You Can Win If You Want

Namna Ya Kubadilisha Maisha Milele8 Min Read

kubadili maisha

Utangulizi

Kubadili maisha milele ( Kuishi maisha mazuri zaidi yenye mafanikio) ni ndoto ya kila mtu Duniani ila wachache sana hufanikisha

Kila mmoja kwa namna yake hutamani kubadili maisha aliyonayo na kufikia hatua za juu zaidi kuliko alivyo au anavyo jiona sasa.

Wengi sana huishia kwenye matamanio tu akilini lakini hushindwa kabisa kuingia kwenye uhalisi wa nje na vitendo,

Kubadili maisha sio jambo kubwa sana kama wengi wanavyo dhani haijalishi mtu hutaka mabadiliko eneo gani.

Hakuna jambo lisilo wezekana chini ya jua, jitihada na subra ndio hufanya jambo liwe gumu sana au jepesi zaidi.

Kila mmoja ana malengo na ndoto zake hususani eneo la kipato na mabadiliko ya mzunguko mzima wa maisha yake,

Kupiga hatua kutoka sehemu moja kwenda nyingine na kuwa bora zaidi ni ndoto ya kila mtu Duniani kila mmoja kwa namna yake.

Wachache huweza kufikia ndoto hizi bila vizuizi vingi na wengi hukutana na changamoto mbali mbali na hata kukata tamaa kabisa.

Kubadili maisha ni pamoja na kufungua mlango wa maisha mapya na kufunga mlango wa maisha ya zamani,

Kisha kutupa kabisa funguo za maisha ya zamani kwani hazina faida wala uhitaji tena kwenye maisha mapya.

crop woman with dry leaf and plant seedling
Photo by Olha Ruskykh on Pexels.com

Maana Ya Kubadili Maisha

Kila mmoja ana maana au tafsiri yake ya kubadili maisha kulingana na ndoto au malengo aliyonayo kwenye maisha yake

Ila kwa ujumla kubadili maisha kwa namna inayoongelewa hapa ni kubadili au kuboresha maisha ya zamani kuwa na thamani zaidi,

Ikiwa na maana kuwa maisha aliyo nayo mtu husika ,kuyafanya yaongezeke thamani kwa kuambatana na malengo aliyonayo.

Malengo ni dira ya maisha ya mtu hivyo kutimiza malengo ni sawa na kubadili maisha ya nyuma na kuwa ya thamani zaidi

Haijalishi kwenye eneo gani, hakuna mtu ambae hutamani kubomoa maisha yake au kushusha thamani ya maisha yake.

Watu wote hupambana usiku na mchana kwa lengo la kuyapa thamani maisha waliyonayo ili kuwa bora zaidi.

Hakuna Anae Penda Kurudi Nyuma

Kwenye maisha hakuna mtu apendae na kufurahia maisha yake kushuka thamani, kufirisika au hata kuwa mabaya,

Japokuwa malengo hutofautiana kati ya mtu na mtu lakini kwa namna ya kupanda na kufika mbali zaidi na sio kushuka chini zaidi.

Hivyo basi tunapo zungumzia kubadili maisha ,maana nzima ni kutoka hatua ndogo na kupanda hatua kubwa,

Au kuhuisha maisha ya nyuma na yale ya sasa ili kuwa maisha bora zaidi yajayo kwenye eneo lolote kupitia malengo.

Kujua kuhusu malengo na njia za kufanikisha malengo yako soma hapa.

Kubadili Maisha Inawezekana

Haijalishi kwa sasa uko wapi na unafanya nini, wala haijalishi unataka kuwa nani na kutimiza nini ,elewa kuwa inawezekana

Hakuna jambo lisilo wezekana kabisa ila tu njia za kufikia lengo huweza kuwa na changamoto kadhaa baina ya mtu na mtu.

Chochote kinacho wezekana akilini basi pia huwezekana kwenye maisha halisi

Kama akili yako inaweza kuwaza na kuona jambo fulani linawezekana, basi elewa kuwa ni kweli linawezekana,

Akili haiwezi kuwaza isichoweza kutenda kamwe na mtu huwaza kadiri anavyoweza kutenda kwa nje kupitia akili yake.

Ndio maana kila mmoja ana mawazo yake au hata utendaji wake na watu hawafanani hata kimalengo au kusudi la kuumbwa

Hivyo uwazavyo wewe ni tofauti na mimi au hata mwingine yoyote na kila akili au mawazo huwaza kile iwezacho kukitenda.

Usimshangae mtu mwenye kila kitu na bado hawezi kufanya chochote kwa sababu akili yake haioni vile alivyo navyo,

Kama akili ikiwa kipofu kuona au kuwaza basi ukweli ni kuwa hata utendaji wa mtu pia huwa mgumu na kamwe hatoweza kufanya kitu.

Ndio maana siku zote binafsi nina amini kuwa hata umasikini huanzia akilini.

namna ya kubadili maisha
Photo by Mikhail Nilov on Pexels.com

Kama Kweli Unaamini Kufanikiwa Kupitia Maombi Basi Omba Mungu Akupe Akili

Akili ndio imebeba kila kitu kuanzia uhalisia wa nje wa maisha ya mtu na utendaji wake kwenye kila kitu,

Ukiwa na akili ya kutatua changamoto basi kila jambo utaona jepesi sana na hata kuishi kwa amani sana

Kupitia akili ndio tunapata matokeo yote ya vitendo vya watu kwenye maisha yao kwa maana kuwa kila mtu hutenda sawa na akili yake.

Badala ya kukesha kuomba Mungu kazi, wateja, pesa, nyumba NK nadhani maombi mazuri zaidi ni kuomba kupewa akili,

Mungu akikupa akili nzuri basi maisha pia huwa bora sana na vingine vyote unaweza kuvipata kupitia akili yako

Na kama utapata vitu nje ya akili yako basi vinaweza kupotea mara moja kwa maana kuwa hutaweza kuvitunza au kuviendeleza kamwe.

Utajiri Wa Kwanza Ni Akili

Kwenye kubadili eneo lolote la maisha, kitu cha msingi zaidi ni akili iliyo timamu na yenye uwezo mzuri wa kufikiri,

Akili inayoweza kuchanganua baya na zuri bila kusahau akili inayoweza kupanga mipango na mikakati imara.

Maisha yanataka akili zaidi kuliko nguvu nyingi.

Mabadiliko Huja Kwa Wanaotaka

Ukweli ni kuwa mabadiliko hayalazimishwi kamwe bali huja kwa yule anae yahitaji pekee kwa juhudi zake,

Huwezi kumlazimsha mtu abadilike hata kama mabadiliko hayo yana faida sana kwake au kwako na hata kwenu wote!

Kubadilika ni suala la mtu binafsi na matakwa yake yeye mwenyewe kwa namna atakayoona inafaa zaidi au kwa wakati sahihi zaidi.

Hivyo kuleta mabadiliko kwa wengine basi yafaa zaidi kuanza na wewe mwenyewe ambae kwa sasa umeamua kubadilika.

Hatua Za Kubadili Maisha

  1. Badili namna unavyo fikiri

    Hii ni hatua ambayo haikwepeki kwa gharama yoyote ile kwani akili ndio kizuizi cha kwanza kwenye maisha bora

  2. Fanya tathimini ya maisha yako ya sasa

    Kwa maana ili uweze kugundua kwanini unataka kubadili maisha uliyonayo na kuwa na maisha mengine au mapya

  3. Jua unachotaka kwa dhati (malengo)

    Huwezi kubadili maisha kama hujui hasa unataka nini au mabadiliko katika eneo gani kwenye maisha yako

  4. Andika unachotaka kwenye daftari (malengo mapya)

    Usijiongopee kabisa na kuwa muwazi kwenye nafsi yako au malengo yako kwa dhati kabisa

  5. Weka nia ya dhati

    Nia huamsha hamasa ya ndani na kuleta nguvu kwenye mchakato mzima wa kubadili maisha

  6. Jenga imani kubwa

    Imani ni ufunguo wa kwanza unaofungua mafanikio ya jambo lolote lile hivyo kuweza kuona mafanikio haraka basi imani haikwepeki

  7. Weka mikakati na mipango imara

    Kupitia kile unachotaka kubadilisha kwenye maisha yako basi lazima kiwe na mikakati dhabiti sana inayo toa dira sahihi

  8. Anza utekelezaji kwa hatua ndogo ndogo

    Baada ya kuwa na mipango sasa ni kuingia kwenye utekelezaji kwa vitendo bila hofu wala uoga na wala usiwe na haraka sana kwasababu utachoka mapema

  9. Usirudi nyuma

    Haijalishi changamoto na vikwazo kamwe usiguke nyuma hata iweje ,zingatia kufikia kile unachotaka pekee

  10. Kuwa na subra au uvumilivu

    Hakuna mabadiliko ya siku moja na mwazo huwa mgumu sana ila taratibu mazoea hufanya urahisi na mwisho matokeo chanya.

Mambo Mengine Yanayo Saidia Kubadili Maisha Milele

Haya ni mambo mchanganyiko yanayo saidia kubadili maisha milele kwenye jambo lolote kupitia malengo ya mtu

  • Kuwa na bajeti mpya yenye uhalisia kulingana na kipato
  • Kufanya mazoezi ya viungo vya mwili mara kwa mara
  • Kuamka asubuhi sana na kuanza majukumu mapema husaidia akili kuwa makini (active)
  • Kusoma au kujifunza vitu vipya vinavyojenga zaidi akili
  • Kubadili muonekana na mavazi ya awali
  • Kujifunza ujuzi mpya na kuufanyia kazi
  • Kuwa na marafiki wapya wanao endana na aina ya maisha mapya unayotaka
  • Kujenga tabia mpya nzuri na inayo vutia zaidi kulingana na malengo husika NK
a woman sitting on a chair surrounded by cardboard boxes
Photo by RDNE Stock project on Pexels.com

Mambo Ya Kuzingatia Wakati Wa Kubadili Maisha

  • Epuka kabisa makundi au urafiki na watu wa zamani ambao wanafanya yale ambayo unataka kuyabadilisha
  • Shukuru mara kwa mara kwa kila hatua unayopiga na kujipa moyo kila saa kuwa inawezekana
  • Fanya tahajudi mara kwa mara
  • Kula mlo kamili na chakula chenye afya na kunywa maji mengi
  • Epuka kabisa hali ya kukata tamaa maana safari ya mabadiliko sio rahisi kabisa na kuna muda utatamani kuacha na kurudi kule ulipotoka
  • Usijilinganishe na waliokuzidi au kukutangulia na ukiweza fanya kama huwaoni
  • jifunze kupitia makosa unayofanya na rekebisha ili kuwa bora zaidi
  • Kufanya tathmini ya malengo na hatua ulizopiga mara kwa mara ili kugundua kama unaenda mbele au unarudi nyuma
  • Jipongeze kwa jitihada na juhudi unazopiga kila wakati
  • Usikubali roho ya kuacha ,kupunguza hamasa wala kuchelewa kufanya kwa vitendo ni bora kupumzika unapozidiwa ila sio kuacha kabisa.

Hitimisho

Kwa ujumla mambo yote hayo yanasaidia sana kubadili maisha ya mtu kulingana na aina ya malengo aliyo nayo mtu husika

Jitihada ni muhimu sana kwani safari ya mabadiliko sio safari nyepesi kabisa japokuwa inawezekana kwa mtu yoyote

Changamoto kama kutengwa, kupoteza marafiki na hata upweke haviepukiki kamwe muhimu ni kukaza roho.

Inaweza chukua miaka au miezi kadhaa kuzoea mabadilio mapya na wengine hushindwa na kuishia njiani

Muhimu ni nia ya dhati na subra kwani kuna siku utajishukuru kwa maamuzi uliyofanya.

Share this article
Shareable URL
Prev Post

Wazo La Biashara Ya Pizza6 Min Read

Next Post

Mambo 30 Madogo Madogo Na Mepesi Yanayo Saidia Kubadili Maisha Milele6 Min Read

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *

Read next

Huruhusiwi ku copy. Asante.