusaidia kusahau haraka zaidi maumivu yako na mambo ambayo hutaki kuyakumbuka

Epuka watu kwa kuhama eneo, mtaa, mkoa au hata nchi kama unaweza

Endapo kazi yako ni chanzo cha matatizo yanayokusumbua basi iache haraka sana

Na kama huwezi kuiacha na ndio tegemeo la kipato basi punguza muda wa kuwa kazini

Vile vile hakikisha ukiwepo eneo la kazi weka akili yako yote kwenye majukumu yako tu

Ukiweza badili kabisa namba ya simu yako umayotumia na usimpe mtu yoyote ambae hutaki tena kuwa karibu yake

Chukulia kama funzo na mpango wa mungu katika maisha yako yajayo

Ukitaka kusahau mambo ya nyuma basi usiyachukulie kama tatizo kwani utazidi kuumia zaidi

Badala yake jifunze kupitia changamoto hizo hizo ili kukufanya usirudi tena makosa siku zijazo, 

chukulia kama vile mungu amekuandalia kitu bora na  anataka kukupa uimara zaidi kwenye maisha yako ya baadae

Jiweke bize muda mwingi na tafuta muda mzuri wa kupumzika na kuwa peke yako ikibidi fanya sana meditation

Itakusaidia kusahau haraka mambo yote na kuanza upya kwani kutumia muda mwingi kuwa bize hukufanya kuweka akili kwenye jambo unalofanya na kukuhamisha kimawazo

Pia ukitumia muda mwingi peke yako hukusaidia kujijua zaidi na kuwaza maisha yako na kazi zako huku ukijiona mtu mpya na kufikiria umuhimu na thamani yako

Jiweke karibu na watu wenye mawazo Chanya na marafiki wapya pia Jaribu kufanya vitu vipya

Kuwa karibu na watu wanaowaza vitu Chanya husaidia kusahau mambo yako ya nyuma

Lakini pia marafiki wapya hukupa uzoefu mpya wa maisha

Usisite kujaribu mambo mapya yaliyo ndani ya uwezo wako hata kama ni mambo madogo madogo, itakufanya kugundua vitu ambavyo hukuvijua hapo kabla

Usilipize kisasi wala kushindana na mtu

Kamwe usifikirie kuwatendea mabaya waliokokesa hata kama makosa yalikuwa makubwa na yamekuharibu kabisa

Visasi haitokusaidia na badala yake utajikuta katika wakati mgumu zaidi ya mwanzo na hata kuharibu maisha yako yote kama vile kufungwa jela au kifo

Hivo ili kusahau haraka usifirikie kabisa kulipa kisasi chochote kile bali jipange upya na maisha yako ya mbele

Usizuie hisia zako (lia sana kama unataka kulia) Ondoa mawazo hasi na usiongelee tena mabaya ya nyuma

Kama ukihisi maumivu makali sana, tafuta sehemu ya peke yako na lia kwa uchungu wote

Kikubwa zingatia  ukimaliza kulia jiambie kuwa hutolia tena

Jitahidi kuondoa mawazo mabaya yote na usiongelee wala kufatilia mambo yako ya nyuma tena

Tafuta mtu wa kuongea nae ili kukuwezesha kusahau na kuanza upya

Angalia mtu mwenye busara na unaemuamini sana, kaa nae chini zungumza kila kitu na usifiche

Unaweza kutafuta watoa ushauri nasaha au mtu yoyote ambae huna mazoea nae wala hajui maisha yako ya nyuma

Ongea nae bila kuficha kwa lengo la kukupa ushauri zaidi, mbinu hii hukufanya ujihisi mwepesi na kukupa nafasi nzuri ya kusahau na kuanza upya 

Jipe muda zaidi na itakusaidia kupona, kusahau na kuanza upya

Muda ndio dawa nzuri sana na muda huponya maumivu yote na kukusahaulisha kila kitu cha nyuma,

Ikiwa umefata baadhi ya hatua hapo juu kulingana na aina ya matatizo yako basi ni wakati sahihi wa kujipa muda ili kila kitu kikae Sawa

Tambua kuwa kuna baadhi ya mambo huhitaji muda mrefu kusahaulika na mengine huchukua muda mfupi tu hivyo unapaswa kuwa na subra zaidi

Anza upya kufanya mambo mengine na kuishi maisha unayotaka

Baada ya kujihakikishia kuwa umepona na umesahau kwa kiwango kikubwa mambo ya nyuma

Sasa ni wakati sahihi wa kuanza kuishi vile ambavyo umekusudia na kufurahia maisha yako kama vile hakuna kilichotokea hapo kabla

Fanya vitu vyote bila kuogopa historia yako ya zamani na jione kuwa wewe ni mtu mpya 

Chukulia kama ndio kwanza umezaliwa upya pia historia yako imeandikwa upya

Weka nguvu katika biashara yako au kazi yako kwa kasi kubwa, tafuta mwenza mpya na mpende kama vile hujawahi penda hapo kabla

Endapo ni maradhi ya kudumu tumia tiba kwa usahihi na ishi kama vile huna maradhi yoyote ila fata tahadhari

Kama ulikuwa muasherati na mzinzi ishi kama vile umetakaswa upya na unaweza kuwa kiongozi mkubwa wa dini bila kuwaza mabaya ya nyuma

Hitimisho 

Hivyo basi, kaa ukijua kuwa chochote unachopitia au ulichowahi kupitia kuna watu wamepitia makubwa na Mazito kuliko hilo lako

waliamua kujikana na kukana historia zao na wakawaamua kusahau mambo yote na kuanza upya maisha yao 

Leo hii hakuna kumbukumbu yoyote inayowasumbua na wanafanya mambo makubwa sana

Hivyo hata wewe ukiamua unaweza na utakuwa mtu mkubwa na mwenye mchango Chanya katika jamii ukijikana na kukana mambo ya nyuma. 

Pia soma mafanikio

Share this article
Shareable URL
Prev Post

Namna bora ya kujenga heshima katika jamii

Next Post

Mbinu za kuacha tabia mbaya usiyoipenda 

Acha Comment Yako

Read next

Huruhusiwi ku copy. Asante.