You Can Win If You Want

Umasikini Huanzia Akilini

Umasikini huanzia akilini

Umasikini huanzia akilini kwa maana kuwa akili ya mtu ndio chombo kikubwa kinacho ongoza maisha yake kwenye maamuzi, uchaguzi na hata utendaji wa kila kitu

Ukiona mtu ana maisha mazuri basi ujue akili yake ndiyo haswa ilimfanya akaweza kuwa na kila alichonacho

Na ukiona mtu masikini pia jua kabisa hakuna kurogwa wala laana yoyote bali akili yake ndiyo imemuweka katika maisha aliyonayo

Kimsingi ugumu au ulaini wa maisha upo katika uchaguzi wa mtu binafsi kupitia akili yake

Yaani ukiwa Masikini ujue umechagua kuwa masikini na ukiwa Tajiri pia ni ukweli kuwa umechagua Utajiri.

man lying on barricades
Photo by abhishek goel on Pexels.com

Umasikini Huanzia Akilini Kutokana na Uchaguzi Wa Mtu

Kila mmoja hutafsiri mafanikio kwa namna yake na kila mtu huamua kuchagua aina ya maisha anayotaka kupitia akili yake

Wote tulipewa akili sawa ukiondoa utofauti wa Rangi, Mipaka ya nchi na Maumbile

Hakuna aliyepewa Akili nyingi kuliko mwingine isipokuwa kwa wenye maradhi maalumu ya akili

Kinacho tutofautisha ni matumizi ya akili zetu ,na kila mtu huamua kutumia akili yake kwa namna anavyoona kwake inafaa

Na kisha akili huzalisha matokeo ya nje kwa kile kinacho amriwa na mtu husika kupitia akili ya ndani

Hapa duniani kila kitu kilichopo yani ukitoa vitu asili visivyo tengenezwa na Binaadamu kama Bahari , milima ,mito ,maziwa ardhi ,mbingu nk

Vilivyobaki vyote vimetengenezwa kupitia akili za watu mfano vyombo vya usafiri, nyumba, viwanda,bidhaa zote,mavazi,burudani nk

Kwahio Akili huanza na wazo kisha utekelezaji wa nje na Akili inauwezo wa kuunda kitu kabla ya uumbaji halisi wa nje

Kama akili haitaweza kuunda kitu kwa ndani basi kamwe kitu hiko hakita wezekana kutengenezwa kwa nje

Hivyo basi kama vitu vyote huumbwa kwa kuanzia akilini au akili ndio chombo cha uumbaji wa awali basi pia Umasikini huanzia akilini.

Akili Yako Ndio Chanzo Cha Umasikini Wako

Hakuna mtu aliyeletwa Duniani kwa lengo la kuteseka kamwe na hakuna ambae anateseka kwa sababu Mungu ametaka ateseke

Mateso yote na ugumu wa maisha husababishwa na matumizi ya akili ya muhusika mwenyewe

Namna unavyowaza na kuchagua vitu kupitia akili kwa ndani ndivyo namna akili huzalisha matokeo kwa nje!

Chochote unachoamini au unachochagua kupitia akili yako ndivyo ambavyo utapata matokeo hayo hayo kwa nje kwenye mazingira halisi.

close up of blue paint
Photo by Nikolai Ulltang on Pexels.com

Ukijiona huwezi kufanya kitu fulani kuanzia akilini basi ujue pia hutoweza kukifanya kwa vitendo katika mazingira halisi

Ukiona jambo fulani ni zito basi ukweli utaona uzito hata kama jambo linawepesi ndani yake

Kama kitu kikiwa kigumu na kizito sana kwa nje lakini kwenye akili yako ukihisi kuwa unaweza kukifanya basi lazima utajikuta kweli umekiweza na umekifanya

Yani akili hutoa njia pale tu ambapo imeruhusiwa kutoa njia kupitia muhusika na akili huacha kufanya kazi ikiwa muhusika hatotaka ifanye kazi

Kiufupi akili inatenda kupitia maagizo ya mtu binafsi anapo iamrisha itende na wala Akili haitotenda kama isipotakiwa kutenda.

Namna Akili Inavyoleta Umasikini

Kama tulivyoona kuwa umasikini huanzia akili sasa tuangalie kwa namna gani akili ni chanzo cha umasikini

Kwa maana kuwa karibu kila mmoja au asilimia 98% ya watu wote huwa na malengo ya kufanikiwa lakini asilimia chache sana huweza kutimiza lengo la kufanikiwa

Utofauti wa waliofanikiwa na ambao hawaja fanikiwa upo katika matumizi ya Akili zao pekee ijapokuwa wote wanaweza kuwa na malengo yanayofanana.

Namna ambavyo utajiona kwa ndani na kujenga picha kisha kuweka imani ya kitu ndivyo hivyo hivyo Akili yako itakupa matokeo unayotaka

Kiufupi ni kuwa maisha yako ya nje yameumbwa na wewe mwenyewe kuanzia akilini mwako!

Tofautisha akili ya darasani na akili ya utendaji wa mambo katika maisha

Unaweza kuwa na akili nyingi sana za Darasani lakini ukashindwa mafanikio na mtu ambae hajasoma kabisa

Ndio maana kuna wasomi wengi sana leo hii ambao wanatumikia watu ambao hawajasoma kabisa na wameshindwa kabisa kutumia Taaluma zao kuingiza pesa

Yani Elimu haina uhusiano wowote na mafanikio kimaisha na wala kusoma sana sio chanzo cha kupata maisha mazuri

Zaidi naona kusoma sana ni chanzo cha umasikini , kuongeza hofu ya kupambana na maisha, na kujiweka katika nafasi ya kuwa mtumwa wa wengine.

Ikiwa utaona Biashara ya maandazi ina faida na ukaamua kuifanya katika ubunifu mkubwa basi lazima kweli utapata mafanikio

Na ukiona maandazi hayo hayo hayana maana wala hayawezi kukufanisha kimaisha basi ni kweli itakuwa hivyo na utayadharau na hata kudharau wano uza maandazi

Fikiria huna mtaji wala pesa za matumizi ila unaona aibu kufanya kazi kutumia nguvu hata kama ina malipo kidogo kisa Elimu yako

Au unaona huwezi kuanza biashara kwa mtaji wa elfu 50 na ukaamua kununua kitu cha anasa cha hio pesa

Kisha ukarudi kusema maisha magumu na kulalamika kwa Mungu kuwa amekuacha kwa kukesha kwenye maombi kila siku!

Hapo pia utasema umerogwa? au ni matumizi mabaya ya akili?

Upo na simu janja kubwa nzuri na una taaluma fulani au kipaji ila unaamua kuitumia kufatilia umbea na mpira mitandaoni

Yani umeshindwa kabisa kutumia hio simu na vocha yako kuuza ujuzi wako na kupata pesa !

Umasikini Huanzia Akili Kama Hivi:

Umekaa ukaona ndani ya akili kuwa huwezi kufanya chochote kabisa kisha ukaona njia nzuri ni kutumia mwili wako kupata pesa

Unaamua kushusha thamani ya mwili wako kwa kuutumia kujiingizia kipato kwa hao Mababa au Mashangazi

Huku ukiamini kuwa bila kufanya hivyo hutoboi

Unasahau kuwa mafanikio haya ambukizwi kwa ngono! ila unaweza kuwa na uhakika wa kuambukizwa maradhi!

Huo muda wa kuangaika kuwa mtumwa wa mtu mwingine kisa pesa zake pengine ungeweza kuutumia kwa kuuza hata genge na ungefika mbali

Tuseme chanzo ni mtaji lakini ukiangalia vitu unavyomiliki kuanzia mavazi,simu ,thamani za ndani nk ni zaidi ya mtaji unaotaka!

Au kama kweli unafanya hayo kwa sababu ya mtaji sasa kwanini bado unayafanya kwa zaidi ya miaka kadhaa na hatuoni mabadiliko?

Yani umeshindwa kuogopa maradhi kama HIV nk ila unaogopa kuuza simu kufanya biashara ,

Kisa kukosekana hewani kufatilia umbea na vitu visivyo na faida katika maisha yako huku ukitumia vocha kila siku

Hapo pia utasema umerogwa au shida ipo ndani ya akili yako? mbaya zaidi kila siku unaenda kwa Mwamposa kukesha na kununua maji ya upako.

Hakua Uchawi wala Kurogwa

Ndugu zangu shida sio kurogwa wala kulaaniwa au hata sio kuwa Mungu hajakuona au labda mafanikio yapo kwa ajili ya watu fulani

Bali shida ipo ndani ya akili, namna ya kutazama na kuchukulia vitu na namna unavyo amini mambo kuanzia akilini mwako.

Ukiamini umerogwa utaona kweli kila aina ya dalili za uchawi hata kama hujarogwa

Vile vile ukiamini unaweza hata kama huwezi kwa muonekano wa nje utashaaga kweli umeweza

Uchawi wa kwanza ni akili yako kwahio anza kujiagua akilini kabla hujaoga dawa za masangoma.

Kila Unachofanya Ujue Umeweka Mkataba Nacho Kuanzia Akilini

Maamuzi yako yote na uchaguzi wa kila unachofanya ujue tu umeweka mwenyewe mkataba kuanzia ndani ya akili yako

Hapa namaanisha kila jambo linalo husiana na wewe iwe ulilichagua au umechaguliwa ikiwa tu unahusiana nalo basi ndio mkataba wako

Mfano ugumu wa maisha yako au kazi unayofanya na hata maisha unayoishi kila siku

Ni mkataba ulio saini mwenyewe kuanzia ndani ya akili yako mwenyewe

Ajabu huja pale unapolalamika kila mara kuwa hukipendi hiko kitu wakati muda huohuo bado umekikumbatia na wala hujafanyi mabadilko yoyote

Kiufupi maamuzi ya kubadili maisha yako unayo mwenyewe ndani ya akili yako

Na ukiona maisha hayabadiliki ujue hujataka kubadili akili yako wewe mwenyewe.

Naposema mkataba simaanishi mkabata wa makaratasi bali hapa naongelea uchaguzi wa jambo kupitia wewe na akili yako

Ukichagua kitu maana yake umechagua kuweka mkataba nacho ndani ya akili yako na ndio maana halisi ya neno kuwa umasikini huanzia akilini.

Na akili itakupa matokeo hayo ambayo umeyataka mwenyewe yani kama unataka mababa au mashangazi utapata njia ya kuwapata sana tu

Utajikuta akili inakuonesha njia na mbinu za kuwavutia kila mara maana ndio mkataba wenu ulipo.

Ukitaka kuona fursa za bila mtaji pia akili itakuonesha kila aina ya fursa na utajikuta kila siku unapata mbinu mpya za kitu cha kufanya kujikwamua

Na hata chochote kile unachotaka akili yako ipo kukupatia ila tu lazima uweze kuitumia na kuifanya itende vile unataka kupitia imani uliyonayo juu ya kitu husika.

Akili Inazalishaje Umasikini?

Ndani ya akili hupelekea kuzalisha vitu vifuatavyo ambavyo ni chanzo kikubwa cha umasikini

  • Uvivu
  • Ujinga
  • Imani potofu
  • Utegemezi
  • Umimi
  • vikwazo na aibu
Uvivu

Uvivu huanzia ndani ya mtu na hakuna ambae aliumbwa kuwa lege lege au kuwa imara ukiondoa sababu za maradhi

Uimara na ulegevu ni matokeo ya uchaguzi wa mtu binafsi kupitia akili yake na namna anavyoona na kuyachukulia mambo

Uvivu ni sababu kubwa umasikini kwa hali zote yani hapa naongelea uvivu wa kufikiri na hata ule wa kutenda.

Ujinga

Ujinga huja ndani ya mtu binafsi kupitia akili yake na suala la kuwa mjinga ni maamuzi ya mtu husika

Wala siongelei ujinga wa Darasani bali ujinga unaweza kuwa wa aina nyingi kama vile kutokujua kitu chochote

Unaweza kuwa na akili au elimu kubwa lakini ukawa mjinga kwenye mambo mengine ambayo huyafahamu

Kuwa mjinga sio kosa bali kosa huja pale umegundua ni mjinga na bado usitake kubadilika na wakati huo huo ni mabadiliko yenye faida katika maisha yako.

Imani potofu

Kama vile kujichukulia dhaifu na huna maana yoyote, kujiona huwezi kupata mafanikio, kujihisi umerogwa kila mara au hata kujiona umelaaniwa

Pale ambapo kila saa unajinenea mambo mabaya na kuona kama waliofanikiwa wana nafasi ya kipekee katika dunia ambayo wewe huna.

Utegemezi

Ndio pale watu wengi sana hujiona bila msaada wa wengine hawatoweza kufanikiwa

Na huwa sababu ya kufanya mambo mengi mabaya huku wakinyenyekea na kuteseka kwenye maisha ya wengine kwa kuamini kuwa peke yao hawawezi.

Umimi

Mwanzo wa kujilimbikizia mali na kula Rushwa huanzia hapa ,wengi huamini katika uchoyo na uroho huku wakisahau kuwa hayo yote sio sababu ya mafanikio ya kweli

Nchi za wenzetu wanaamini katika kuinuana na hata nchini Tanzania WACHAGA wamekuwa mfano bora sana wa mafanikio kupitia kusaidiana.

Vikwazo

Vikwazo kama vile kutafuta sababu za kutofanya kitu mara kwa mara kwa visingizio visivyo na tija yoyote

Ndani ya akili ya mtu huweza kuzalisha vijisababu vingi ambavyo havina mashiko yoyote ili mradi tu kupata ushindi wa ujinga wake

Na kusahau kuwa mafaniko huja katika kujitoa muhanga na kuacha kuhesabu sana vikwazo au changamoto zilizopo.

Utawezaje Kuondoa Umasikini Kupitia Akili?

Kuna mbinu moja tu kubwa ambayo husaidia kuondoa umasikini akilini nayo ni

BADILI NAMNA UNAVYO FIKIRI

Ukibadili namna unavyo fikiri utabadili maisha yako yote

Hio ndio njia kubwa na nzuri ya kwanza kama unataka kuondoa umasikini katika maisha na mateso ya kila siku

Unapaswa kwanza kujua kuwa chanzo cha umasikini wako ni Akili yako na kuweza kutibu akili ni kuibadili namna inavyofanya kazi

Kwa kuilazimisha akili ikupe mbinu na njia za kujikwamua kwa lazima bila kutumia nguvu kubwa wala mateso

Ukiweza kuanza kuchukulia maisha kwa utofauti basi pia utaweza kuona mabadiliko ya maisha yako vile vile unavyotaka.

Badala ya kuona huwezi weka neno inawezekana

Ukibadili namna unavyo fikiri kila kitu kitabadilka kwenye maisha na utaona kila jambo lina njia na utatuzi rahisi maana akili itakupa imani na imani itaunda njia.

brown field and blue sky
Photo by Pixabay on Pexels.com

Kwanini Watu Wengi Hawafanikiwi?

Jibu ni rahisi tu kwasababu wamechagua kutokufanikiwa kupitia akili zao na kutaka mafanikio rahisi kwa njia za mkato bila mikakati na malengo ya muda mrefu

Ijapokuwa tunaona kila mtu yuko na harakati za kupambana na umasikini lakini zote huwa ni harakati zisizo na matunda yoyote

“Wazungu wanaita busy for nothing”

huku wakiamini kuwa bila kufanya sana kazi huwezi fanikiwa na kusahau kuwa mafanikio pia huambatana na matumizi sahihi ya akili.

Hitimisho

Haya maisha kila mtu amekamilika kwa package kamili ukiondoa tofauti za maumbile

Hakuna ambae hana masaa 24 , wala mwenye kupumua pumzi tofauti na Oksijeni au ambae hana damu maji au nyama mwilini

Viungo vya kawaida vipo sawa na ndivyo akili ipo sawa ila matumizi ndio tofauti kulingana na matakwa ya mtu.

Badili leo maisha yako kwa kuanza kubadili akili yako ili kuona mafanikio ya kweli kwenye maisha.

Share this article
Shareable URL
Prev Post

Ukitafuta Maisha Usisahau Kuishi

Next Post

Kama Huwezi Kufanya Mambo Makubwa Fanya Mambo Madogo Kwa Ukubwa

Comments 2

Acha Comment Yako

Read next

Huruhusiwi ku copy. Asante.