You Can Win If You Want

Mbinu Rahisi Za Kufanikiwa Bila Kuchoka Sana7 Min Read

kufanikiwa bila kuchoka

Utangulizi

Kufanikiwa bila kuchoka sana sio jambo gumu ambalo linashindikana haijalishi unatafuta mafanikio katika kitu gani

Watu wengi sana wanaamini kuwa ili ufanikiwe basi lazima upitie mateso makubwa kwanza ya aina fulani kitu ambacho sio sahihi

Hii haimaanishi kuwa mafanikio ni jambo rahisi sana kwamba unaweza kufanikiwa bila mchakato fulani

Ila maana yake ni kuwa unaweza kufikia mafanikio unayotaka bila kuteseka wala kuumia zaidi kama inavyo aminika

Vile vile mafaniko sio jambo jepesi sana wala halipaswi kuwa gumu zaidi haijalishi ni mafanikio madogo wala makubwa.

mafanikio bila kuchoka sana
Photo by fauxels on Pexels.com

Hapa haijalishi ni mafanikio katika eneo gani yawe makubwa au madogo ya muda mrefu au mfupi kwenye maisha ya mtu

Kila mmoja huwa na malengo kwenye maisha yake ambayo hupambania kuyatimiza kila siku

Sasa kuna watu wengi wameaminishwa kuwa mafanikio yanataka kusota sana ndio uyapate bila hivo haiwezekani

Usisahau wakati huo huo kuna watu wanapata mafanikio makubwa bila kutumia nguvu nyingi sana wala kuteseka sana

Na wapo wanaopitia mateso mengi na wanapambana mno kwenye maisha yao ila bado wana hali ngumu sana.

Hapa tunaongelea mateso ya mwili na akili pia.

Kama Mafanikio Ni Kuteseka Sana Basi Watu Wengi Wangefanikiwa

Asilimia kubwa ya watu mjini na vijijini kila mmoja kwa wakati wake huteseka kupata aina fulani ya mafanikio

Lakini hakuna kinachopatikana zaidi ya vilio vya ugumu wa maisha miaka na miaka kwa watu wale wale

Wengi hufanya kazi ngumu sana kwa masaa mengi wakiamini ndio njia ya kupata mafanikio yao

Wapo wanaoamua kujiajiri au hata wale waajiriwa pia, Hufanya kazi kwa nguvu na masaa mengi bila mafanikio wanayotaka,

Furaha imekuwa hadithi kwao ,haiji kabisa na hata ikija haichelewi kuondoka kisa harakati za kusaka mafanikio hewa

Unakuta mpaka mtu huyu apate mafanikio basi ameshapitia mambo magumu sana na hata alikaribia kukata tamaa kabisa

Msoto wa kila siku unafanya watu wengi kuishia njiani na kukata tamaa mapema sana au hata kuamini kuwa mafanikio ni kwa ajili ya watu wengine

Miaka nenda rudi mtu anapambania jambo fulani lakini halipati zaidi ya kuishia kupata mateso na maumivu makali

Yaani kitu ambacho kilipaswa kupatikana au kutafutwa kwa furaha badala yake kinapatikana au kutafutwa kwa mateso

Mchakato wa mafanikio hupaswa kuwa wakufurahika sana kwa kila hatua unayopiga iwe nzuri au mbaya

Mungu hakuumba mtu aje kutafuta mafanikio kwa kupitia mateso, yaani Dunia sio uwanja wa kuteseka kabisa

Mateso yamesababishwa na watu wenyewe kwa kutoka nje ya utaratibu unaofaa kwenye utafuataji

Matokeo yake ndio imesabisha kuumia na kuumiza wengine kisa mafanikio ambayo kuna siku utaayacha Duniani.

Kwanini unapaswa Kufanikiwa Bila Kuchoka

Kivipi, uteseke kisa kitu ambacho huna uhakika wa kudumu nacho? Kwanini uumize wengine kisa vitu vya mapito?

Au kwa sababu gani ukose raha na amani kisa mafanikio ya jambo ambalo hata kama utalipata bado utaliacha

Mwisho wa siku KUFA ni kitu cha lazima haijalishi ulishinda vitu vingapi Duniani lazima utakufa tu

Maisha ni mafupi sana na bila kujali kiwango cha mafanikio yako lazima ufurahie maisha yako kwa namna yoyote ile

Wakati unafanya mchakato wa kufanikiwa pia lazima mchakato wako uambatane na furaha yako kamili

Dunia sio sehemu ya kuchukiza bila kujali changamoto ulizonazo bali Dunia ni sehemu salama na nzuri kwa watu wote.

Dalili Za Kupata Mateso Wakati Wa Kutafuta Mafanikio

  • Kuchoka sana
  • Hasira za mara kwa mara
  • Kuhisi hali ya kuchanganyikiwa
  • Kukata tamaa mara kwa mara
  • Kukosa usingizi mara kwa mara
  • Kupoteza uhusiano na watu wa karibu
  • Ubize uliopindukia na kukosa muda wa kupumzika kabisa
  • Ukosefu wa hamasa mpya
  • Kupata hali ya majonzi kila wakati
  • Kuhisi kujuta mara kwa mara
  • Msongo wa mawazo uliopitiliza
  • Hasara za mara kwa mara na kupoteza vitu vya msingi bila kutarajia

Sio kama kupata mafanikio ni rahisi na hauwezi kupitia haya yaliyotajwa hapa juu hapana

Ila angalau kwa asilimia chache mchakato wa mafanikio hupaswa kuwa mwepesi na rahisi.

Sababu Za Kuteseka Wakati Wa Kutafuta Mafanikio

  • Kufanya na kutumia nguvu kubwa kwenye kitu usicho kipenda kutoka moyoni
  • Kutafuta mafanikio nje ya nyakati sahihi
  • Kulazimisha kitu usicho kiweza
  • Kuwekeza kwenye kitu nje ya kusudi la kuumbwa kwako
  • Kufanya jambo nje ya maana halisi ya maisha yako
  • Kukosa sababu za msingi za dhati kwenye kitu unachokifanya
  • Ukosefu wa malengo na dira sahihi

Mambo Ya Kuzingatia Kama Unataka Mafanikio Bila Kuchoka Sana

Kama unatamani kuyaona mafanikio yako bila kuchoka sana au kupata aina nyingi za mateso mambo haya yanaweza kukusaidia

  • Soma alama zako za nyakati, sio kila nyakati ni sahihi kufanya jambo fulani hata kama una lihitaji sana kwasababu kila mtu ameumbwa na nyakati tofauti tofauti ambazo ndio humsaidia kupata kitu anachotaka bila kuchoka sana
  • Fanya kitu unacho kipenda sana, kitu ambacho kipo ndani ya moyo wako bila kuhitaji msukumo wa nje wowote wakati wa kukifanya au kukitekeleza
  • Angalia kitu unacho kiweza zaidi, kile ambacho hata ukiamshwa usingizini bado unaweza kufanya bila kuumiza kichwa wala kuhitaji kukumbuka sana
  • Chunguza kusudi lako la kuumbwa kisha tafuta mafanikio yako kupitia kusudi hilo la kuumbwa kwako
  • Kwenye kila unachofanya weka malengo ya wazi kwanza kabla ya kutumia nguvu kubwa ukiweza maliza utekelezaji ndani ya akili kwanza kabla ya vitendo
  • Beba sababu zenye uzito wa wazi zinazo sababisha ufanye au utafute mafanikio yako ili kujenga hali ya hamasa mara kwa mara ndani yako.
mafanikio bila kuchoka sana
Photo by god picture on Pexels.com

Hatua Muhimu Zaidi Kwa Kila Anaetaka Kufanikiwa Bila Kuchoka Sana

  1. Chagua kitu sahihi unachotaka kufanikisha

    Hapa zingatia kile unachokipenda au kukiweza sana bila kusahau alama zako za nyakati

  2. Chunguza changamoto zikubali na zipokee

    kabla hujaanza utekelezaji elewa changamoto za kitu hiko kwanza zikubali kwa moyo mmoja na zipokee kisha tafuta njia ya kukabiliana nazo

  3. Weka malengo makubwa kwenye kitu unachotaka kufanikisha

    Usiogope kujenga picha kubwa akilini mwako haijalishi udogo unao anza nao

  4. Vunja vunja malengo yawe madogo madogo

    Yale malengo yote makubwa kwenye mafanikio unayotaka yavunje sasa ili upate urahisi wa utekelezaji kwanza

  5. Weka mipango madhubuti

    Zingatia mipango sahihi iliyo ndani ya uwezo wako na kamwe usilazimishe kutoka nje ya uwezo hasa katika hatua za mwanzo

  6. Anza utekelezaji kidogo kidogo

    Usiwe na haraka kabisa hata kama unaona njia ni nyepesi mbele yako yaani fanya kwa mwendo wa taratibu lakini hakikisha hukosei sana na ukikosea rekebisha kosa

  7. Fanya kwa mazoea

    Ule utekelezaji mdogo mdogo sasa ufanye kwa mazoea kila wakati na kila siku yani iwe sehemu ya maisha yako

  8. Usitumie nguvu kubwa

    Acha mipango uliyoweka ikuoneshe njia kupitia hatua ndogo ndogo unazofanya mara kwa mara kila siku

  9. Jifunze zaidi

    Kwa kila hatua unayopiga tafuta namna ya kuongeza maarifa ili kabla hujaenda hatua nyingine uwe na uhakika kuwa hukosei

  10. Rekebisha makosa

    Kila unapoona unakosea haraka rekebisha na anza upya tena yani usiende haraka huku unafanya vitu tofauti

  11. Pumzika na furahia mafanikio madogo madogo

    Ukihisi kuchoka sana acha na weka pembeni kwanza vuta pumzi mpya kisha rudi tena na ukiona umefanikiwa hata kama ni kakitu kadogo basi haraka jipongeze kwanza.

Maswali Yanayo Ulizwa Mara Kwa Mara

Je, naweza kufanikiwa hata bila kuchoka zaidi?

Ndio inawezekana kabisa unapaswa kutumia akili zaidi na nguvu kiasi wakati unatafuta mafanikio yako

Je,naweza kupata mafanikio makubwa kwa kuanza bila kitu?

Ndio unaweza kufikia mafanikio makubwa yoyote unayotaka bila kuwa na kitu chochote zaidi ya nia ,jitihada na mikakati thabiti

Kwanini watu wengi huishia njiani?

Ni kwasababu ya kufanya mambo nje ya utaratibu sahihi uliowekwa kwenye asili ya mtu husika au hata nje ya nyakati za mafanikio hivyo huchoka mapema

Je, ninaweza kupata mafanikio nikiwa ndani?

Unaweza kufanikiwa hata kwa kufanya kazi kwa njia yoyote na kupata mafanikio hutegemea na aina ya kitu unachofanya bila kusahahu mipango na maandalizi ya awali sio lazima ufanye kazi za nje pekee

Hitimisho Kwenye Kufanikiwa Bila Kuchoka

Kutafuta mafanikio bila kuchoka sio suala linalo ambatana na uvivu kabisa bali hali ya kuleta uwiano sawa wa maisha na mafanikio

Hupaswi kuteseka kisa mafanikio unayotaka na mafanikio sio jambo lenye kuumiza au kulazimika sana kufanyika

Endapo unaona unateseka badala ya kufurahia unachofanya sio dhambi kupumzika kwanza na ukiona huwezi kabisa basi badili njia zako.

Share this article
Shareable URL
Prev Post

Namna Ya Kupanga Malengo Ya Biashara5 Min Read

Next Post

Namna Ya Kufanya Maamuzi Sahihi7 Min Read

Comments 8
  1. 🔥🙏

    Kama upuo uwezekano madam uanzishe ka masterclass kuhusu haya mambo ya mitaji na biashara kujiajiri ikibidi. Au na wewe haufundishi? (Private Lessons)

  2. Nimeanza mambo za Graphics Design bila mtaji kabisa ilikua mimi na laptop yangu tu nakumbuka software ya Photoshop nlipewa na Kainetics 2021 huko haha. Haya maisha bhana, thanks for this 🙏

  3. Mimi kukutana na hii post nadhani nadhani ndo alama za nyakati zenyewe kuniambia huu ni wakati sahihi 💯💯
    Hopefully nitakua na mrejesho wangu someday hapa.

  4. Kuna hii point ya kuwekeza kwenye kitu kilicho nje ya kusudi la uumbaji wangu. Hii imenichanganya kidogo, hili kusudi nalijuaje madam?

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Read next

Huruhusiwi ku copy. Asante.